Ukipanga maeneo haya Dar sahau kufanikiwa

Ukipanga maeneo haya Dar sahau kufanikiwa

Sasa tukaishi wap maana Dar yote ni uswazi tu na hayo maeneo machache ili ukakae huko masaaki inabidi uwe ushafanikiwa kabisa
Life style yako ndio itaamua ufanikiwe au laa
Sina uelewa sana, lakini kuna mitaa ina ulozi mbaya sana. Hakuna nuru hata kidogo. Kufanikiwa kwenye hayo maeneo inahitaji mtu mwenye supernatural powers au upate kibali cha muumba otherwise huwezi ona mwanga. Kuna mahala unaweza kukuta watu wa kawaida sana lakini wenye mioyo nyoofu na wasio na makuu- Very very good people.
 
Niende moja kwa moja kwenye mada.

Ukipanga haya maeneo dar ni uswazi kupindukia ukila vizuri au ukiwa ni mtu wa kuvaa vizuri sana lazima watu wakuwekee vikao.

Tandika

Buguruni

Mbagala

Gongo la mboto

Buza kwa mpalange

Mwananyamala

Niliwahi kuishi Tandika nyumba tofauti tofauti, kipindi hicho nafanya kazi maeneo ya uwanja wa ndege hivyo niliona ni sehemu sahihi kufikika kirahisi kwenye kibarua changu.

Nikiwahi kukutana na kisa kimoja mama mwenye nyumba alikuwa na binti zake, wapo tu nyumbani.

Jumapili nikiwa nikishinda nyumbani girlfriend wangu alikuwa kila weekend anakuja magheto, sasa tulikuwa tunakutana na kero mama na wanae ni vicheko vya kinafiki makelele mara waweke muziki wa taarabu sauti juu.

Maeneo haya ukijichanganya ukaanza mahusiano na mabinti wa maeneo hayo umekwisha, wakikuona unamaisha mazuri wanakutegeshea binti yao wakikunasa ujue ndoa ya mkeka inakuhusu.

Sasa wakaona sinasi wakaanza kuniwekea msosi kila nikirudi kutoka job nakuta msosi, nikasema poa wakileta nafinya alafu sitaki mazoea 😃😃.

Mara wewe upo busy sana, uwe unaacha nguo tukufulie nasema poa, nilikuja kuhama haya maeneo nilihamia maeneo fulani hivi Tabata huku kidogo nilikutana na utofauti kila mtu na mishe zake.
Kutofanikiwa au kufanikiwa kunatokana na mipangilio yako ya kimaisha
 
🤣 🤣 🤣 Dah- Kuna mtaa niliwahi kuishi hakuna hata kijana mmoja amewahi toboa, hata waliosoma maisha ni yaleyale tu. Halafu kuna mtu anasema hakuna uchawi 🤣🤣, uchawi upo ndugu zangu ingawa usipoyaona inakuwa ngumu kuamini. Kuna nyumba niliwahi panga LINDI acha tu, nilikaa pale kama wiki 3 nikatonywa na jirani wa mtaa wa 4 ambaye huyo mama ni rafiki wa rafiki yangu tulikutana huko, alivyojua ninaishi kwenye hiyo nyumba alishangaa nime-survive vp manake kila mpangaji lazima afie ndani.
Huwezi amini nilikaa pale kama mwaka, nikajiwekeza kwenye kusali kwa bidii, ila mengi niliyaona. Kama siyo MUNGU, sijui asee 🤣🤣🤣. LINDI uchawi wa kiukwelikweli upoo wala siyo story
Lindi huko niliendaga kufatilia mishe za kangomba nikakaa week ila ilikuwa kila saa 3 usiku naskia usingizi mzito baada ya mda unakata ukicheki ushachalazwa chale 😀😀😀
 
Kutofanikiwa au kufanikiwa kunatokana na mipangilio yako ya kimaisha
Kuna mipangilio gani kwa wengi zaidi ya kusoma vizuri na kufaulu kuomba ajira? Au wengine kumaximize mitaji kwenye biashara.

Hizo ndio njia ambazo wengi wamezitumia kufikia standard nzuri ya maisha. Kama umefata hatua zote kwa usahihi kwanini wengine wanatoboa we hutoboi kama unahisi maisha ni mpangilio?

Acha kuongelea maisha kiwepesi namna hio.
 
Uliyoyataja ndo mipangilio yenyewe.. Sasa we mtu anahisi alikopanga ndo kunampa umasikini badala ya kudeal na mipangilio yake unategemea nini?

NB Diamond ni wa TANDALE
 
Uliyoyataja ndo mipangilio yenyewe.. Sasa we mtu anahisi alikopanga ndo kunampa umasikini badala ya kudeal na mipangilio yake unategemea nini?

NB Diamond ni wa TANDALE
Hahahahaha kuna mazingira yanaingilia natural forces of nature nayo yanajulikana kama shirki
 
🤣 🤣 🤣 Dah- Kuna mtaa niliwahi kuishi hakuna hata kijana mmoja amewahi toboa, hata waliosoma maisha ni yaleyale tu. Halafu kuna mtu anasema hakuna uchawi 🤣🤣, uchawi upo ndugu zangu ingawa usipoyaona inakuwa ngumu kuamini. Kuna nyumba niliwahi panga LINDI acha tu, nilikaa pale kama wiki 3 nikatonywa na jirani wa mtaa wa 4 ambaye huyo mama ni rafiki wa rafiki yangu tulikutana huko, alivyojua ninaishi kwenye hiyo nyumba alishangaa nime-survive vp manake kila mpangaji lazima afie ndani.
Huwezi amini nilikaa pale kama mwaka, nikajiwekeza kwenye kusali kwa bidii, ila mengi niliyaona. Kama siyo MUNGU, sijui asee 🤣🤣🤣. LINDI uchawi wa kiukwelikweli upoo wala siyo story
Duh!
 
Huyo kijana aliyeishi huko unakokusema ni kwamba aliamua kuishi ROMA akawa kama WAROMA wanavyotaka, badala ya kuhangaika na mambo yake ya kimaisha
 
Ungejuwa matajiri wanapaki ma-V8 huko kigilagila usingesema. Yaani wa Ushuani na ndiyo wenye majumba yao ni washirikina hatari
Hilo huenda mwenzetu halijui...Katika haya maisha kama hujaotea chance ya kulamba asali kwenye mashirika na mamlaka za nchi basi wewe lazima uwe mtu wa kawaida sana...Ukifosi utapitia vichochoro vya gizani au kuichezea sharubu katiba 😂😂😂
 
sijaona ubaya wa watu wa maeneo hayo au vicheko na taarabu?
watu hadi msosi wanakupikia na nguo wangekufuria kweli binadamu amna wema. halafu kama unajiamini wew ni mwanaume hakuna wa kukulaazimisha kuoa
 
Nakata Rufaa kwanini umekusahau Kawe? Kuna sehemu inaitwa Ukwamani Makaburi Matatu jirani na kwa Mzee Marehemu Mzee wa Chabo ( Baba Naa ) huko Kukutana na Paka ama Anajamba au anakuamkia Shikamoo au Anakusonya au anakuomba ukibakiza Chakula umhifadhie ni Jambo la Kawaida sana.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Uzur wa uswahilin gharama za maisha ni ndogo alafu kama mtu wa madem utakula kuku wa kienyeji mpaka uvimbiwe, binafsi nilivyotoka Singida sehemu ya kwanza kuishi ni keko machungwa then keko magurumbasi nikaja kawe mzimuni na Sasa nipo mwananyamala, kufanikiwa kwa mtu na hicho ulichokiandika havina hluhusiano wowote
 
Narudia tena ukiishi maeneo haya sahau kutoboa:
*sinza
*kinondoni
*tabata
*mwenge

Maisha ya hizi sehemu vyumba au nyumba zake aziwezi kukupa tamaa ya kujiongezea asseti zaidi ya flat tv na kitanda cha chuma.

maisha ya hizi sehemu ni mwendo wa kula vizuri na bata sana.

maisha ya sehemu hizo kuna maduka mengi ya nguo na mabaa sana.

maisha ya sehemu hizo kuna wavivu na majobless wengi ila ni mabingwa wa matumizi.

maisha ya sehemu hizo kuna ukioa au kuolewa kuna
mawili umepata muhuni mwenzako.
 
Ahsante kwa taarifa... tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom