MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Maisha ni matamu ndugu yangu. Siri kubwa ni 'early diagnosis', ugonjwa wa saratani ukigunduliwa mapema una chance kubwa zaidi ya kusurvive. Hatua hiyo nayo inahitaji 'regular medical check ups', hapo sasa ndio utata ulipo kwetu sisi waafrika. Kumtembelea daktari bila sababu kwetu ni kama kuingia kituo cha polisi kuwaamkua ma afisaa.
Aina za saratani zipo zaidi ya mia, na kila moja ina uwezo wa kukuondolea mbali, sasa utakaguliwa ipi uache ipi, tufe tu, ikija ije wa kutangulizwa mbele za haki aende zake tutamfuata. Sipendi stress na kuchekiwa na daktari, maana na wenyewe makajanja, atakubabaisha ujikute na presha bure na kukutafuna mihela.
Juzi nimekwenda kupima UKIMWI, yaani ile taharuki niliyokua nayo utadhani ikipatikana nina ngoma nitakufa papo hapo. Bwana tuache tuishi hivi hivi tu, wewe kula vizuri, piga tizi, cheka sana, furahia kila siku na kuichukulia kama bakshshi kutoka kwa Mwenyezi Mungu, maana wanaotutangulia wapo wenye hela zaidi yetu, wenye elimu zaidi yetu, wengine hata watakatifu zaidi yetu, yaani hapo ulipo huna chochote cha maana zaidi ya hao wanaotutangulia, hivyo ile tu umesazwa na unaiona siku nyingine mpya, aisei piga magoti na kushukuru Mungu sana.