Ukipata saratani usipoteze pesa kwa matibabu anza kupanga mazishi. Katika July Joyce Laboso, Kenneth Okoth na Bob Colymore wameangushwa na saratani

Ukipata saratani usipoteze pesa kwa matibabu anza kupanga mazishi. Katika July Joyce Laboso, Kenneth Okoth na Bob Colymore wameangushwa na saratani

Maisha ni matamu ndugu yangu. Siri kubwa ni 'early diagnosis', ugonjwa wa saratani ukigunduliwa mapema una chance kubwa zaidi ya kusurvive. Hatua hiyo nayo inahitaji 'regular medical check ups', hapo sasa ndio utata ulipo kwetu sisi waafrika. Kumtembelea daktari bila sababu kwetu ni kama kuingia kituo cha polisi kuwaamkua ma afisaa.

Aina za saratani zipo zaidi ya mia, na kila moja ina uwezo wa kukuondolea mbali, sasa utakaguliwa ipi uache ipi, tufe tu, ikija ije wa kutangulizwa mbele za haki aende zake tutamfuata. Sipendi stress na kuchekiwa na daktari, maana na wenyewe makajanja, atakubabaisha ujikute na presha bure na kukutafuna mihela.

Juzi nimekwenda kupima UKIMWI, yaani ile taharuki niliyokua nayo utadhani ikipatikana nina ngoma nitakufa papo hapo. Bwana tuache tuishi hivi hivi tu, wewe kula vizuri, piga tizi, cheka sana, furahia kila siku na kuichukulia kama bakshshi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, maana wanaotutangulia wapo wenye hela zaidi yetu, wenye elimu zaidi yetu, wengine hata watakatifu zaidi yetu, yaani hapo ulipo huna chochote cha maana zaidi ya hao wanaotutangulia, hivyo ile tu umesazwa na unaiona siku nyingine mpya, aisei piga magoti na kushukuru Mungu sana.
 
Serikali itusaidie tu otherwise hatuwezi toboa
 
Serikali itusaidie tu otherwise hatuwezi toboa

Tabia ya saratani hata ukiwahi matibabu mapema baadae lazima itarudi kukumaliza tu.
Ugonjwa huo ni Jehanamu ya Duniani, unakutafuna mwili hadi unakumaliza 💀
 
Umeanza vizuri sana ila hapo mwisho tu kwenye "kuwaamkia" ndio umechemka naona Tecno yako imeanza wenge
Sijakuelewa, hebu soma tena, nimeandika kuwa amkua sio hiyo kuwaamkia uloandika hapo. Mambo ya Tecno kwenye mada kuhusu saratani ni ukichaa flani hivi.
 
Serikali itusaidie tu otherwise hatuwezi toboa. Bei ya chemotherapy na radiotherapy pia ipunguzwe. Waafrika wa zamani hawakuwa wanapata cancer kwa fujo kama siku hizi. Pengine ni chakula. Tuwache kukula broiler iliyodungwa madawa ya antibiotics na chips iliyopigwa deep fry. Tuanze kula chakula iliyokuzwa bila fertilizer. Mambo ya canned food iliyowekwa preservatives pia tuwache. Turudi enzi ya kula mboga fresh straight from the shamba. Nyama fresh ndio sawa sio yenye imekaa kwa fridge miezi miwili.
 
Una habari hata Steve Jobs wa Apple ni saratani ilimuondoa?
Kuna wengi ambao wamepata matibabu na wakapona. Mfano mzuri ni babake Lupita Nyong'o, gavana wa gatuzi la Kisumu Prof. Anyang' Nyong'o.
 
mie naona tuwe na Therapists ama counsellors, is not easy to accept unaumwa na there's no cure,wengi wanakimbilia huko kwa TB Joshua na wengineo in desperation.
 
Aina za saratani zipo zaidi ya mia, na kila moja ina uwezo wa kukuondolea mbali, sasa utakaguliwa ipi uache ipi, tufe tu, ikija ije wa kutangulizwa mbele za haki aende zake tutamfuata. Sipendi stress na kuchekiwa na daktari, maana na wenyewe makajanja, atakubabaisha ujikute na presha bure na kukutafuna mihela.

Juzi nimekwenda kupima UKIMWI, yaani ile taharuki niliyokua nayo utadhani ikipatikana nina ngoma nitakufa papo hapo. Bwana tuache tuishi hivi hivi tu, wewe kula vizuri, piga tizi, cheka sana, furahia kila siku na kuichukulia kama bakshshi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, maana wanaotutangulia wapo wenye hela zaidi yetu, wengine hata watakatifu zaidi yetu, aisei piga magoti na kushukuru Mungu sana.
Hapo uliposema acha tufe ndio sasa umetia ukakasi. Mimi hapa bado sijamaliza shughuli zangu duniani, za kula bata. 'Medical check ups' mara kwa mara ndio njia mojawapo ya kuzuia maafa yanayosababishwa na saratani. Haijalishi ni aina gani ya saratani.
 
Tony254, waulize wakenya wanaoishi Tanzania, au nikupe Simu ya Mkurugenzi MKUU wa Ocean Road Cancer Institute ili uwasiliane naye?
Sasa wewe unataka Wakenya karibia milioni hamsini waje watibiwe katika hospitali moja? Hio hospitali moja hata haiwatoshi ninyi Watanzania milioni hamsini na tano. Nilidhani hospitali zote public T.Z zinafanya checkup? Kumbe ni hospitali moja?
 
We are all the Walking Dead..., Eventually that's our path Cancer or not...... , so seeking medication is just to delay the inevitable.. and since one has earned his wealth..., what's the use of such wealth if not using it to have a fighting chance ?
 
Hapo uliposema acha tufe ndio sasa umetia ukakasi. Mimi hapa bado sijamaliza shughuli zangu duniani, za kula bata. 'Medical check ups' mara kwa mara ndio njia mojawapo ya kuzuia maafa yanayosababishwa na saratani. Haijalishi ni aina gani ya saratani.
Kifo ni jambo la lazima. Inabidi ujitayarishe kisaikolojia. Unaeza toka nje ukagongwa na gari, sio lazima mtu afe kwa cancer. Kwa hivyo kifo haikwepeki. Aliyezaliwa lazima ataonja mauti. Tenda mema nenda zako.
 
Kuna wengi ambao wamepata matibabu na wakapona. Mfano mzuri ni babake Lupita Nyong'o, gavana wa gatuzi la Kisumu Prof. Anyang' Nyong'o.

Nilikunukuu kwenye bandiko lako hasa ulipoandika kwamba Afrika ndio tatizo kwa vile hatucheki afya zetu mara kwa mara, nikaona nikukumbushe kwamba saratani imepeleka watu wenye uwezo wasioishi Afrika. Uzuri wewe mwenyewe umekuja na mifano ya watu wa afrika walipona Saratani.
 
Sasa wewe unataka Wakenya karibia milioni hamsini waje watibiwe katika hospitali moja? Hio hospitali moja hata haiwatoshi ninyi Watanzania milioni hamsini na tano. Nilidhani hospitali zote public T.Z zinafanya checkup? Kumbe ni hospitali moja?
Sasa mbona unaanza kuwa negatives badala ya kuwa positive?. Kila Hospitali iko na level yake ya kufanya kazi. Cancer screening Equipments huwezi kuzikuta katika level ya Health centres.

Tanzania Hospital zote za Referral zinafanya cancer screening free of charge, ila advanced treatment ya Chemotherapy kwa kutumia "Lenear accelerator" inapatikana Ocean road na Bugando pekee., Ocean road ni free of charge, wakati Buganda unalipa bei yenye Government subsides kwasababu hiyo Hospital ni PPP.

Kumbuka huko kwenu Kenya, " Lenear accelerator Machines ipo Agha Khan Hospital pekee, na ni very expensive for 95% of Kenyans.
 
Hapo uliposema acha tufe ndio sasa umetia ukakasi. Mimi hapa bado sijamaliza shughuli zangu duniani, za kula bata. 'Medical check ups' mara kwa mara ndio njia mojawapo ya kuzuia maafa yanayosababishwa na saratani. Haijalishi ni aina gani ya saratani.

Naona unalichukulia lightly,Mtu kupata ajali..si kitendo cha mara moja??,jiuguze miezi/miaka huku ukijua unakufa sio kitu rahisi..especially ukiwaona familia yako iko distressed na ugonjwa wako..na wewe uko helpless...NO,usilinganishe kifo cha ajali iwe sawa na kifo cha saratani..
 
Back
Top Bottom