Ukiondoa Ukakasi wa Kauli za RC Chalamila Mnyonge Mnyongeni Ila Haki Yake Mpeni, Waafrika Tunapenda Kulelewa Mpaka Imekuwa Ulemavu

Sasa mkuu unamaanisha kwamba serikali viongozi watumie Noah, rumion, crown na juke let say kutoka DSM mpaka mwanza, bukoba, RUVUMA au rukwa? Tuwe wakweli tu.

Hii nchi Kuna muda unahisi kama matatizo na umasikini tulionao ukikaa sawa kabisa utakuta sisi wananchi wa chini ndyo tunachangia pakubwa kuifikisha mpaka hapa ilipo
 
Viongozi ni reflection ya jamii wanayoingoza
 
Hiki kitu ukiwaambia watz hawakuelewi, ila truth to be told. Kwma population ya sasa inawaelemea, wakifika mara mbili yake wata colapse kabisa
 
Nimesoma paragraphs 3 tu. Umeandika US3NGE, samahani.

Kodi tunazolipa zina msaada gani? Kuna nchi hapahapa Africa zina free healthcare. Ghana tu wana free maternal healthcare.
Sijui ni kaka"

Naomba nikueleze jambo moja... Unapopata nafasi ya kuwa msomi hata kwa bahati mbaya...

Jitahidi kuutumia usomi na kufanya tafiti kwenye hizo taasisi zinazosaidia akina mama kujifungua...

Inahuzunisha sana' tumekalia kila siku kuambiwa na kuimbiwa vya bure bure ndio vinavyoleta matokeo ya Magonjwa ya hovyo hovyo

Hizo health facility zinazalisha vya kutosha kuweza kuhudumia kundi la akina mama wajawazito 40 mpaka 100 kwa mwezi?


Tuko kwenye mifumo ya kuhitaji vituo vijihudumie vyenyewe, je vinaweza kujiendesha?

Facility inahudumia watu mfano 200 mpaka 300 kwa mwezi free, hizo Dawa na vifaa tiba mtanunua na nini?


Kuna wakati wasomi mnapaswa kuwa wakwanza kuwafundisha na kuwaelimisha ndugu' na Wana nchi kuchangia huduma ili hivi vituo viweze kuinuka na kujiendesha....

Nawaza wadau wa maendeleo wakijitoa siku moja sijui hivi vituo kama vitakuwa na uwezo wa kununua hata packet moja ya kidonge sidhani....

Badilika msomi
 

Umeelewa hoja yangu?

Nimeuliza kuna ulazima gani wa ku update gari zote za serikali wakati zilizopo zinafanya kazi? LC200 bado imara kufika popote pale ila LC300 zilipotoka wamechukua mpya, hivyo ndo vipaumbele? Wananchi wanapohoji kwanini wanunue vifaatiba msiwazogoe wakati wanaona kodi zao zinatumika ndivyo sivyo.
 
USA ni taifa lililofeli ?
100%

Mtu 1 kati ya watu 5 Marekani ana deni kutokana na matibabu ya kiafya. Marekani wanatumia 17.6% (2024) ya pato la taifa kwenye afya na bado wanatoa huduma zenye gharama kubwa, ukilinganisha na Uingereza ambayo ina mfumo wa huduma za afya wa Kitaifa (NHS), ambao ni mfumo wa umma unaolipiwa na serikali kupitia kodi.

Uingereza, huduma nyingi zinatolewa na serikali na kila mtu ana uwezo wa kupata huduma bila kujali hali yake ya kifedha. Marekani, mfumo wao una mgawanyiko, ambapo kuna bima binafsi, bima kupitia ajira, na pia Medicare & Medicaid za serikali. Mgawanyiko huu unasababisha ufanisi mdogo, gharama za huduma kuwa juu, na upatikanaji wa huduma kutofautiana kulingana na bima na hali ya kifedha ya mtu.
 
50,000/- kwajili ya kujifungua ni gharama?
Siyo kila mtanzania ana uwezo wa kumudu hizo gharama. Ndiyo maana kama taifa ni lazima pia, kuwe na mipango dhabiti ya kuinua uchumi wa taifa na mtu mmoja-mmoja ili kuongeza walipa kodi na kupunguza namba ya umasikini. Kama taifa inasikitisha kuona vipaumbele vyetu ni vingine kabisa.
 
Ushawahi kujiuliza kwanini hujawahi kusikia mtanzania yeyote amekwenda airport kupanda ndege za Air Tanzania bure?
Jibu ni kwamba serikali haijawahi kuwambia hivyo. Sasa unakuta waziri ili serikali ipate sifa anawambia akina mama wajawazito kutibiwa, huduma na dawa ni bure, same kwa elimu halafu wanaenda wanakuta si bure.
Mkosaji hapa ni serikali ambayo haitaki kuwambia ukweli. Leo waziri kaulizwa bungeni bado anasema ni bure.
Wambieni ukweli kuwa labda utachangia lakini si bure.
 
 
Chalamila ni CCM na serikali iliyopo madarakani inaongozwa na CCM na ilani ya CCM huduma ya kujifungua ni bure na kiukweli wananchi sidhani kama wanashindwa kuwa na hela kidogo ya kuchangia bali viongozi wenyewe wa serikali wamewalemaza na tena wanazungumza live bila chenga kwamba KUJIFUNGUA NI BURE na kama kuna Mtumishi wa afya amelipisha fedha mwananchi akalalamika ikafika kwenye vyombo vya habari itaitwa na PRESS kukemea kilichofanyika.

Hata hivyo ukijifingulia hospital za umma ni BURE except kama utaenda kijifungulia hospitali ya RUFAA bila kupewa rufaa hapo ndo kuna kulipia. Msiwasimange wananchi wakati wao wenyewe kina Chalamila (Serikali) ndo wanawaambia kujifungua ni bure hivyo hiyo buku 5 unayoiona ndogo wenzako wanaona wanapigwa

Ni kuwapa taarifa sahihi tu wananchi, mbona mwananchi huyo huyo kwenye elimu ameambiwa elimu bure (elimu bila malipo) analipia mahitaji kibao kuliko hata ile ada iliyofutwa alafu ashindwe kulipia huduma ya kujifungua ambayo ni BURE na hata kama kuna complication atapakiwa kwenye AMBULANCE kwenda hospitali ya rufaa nako pia ni BURE kwa kuwa alianzia hospitali za chini.

Wapeni wananchi taarifa sahihi msiwasimange
 
Nimesoma paragraphs 3 tu. Umeandika US3NGE, samahani.

Kodi tunazolipa zina msaada gani? Kuna nchi hapahapa Africa zina free healthcare. Ghana tu wana free maternal healthcare.
Kaka jitahidi ukiweka mimba uwe responsible, mengine yawe ziada tuu.
 
Kila mwaka zinapotea pesa nyingi za walipa kodi kutokana na matumizi mabaya ya rasilimali, wizi, udanganyifu, uhujumu uchumi, rushwa.

Tatizo kubwa ni kwamba system yetu ilishafeli kitambo sana, kwa nchi yetu imekuwa kawaida kuona watumishi wa umma wanachezea au kutumia rasilimali isivyotakiwa, hakuna uwajibishaji kwa watu wanaofanya makosa yanayogharimu taifa pesa nyingi sana. Halafu muda huohuo mwananchi wa kawaida tu anahamasishwa alipe kodi, pesa zinazoenda kufanya kazi nyingine nje na mipango.

Nchi yetu ina namba ndogo sana ya watu wanaolipa kodi na huwezi kuwalaumu wananchi. Itakuwa rahisi sana watu kulipa kodi kwa hiari pale watakapoona serikali yao inafanya jitihada kuboresha maisha yao na taifa kwa ujumla bila kujali cheo, undugu, au kabila. Imeshakuwa kawaida kwa nchi hii ili upate huduma bora basi lazima ujuane na mtu (connection) au uwe kwenye mfumo.
 
Kujifungua ni bure, ila vifaa ndio vya kugharamia hii mbona iko wazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…