mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Watanzania walio wengi walimkubali sana Magufuli. Magufuli aliwafungua macho watanzania, Wanasiasa walikuwa wanatudanganya kuwa nchi yetu ni maskini ili kuhalalisha wizi na ufisadi wao. Wengi wa wanaomchukia Magufuli ni mafisadi na familia zao. Ni wale ambao hawakupata kabisa fursa ya kuendelea kujifanya miungu watu kwenye ofisi za umma na wakwepa kodi. Mtu ulikuwa ukiingia ofisi ya umma unapokelewa na kuhudumiwa kwa heshima. Sasa hivi miungu watu wamerudi kwa kasi maofisini.
Lakini pia Magufuli alituongoza vizuri sana kwenye vita dhidi ya corona. Wakati wa Magufuli mabeberu hawakupata kabisa fursa ya kutumia corona kutunyonya! Chanjo za corona zisizo na sifa ya kuitwa chanjo (maana hazimkingi mtu na corona) hazikupata nafasi kabisa nchini mwetu! Hatimaye Dunia imekubali kile ambacho Magufuli alikiona mwanzo kabisa kuwa Dunia inabidi ijifunze kuishi pamoja na corona kama ilivyo kwa magonjwa mengine! Watanzania tulio wengi huwezi kutuambia kitu kuhusu Magufuli!! Tunampenda!! Tunamkubali!!! Ni mchapa kazi!! Ameacha alama isiyofutika: SGR, STIGLER'S GEORGE, MAKAO MAKUU DODOMA!!
Haya yote yalikuwa kama ndoto ya mchana isiyotekelezeka kabla ya Magufuli!! Lakini Chini ya Magufuli yote yamewezekana tena kwa muda mfupi!!! Ukimpiga vita Magufuli ni kutwanga maji kwenye kinu!!! Hata ukishindana na kaburi lake atakutoa knock out!