Ukipoteza Meno huna Ulazima wa Kubaki na Mapengo Kuna Suluhisho la Kudumu

πŸ˜…πŸ˜…Asante sana, kwakweli Mungu kanitetea maana shetani alikusudia mabaya.

Nakuja Pm πŸ˜…
 
Nimesikitika

Hakuepo hewani karudi lkn bado hana jibu la moja kwa moja hadi simu.
 
Na marketing ni tatizo kubwa kwa Watanzania
 
Siyo kweli. Bei zinaeleweka. Kusafisha meno. Kuweka veneers. Lumineers. Kuziba cavity. Root canal. Braces. Ranges zake zote zinaeleweka. Weka bei za msingi za kila huduma; na of course kila mtu anajua kuna contingencies nyingi tu na bei zinaweza kubadilika kulingana na tatizo la mtu; maana matatizo ya watu hayatafanana. Nadhani hii ni common sense tu na kila mtu anajua.

Hata Profesa Janabi anakwambia kuwa kuweka stents kwenye moyo ni milioni 7 lakini tunajua kuwa inaweza kuwa zaidi kulingana na mahitaji ya mgonjwa na mgonjwa.

Na tunacholalamikia hapa ni general trends ya advertisement za Wabongo. Ni wagumu sana kuweka wazi bei ya bidhaa wanazouza na matangazo yao mengi ya biashara huwa hayajitoshelezi mpaka uanze kupiga simu huko ambazo mara nyingi pia unaweza usijibiwe.
 
Inaonekana huyu winga wa meno ni tapeli... Ukijichanganya anaweza kukuwekea mahindi ya makande akwambie ni meno
 
Samahani kwa kuchelewa kuona comment yako , huduma ya meno bandia yapo ya kuanzia Tsh 40,000/= mpaka Tsh 400,000/= kwa jino moja bei zinatofautiana Kulingana na Aina ya meno karibu sana
Ulishindwa nini kuandika hivyo tangia mwanzo unaishia kutoa majibu ya kuzurura tu?.

Kumbuka mnachofanya siyo msaada bali ni biashara kama ilivyo biashara nyingine...

Hivyo kwenye soko huria la kibepari unapaswa kuainisha bayana taarifa anuai ili kutanabaisha kile ukitangazacho.

Ukifanya hivyo inaondoa hofu na kuleta imani kwa baadhi ya walaji wa bidhaa yako.
 
Ahsante kwa ushauri mzuri , Nitaufanyia Kazi Boss πŸ™
 
Bei unazozifahamu wewe siyo lazima ziwe bei zao.

Kila mtoa huduma anaweza ku charge aonavyo yeye ni sawa kwake, mlaji anao utashi kupokea au kukataa.

Bei hupangiwi na serikali na hakuna bei elekezi kwa huduma hizo, kila mtoa huduma hutumia technologia tofauti na wana nunua vitendea kazi kutoka sehemu tofauti ndio maana unakuta kila mtoa huduma anakuwa na bei yake.

Kama wewe unajua bei zako basi nenda huko ulikokuzoea huna haja kumlazimisha naye a charge kama huyo uliyemzoea.
 
Nimepokea Ushauri wako Nitaanda Poster Yenye Kila Kitu Na Gharama Zake Nitaweka πŸ™
 
Ahsante Sana Ubarikiwe Na Mungu , Umenisaidia Kujibu Kwa Usahihi Mkubwa Sana πŸ™
 
Jf imevamiwa na nyumbu wengi Sana umeandika fact
Nashukuru, JF nyumbu ni wengi lakini hatutaki kukubali.

Hatuwezi kujua kila kitu lakini tunachangia kila kitu humu JF, ni jukwaa huru kwa kila mtu lakini kuna wataalam wa nyanja tofauti pia humu humu JF ila wamejificha nyuma ya hizi ID fake, zinasaidia tunapoandika ujinga wetu tusijulikane.

Ni jukumu letu pia kukosoa tunapoona mtu anapotosha na tunaweza kusaidia kunyoosha kwa uelewa wetu.

Watu hawaelewi ugonjwa ni personal ndio maana unakura mti anaugua ana meza dawa za mama au baba yake kwasababu wana hisi ugonjwa wa mama unaweza kuwa ndio huo huo wa mtoto.

Ndio maana tunawashauri wasinywe dawa kabla ya kumuona daktari na kupata vipimo stahiki.

Ila kumbuka mfumo wetu wa afya umepinda ila tutaelimisha na wapo wataelewa na wapo vichwa ngumu.
 
Samahani kwa kuchelewa kuona comment yako , huduma ya meno bandia yapo ya kuanzia Tsh 40,000/= mpaka Tsh 400,000/= kwa jino moja bei zinatofautiana Kulingana na Aina ya meno karibu sana
Safi sana mambo si haya bhana.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Samahani kwa kuchelewa kuona comment yako , huduma ya meno bandia yapo ya kuanzia Tsh 40,000/= mpaka Tsh 400,000/= kwa jino moja bei zinatofautiana Kulingana na Aina ya meno karibu sana
Hapa sasa unaongea mkuu, kutokea hapa sasa mtu baada ya kuona price zako hapa anaweza kuja inbox ili muyajenge, ndo biashaara hiyo
 
Kama wewe unajua bei zako basi nenda huko ulikokuzoea huna haja kumlazimisha naye a charge kama huyo uliyemzoea.
Nimemlazimisha wapi acharge? Nani niliyemzoea? Ni wewe ndiye uliyeweka tangazo hili na hii ni ID yako nyingine maana si kwa kupaniki huku! πŸ˜‚

Hoja yangu ya msingi ni hii: Ukiweka tangazo la biashara jitahidi sana uweke habari zote zinazohitajika zikiwemo BEI ELEKEZI kwa huduma zako unazotoa. . Full stop! Is this too much to ask? Ni kitu gani ambacho huelewi hapo ili nikufafanulie tena? Jizazi! πŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈπŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈπŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈπŸšΆπŸΏβ€β™‚οΈ

 
sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…