Ukipewa nafasi ya kuwa Kiongozi kwa siku moja ni kitu gani utabadilisha cha kwanza?

Ukipewa nafasi ya kuwa Kiongozi kwa siku moja ni kitu gani utabadilisha cha kwanza?

Kama ni nafasi ya uraisi cha kwanza nibadili katiba na kuweka katiba Mpya inayoleta haki usawa na huruma Kwa wananchi.
Cha pili ningefanya elimu kuanzia chekechea mpaka chuo iwe bure.
Cha tatu ningefanya matibabu iwe bure. Najua Kwa rasilimali tulizo nazo inawezekana..
Pia ningevunja mikataba mibovu na kulinda rasilimali za nchi.
 
1. Nitapiga palanja kali kuwasaka mafisadi wote hata km uko nje ya Tanzania, nitawafungulia kesi za kuhujumu uchumi Kisha nusu ya Mali zote nazitaifisha iwe Mali ya serikali.
2. Nitafuta mfumo wa elimu hii duni, nitabadilisha mitaala yote nitabakiza masomo ya sayansi, computer na ufundi mengine yote futa kbs
3. Rasilimali zote za nchi zitakuwa chini ya jeshi management yote ni jeshi Tena wale commando kbs wao ndio wazalendo madini,wanyamapori na n.k
4. Mashirika yote ya serikali yatasimamiwa na special forces jeshi hakuna longolongo
5. Mikataba isikuwa na tija yote futa kbs fukuza
6. Futa uchawa serikalini kuwe na ukweli na uwazi
 
Ikitokea umepewa fursa ya kuwa kiongozi kwa siku moja, unapata nafasi ya kufanya mabadiliko katika sehemu uliyopo na kubalisha kitu kimoja kwenye sehemu uliyopewa uongoze.

Ikitokea ninafursa ya kuwa kiongozi kwa siku moja, ningependa kuwa kiongozi wa taasisi ya elimu, kama chuo kikuu. Elimu ni msingi wa maendeleo ya kitaifa na binafsi. Kipaumbele changu cha kwanza kingekuwa kuangalia upya mfumo wa elimu na kuhakikisha kuwa unaendana na mahitaji ya sasa ya jamii na soko la ajira.

Ningependa kuwekeza zaidi katika teknolojia na rasilimali za kufundishia ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wanapata elimu bora na inayokidhi viwango vya kimataifa. Kwa kufanya hivyo, ningewawezesha wanafunzi kufikia uwezo wao kamili na kujenga msingi imara kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.

Unatamani uwe kiongozi wa nini na wapi na ni kitu gani ungekipa kipaumbele cha kukifanya cha kwanza na kwa sababu gani?
Nawatia ndani almost asilimia 80 ya viongozi wa sasa
 
Back
Top Bottom