Ukipata pesa hakikisha unatulia nyumbani kwako

Ukipata pesa hakikisha unatulia nyumbani kwako

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
23,928
Reaction score
63,499
Unapopata pesa nawazungumzia vijana wa Leo hakikisha unakaa nyumbani , hakikisha pesa inageuka Akiba ya kudumu usikubali kutumia pesa yako kununua Magonjwa ili baadae uishi kwa mateso.

Wewe ndio Mwalimu wa Maisha yako wewe ndo daktari wa Maisha yako yaani wewe ndo kila kitu.

Hizi hadithi za zamani nilikuwa na PESA acha zibaki kwao usiziruhusu zitokee kwako.

Ukipanda Juu hakikisha unakuwa makini zaidi ya ulivyokuwa chini . Maana siku zote kushuka chini ni rahisi kuliko kupanda Juu. Pia usisahau kujisamehe na kuanza upya .
 
Sasa mzee vijana hwana familia 😀ni wazee wa kuvuta demu na kumalizana nae ,Wana mnyonyoro mrefu kama wanawake ndo wengi hapo kweli nafsi itatulia?

Sio lazima ufanye yote hayo ila inapendeza unazitawala hisia zako .

Then tutofautishe anasa na Bata hizi tunakula vijana sio Bata ni Anasa na Anasa zinakufanya unakuwa mtumwa wa watu Maisha yako yote
 
Nice!
Nimeipenda haya ya mwisho.
Vitu vyote vinavyonididimiza kiroho, kiafya au kiuchumi nimeviweka kando. Kwa sasa nimeamua kufuata uelekeo wa hatma ya maisha yangu. Siijui ipo vipi ila naamini naelekea pazuri kwa kuwa naendelea kujiandaa.
Nafanya tafakari ya nilipotoka na ninapoelekea. Tafakari kubwa zaidi nitaifanya nikifika mid-20's. Hapo ndipo nitaamua niende pembe ipi kati ya zile nne za dunia.
 
Unapopata pesa nawazungumzia vijana wa Leo hakikisha unakaa nyumbani , hakikisha pesa inageuka Akiba ya kudumu usikubali kutumia pesa yako kununua Magonjwa ili baadae uishi kwa mateso.

Wewe ndio Mwalimu wa Maisha yako wewe ndo daktari wa Maisha yako yaani wewe ndo kila kitu.

Hizi hadithi za zamani nilikuwa na PESA acha zibaki kwao usiziruhusu zitokee kwako.

Ukipanda Juu hakikisha unakuwa makini zaidi ya ulivyokuwa chini . Maana siku zote kushuka chini ni rahisi kuliko kupanda Juu. Pia usisahau kujisamehe na kuanza upya .
Nawakumbusha vijana.

Bata ya uhakika ni kutafuta kuku maishs yote,hakuna madhara ya mtu kupiga kuku,bali kuna madhara ya mtu kula pombe sana.
 
Back
Top Bottom