Ukipanga maeneo haya Dar sahau kufanikiwa

Sasa tukaishi wap maana Dar yote ni uswazi tu na hayo maeneo machache ili ukakae huko masaaki inabidi uwe ushafanikiwa kabisa
Life style yako ndio itaamua ufanikiwe au laa
Sina uelewa sana, lakini kuna mitaa ina ulozi mbaya sana. Hakuna nuru hata kidogo. Kufanikiwa kwenye hayo maeneo inahitaji mtu mwenye supernatural powers au upate kibali cha muumba otherwise huwezi ona mwanga. Kuna mahala unaweza kukuta watu wa kawaida sana lakini wenye mioyo nyoofu na wasio na makuu- Very very good people.
 
Kutofanikiwa au kufanikiwa kunatokana na mipangilio yako ya kimaisha
 
Lindi huko niliendaga kufatilia mishe za kangomba nikakaa week ila ilikuwa kila saa 3 usiku naskia usingizi mzito baada ya mda unakata ukicheki ushachalazwa chale πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kutofanikiwa au kufanikiwa kunatokana na mipangilio yako ya kimaisha
Kuna mipangilio gani kwa wengi zaidi ya kusoma vizuri na kufaulu kuomba ajira? Au wengine kumaximize mitaji kwenye biashara.

Hizo ndio njia ambazo wengi wamezitumia kufikia standard nzuri ya maisha. Kama umefata hatua zote kwa usahihi kwanini wengine wanatoboa we hutoboi kama unahisi maisha ni mpangilio?

Acha kuongelea maisha kiwepesi namna hio.
 
Uliyoyataja ndo mipangilio yenyewe.. Sasa we mtu anahisi alikopanga ndo kunampa umasikini badala ya kudeal na mipangilio yake unategemea nini?

NB Diamond ni wa TANDALE
 
Uliyoyataja ndo mipangilio yenyewe.. Sasa we mtu anahisi alikopanga ndo kunampa umasikini badala ya kudeal na mipangilio yake unategemea nini?

NB Diamond ni wa TANDALE
Hahahahaha kuna mazingira yanaingilia natural forces of nature nayo yanajulikana kama shirki
 
Duh!
 
Huyo kijana aliyeishi huko unakokusema ni kwamba aliamua kuishi ROMA akawa kama WAROMA wanavyotaka, badala ya kuhangaika na mambo yake ya kimaisha
 
Ungejuwa matajiri wanapaki ma-V8 huko kigilagila usingesema. Yaani wa Ushuani na ndiyo wenye majumba yao ni washirikina hatari
Hilo huenda mwenzetu halijui...Katika haya maisha kama hujaotea chance ya kulamba asali kwenye mashirika na mamlaka za nchi basi wewe lazima uwe mtu wa kawaida sana...Ukifosi utapitia vichochoro vya gizani au kuichezea sharubu katiba πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
sijaona ubaya wa watu wa maeneo hayo au vicheko na taarabu?
watu hadi msosi wanakupikia na nguo wangekufuria kweli binadamu amna wema. halafu kama unajiamini wew ni mwanaume hakuna wa kukulaazimisha kuoa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Uzur wa uswahilin gharama za maisha ni ndogo alafu kama mtu wa madem utakula kuku wa kienyeji mpaka uvimbiwe, binafsi nilivyotoka Singida sehemu ya kwanza kuishi ni keko machungwa then keko magurumbasi nikaja kawe mzimuni na Sasa nipo mwananyamala, kufanikiwa kwa mtu na hicho ulichokiandika havina hluhusiano wowote
 
Narudia tena ukiishi maeneo haya sahau kutoboa:
*sinza
*kinondoni
*tabata
*mwenge

Maisha ya hizi sehemu vyumba au nyumba zake aziwezi kukupa tamaa ya kujiongezea asseti zaidi ya flat tv na kitanda cha chuma.

maisha ya hizi sehemu ni mwendo wa kula vizuri na bata sana.

maisha ya sehemu hizo kuna maduka mengi ya nguo na mabaa sana.

maisha ya sehemu hizo kuna wavivu na majobless wengi ila ni mabingwa wa matumizi.

maisha ya sehemu hizo kuna ukioa au kuolewa kuna
mawili umepata muhuni mwenzako.
 
Ahsante kwa taarifa... tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…