Asilimia mia moja ni kujiendekeza tu...hamna lolote...
sijawahi kucheza kamari yeyote ile kwa zaidi ya miaka kumi na tano mpaka sasa,...
Situmii kilevi chochote kile kwa zaidi ya miaka mitano sasa...
Nikiwa najitafuta migodini, rafiki zangu walikuwa wanashangaa nawezaje kwenda kugonga nyundo maporini huko, ilihari nina zaidi ya million kwenye account yangu..wakati huo na mimi nawashanga WANASHINDWA NN...
kifupi wengi hawana ndoto kubwa,na walionazo hawawezi kujitoa muhanga vya kutosha ili kutimiza ndoto zao,wapenda sifa za kijinga zinazodumu kwa siku moja na kisha kuyeyuka kama barafu tu,na ndio sababu kama umechunguza vizuri watu wengi wakishajenga kanyumba tu ka kulaza mbavu, hata jitihada za utafutaji au uwekezaji zinapungua, akinunua kipikipiki au kigari basi kamaliza kila kitu..kinachobaki ni kujitamba huko bar, vijiweni na kwenye mitandao ya kijaamii.....
mtu ambaye akipata pesa kidogo hakamatiki, wala hashauriki na zikiisha ndo anatia huruma na kuwa msikilizaji mzuri na kuapa kuto kurudia kwingi, kamwe usimsaidie kwa kumpa pesa, anapolia njaa mkumbushe juu ya kutapanya kwake pesa kipindi alipopata kilaki moja...