Ukiondoa malalamiko yake binafsi, ukweli mchungu aliouongea Mbowe jana ni "tunaongozwa na wabunge ambao hatukuwachagua"

Ukiondoa malalamiko yake binafsi, ukweli mchungu aliouongea Mbowe jana ni "tunaongozwa na wabunge ambao hatukuwachagua"

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Jambo la msingi nililoliona kwenye hotuba ya Freeman Mbowe jana ni ukweli kwamba tunaongozwa na wabunge ambao hatukuwachagua.

Kwa mfano Babu Tale Kigwangalla, January nk nk walipigiwa kura na nani hadi wakafika bungeni.

Kadhalika wakurugenzi ambao ni makada wa CCM ndio wasimamizi wa uchaguzi, hapo mshindi anajulikana kabla ya uchaguzi.

Mengine aliyoongea ya ukabila na ukatili msingi wake uko ndani ya vyama vyote vya siasa, na huko serikalini vimepelekwa na wanasiasa

Ukatili unaanzia kwenye makundi kama Green guards, red nini sijui, blue....nk nk

Hilo la kufungiwa akaunti na TRA siyo jipya mzee Hashimu Rungwe akiwa NCCR alifungiwa account zote na kampuni yake ya kuuza magari kufilisiwa ikiwa na magari kibao yard na bandarini. Nadhani bwashee Mrangi wa Ufipa unaikumbuka Bahari Motors ya Spunda!

Niishie hapo.
 
Siku busara itakapoachwa kutamalaki dhidi ya ushabiki uchwara, serikali zetu zitajifunza kuyatenda yale ambayo wananchi wanataka na si vinginevyo.

Kwa mtaji huu hata mikataba ya bandari za bwagamoyo tutaishia kuambiwa kilichomo bila ya kupewa tuseme wenyewe.

Hiiiiii bagosha!
 
Bwashee kuna wakati kichwa chako kinakuwa vizuri sana! Halafu kuna wakati, huwa unajitoa ufahamu kabisa!! Natamani ubakie na kichwa hiki, badala ya kile kingine cha kimataga mataga!
Bwashee kwenye ukweli lazima tuuseme.

Kwa mfano kwa viapo vile vya DC Ole sabaya na OCD unadhani Freeman angeshindaje ubunge?
 
Bwashee kwenye ukweli lazima tuuseme.

Kwa mfano kwa viapo vile vya DC Ole sabaya na OCD unadhani Freeman angeshindaje ubunge?
Mkuu hata sisi wananchi tunapaswa kulaumiwa kwa haya yanayotokea, huku mtaani tunakaa tunabishania chama cha nani kina wabunge wengi, kwahiyo kitendo cha wananchio kuona ufahari kuwa chama chake kinawabunge wengi ni ujuha, mi nafikiri wananchi hatupaswi kuwa na chama tunabidi tuchague mtu tunaehisi atatuvusha
 
Hatari kwenye lango la CCM Asilia, MATAGA wameicheza vizuri hoja lakini mshika kibendera kasema ni Off Side
 
moja kati ya urithi mbaya ambao jiwe kawaachia baadhi ya vijana wanaotoka katika familia za kifukara(mwenyewe alikuwa anawaita wanyonge), ni kuwaachia tabia ya kuwachukia matajiri bila sababu.

huu sio urithi mzuri na jiwe alifanikiwa sana kuwa-brainwash katika hili. itachukua mda mrefu huu urithi kuwatoka kwenye akili zao.
 
Back
Top Bottom