Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Ukishuka Airport Dar ukapita barabara kuu unaona jinsi nchi na watu wake walivyochoka. Viongozi mnafeli wapi?

Na yeye complete human being akaona pawe na shule,usafiri tofauti kati ya yeye mweupe na weusi!?..hivyo ndivyo wafikirivyo complete human beings!?
"Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa Watu weusi kwenye Mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake kwa sababu HAWANA AKILI NZURI. Endapo kama tungewajumuisha, basi wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika ya Kusini leo hii."

Pieter W. Botha, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini enzi za ubaguzi wa rangi.

Nafikiri umeelewa Sasa kwa nini Makaburu walifanya hayo uliyolalamikia kwenye comment yako.
 
Jaribu kutumia vyoo vya chuo kikuu au Halmashauri za vijijini.
Vyoo vya vyuo vikuu nimetumia Sana,wewe ilibahatika kutumia vyoo vya umma vya makaburu?..nimetazama Sana snakes in the city south Africa,nyumba za makaburu chafu tu,mmoja aligongwa na Kobra kwenye govi lake,Kobra alipenya kupitia Bomba la mavi lililopasuka
 
Mkuu utasemwa unajiona sasa hivi.

Dar kwanza advertise unaiona kutoka juu, vibati vyenye kutu mji mzima.

Nilishangaa sana Oysterbay pale shuleni barabara ina mashimo kibao.

Mandela Road barabara kubwa inasafirisha malori kwenda bandarini, ilikuwa haina taa.
Nchi inatafunwa na koo ambazo hazizidi 10 sababu ya ujinga wetu kupenda Simba na Yanga na kuacha kufuatilia mambo ya msingi
 
"Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa Watu weusi kwenye Mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake kwa sababu HAWANA AKILI NZURI. Endapo kama tungewajumuisha, basi wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika ya Kusini leo hii."

Pieter W. Botha, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini enzi za ubaguzi wa rangi.

Nafikiri umeelewa Sasa kwa nini Makaburu walifanya hayo uliyolalamikia kwenye comment yako.
Angeenda kujenga kwao uholanzi,kiliwapeleka kipi hapo?..walipofika hawakukuta social order?!
 
Siku nyingi nilitaka kusema haya ila moyo ukawa unasita, kwa kweli sielewi kabisa iweje njia ya kuu ya kuingia Tanzania sio Dar tu ni Tanzania tunashindwa kuweka lami ya kiwango na taa za barabarani maana taa weka za solar tu nini kinatushinda. Na hapa nalaumu serikali ya ndani kwa maana ya wabunge na madiwani. Huku juu ukiwa unatua vibati vimechakaa unaona aibu kuchungulia chini kidogo afadhali kama ndege inatua upande wa Posta ila ikipita huku sijui kunaitwaje ni vurugu mechi unaiona kwa juu.
 
Kumbbuka: Kwenye nchi yoyote ile hapa duniani ambayo Ina Utawala wa kidikteta au Utawala wenye itikadi ya Ukomunisti au Ujamaa, Wasomi na Watu wengine wenye akili na elimu kubwa huwa wanahesabika kuwa ni Maadui wakubwa zaidi wa Utawala uliopo madarakani.
Usithubutu hata kidogo kutaka kuleta idea, fikra au mawazo yako mapya kwenye nchi yoyote ile yenye Utawala wa namna hiyo, utapotezwa ndani ya muda mfupi kabisa, utahamishwa kutoka kwenye Sayari hii ya Dunia haraka sana bila kuchelewa. Take care!
Hali hii ni tofauti kwa nchi zilizo endelea zenye ubora mkubwa kuliko Tanzania mfano China,Vietnam na Korea kaskazini
 
Mod naomba univumilie niteme nyongo!.

Yaani kama ulitoka nje ukashuka airport Dara miaka 8 iliyopita, ukashuka miaka mitano iliyopita na ukashuka leo, unakutana na barabara ni lami siyo lami, vumbi tupu, makorongo matupu, mitaro ya waziwazi iliyojaa maji machafu, yaani kanchi kamechoka kamechoka kwelikweli. Hivi nyie watawala mnaoshinda kwenye ndege kila kukicha mnnaenda kwenye nchi za watu huwa hamuoni huko kwa wenzenu kukoje?

Yaani just imagine, barabara ya mwanzo ambayo wageni wanapita kabala hawajaenda popote nchini wanakutana na kituko cha barabara ile. First impression inayopatikana hapo ni ya kanchi masikini ka watu masikini, ka viongozi hopeless!

Yaani hako kabarabara kako hivyohivyo miaka nenda rudi pachovu choka mbaya, yaani vagalanti hovyohovyo.

Nyie watawala mnatutia aibu, mnajionaje fahari kuwa viongozi msioweza kudeal na issues ndogo namna hiyo kama hiyo ya kuipa nchi "reception" ya maana?

Kwa kweli aibu naona mimi.

Miviongozi kazi kujilimbikizia mali, kutwa kucha kwenye ndege, misafara ya mamia ya magari, lakini barabara tu ya airport wanayopita daily kwenda huko nje ya nchi kuuza sura imewashinda!. Sijui hii mijitu ikoje?

Kila siku ukipita maendo hayo unakutana na miradi uchwara as if wanajenga, lakini miaka yote huo ujenzi huwa hauishi, ni magumashi, hakuna lolote la maana linaloonekana!. Yaani choka mbaya choka mbaya, hovyo hovyo kabisa!.

Nyie viongozi wa nchi hii badilikeni. Ibcompentency yenu ndo inatufanya sisi huko duniani tuonekane kama nyani tu. Nchi zina marasilimali kibao halafu unakutana na vinchi vimechokaaa. Hii inakuwaje.

Yaani unapita barabarabani pembeni unakutana na mamitaro makubwaaa hayajafunikwa ambayo keanza ukifuatilia vizuri hayana exit ya mitoni wala sewage system yoyote ya maana, yaani yapo ceremonial tu.

Mamitaro makubwa hayajafunikiwa na yamekaa kama mahandaki ya vita kuu ya kwanza ya dunia. Hii hawa wenye dhamana ya utawala wakienda huko kwa wenzetu wanajifunza chochote kweli?.

Achilia mbali hilo. Ukishuka airport njiani unakutana na wabongo wamechoka mbaya, hali ngumu, wamekonda, wameweka vimizigo vyao barabarani masikini wanahustle. Hii iko hivyo miska nenda rudi. Wakati huo kuna watu wanaitafuna nchi hii kwa kula na kusaza. Ni lini wansnchi wataanza kula matunda na mema ya nchi?. Watawala wanawaza siasa tu, siasa tu.

Pia soma
- Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Mwigulu kajitutumua na tu miradi na mchina wake yule mkandarasi wa miradi ya BBRt, yenye 10 percent. utafikiri wako serious kumbe ni ufisadi mtupu

Na hivi serikari Haina hela baada kutifuatifua watapeleka claim ya hela nyingi isiyoendana na wanachokifanya
 
LOOoooh!

Leo nimebaki nikisoma na kucheka tu; halafu naingiwa na huzuni!

Kwa kawaida mada zako, mkuu 'Missile' huwa nazisoma kwa makini na fikra tulivu kama zilivyo wasilishwa kwa utulivu pia. Leo naona umeghadhabika kweli kweli; kama tunavyo ghadhabika sisi wengine siku zote tunapoona inako elekea nchi yetu hii.

N i hivi: kwa mwendo wetu huu tunao kwenda nao sasa, ukirudi baada ya miaka mitano mingine ijayo hutaamini macho yako yanacho kuonyesha.
Wenyewe hali hii tumeizoea, hatuoni tofauti, na hatuna uwezo wa kulinganisha. Hapo Kigali au Nairobi penyewe hatujui huko kulivyo; kama tusivyojuwa ya huko kwingineko.
Tuombe uzima tu.
 
Mod naomba univumilie niteme nyongo!.

Yaani kama ulitoka nje ukashuka airport Dara miaka 8 iliyopita, ukashuka miaka mitano iliyopita na ukashuka leo, unakutana na barabara ni lami siyo lami, vumbi tupu, makorongo matupu, mitaro ya waziwazi iliyojaa maji machafu, yaani kanchi kamechoka kamechoka kwelikweli. Hivi nyie watawala mnaoshinda kwenye ndege kila kukicha mnnaenda kwenye nchi za watu huwa hamuoni huko kwa wenzenu kukoje?

Yaani just imagine, barabara ya mwanzo ambayo wageni wanapita kabala hawajaenda popote nchini wanakutana na kituko cha barabara ile. First impression inayopatikana hapo ni ya kanchi masikini ka watu masikini, ka viongozi hopeless!

Yaani hako kabarabara kako hivyohivyo miaka nenda rudi pachovu choka mbaya, yaani vagalanti hovyohovyo.

Nyie watawala mnatutia aibu, mnajionaje fahari kuwa viongozi msioweza kudeal na issues ndogo namna hiyo kama hiyo ya kuipa nchi "reception" ya maana?

Kwa kweli aibu naona mimi.

Miviongozi kazi kujilimbikizia mali, kutwa kucha kwenye ndege, misafara ya mamia ya magari, lakini barabara tu ya airport wanayopita daily kwenda huko nje ya nchi kuuza sura imewashinda!. Sijui hii mijitu ikoje?

Kila siku ukipita maendo hayo unakutana na miradi uchwara as if wanajenga, lakini miaka yote huo ujenzi huwa hauishi, ni magumashi, hakuna lolote la maana linaloonekana!. Yaani choka mbaya choka mbaya, hovyo hovyo kabisa!.

Nyie viongozi wa nchi hii badilikeni. Ibcompentency yenu ndo inatufanya sisi huko duniani tuonekane kama nyani tu. Nchi zina marasilimali kibao halafu unakutana na vinchi vimechokaaa. Hii inakuwaje.

Yaani unapita barabarabani pembeni unakutana na mamitaro makubwaaa hayajafunikwa ambayo keanza ukifuatilia vizuri hayana exit ya mitoni wala sewage system yoyote ya maana, yaani yapo ceremonial tu.

Mamitaro makubwa hayajafunikiwa na yamekaa kama mahandaki ya vita kuu ya kwanza ya dunia. Hii hawa wenye dhamana ya utawala wakienda huko kwa wenzetu wanajifunza chochote kweli?.

Achilia mbali hilo. Ukishuka airport njiani unakutana na wabongo wamechoka mbaya, hali ngumu, wamekonda, wameweka vimizigo vyao barabarani masikini wanahustle. Hii iko hivyo miska nenda rudi. Wakati huo kuna watu wanaitafuna nchi hii kwa kula na kusaza. Ni lini wansnchi wataanza kula matunda na mema ya nchi?. Watawala wanawaza siasa tu, siasa tu.

Pia soma
- Kwanini Watanzania na Tanzania ni masikini pamoja na rasilimali (resources) tulizonazo?
Umasikini ni mtaji wa CCM
 
Nchi hii imefail karibia kwa kila kitu isipokuwa kwenye ufisadi, wizi wa kura na sifa za kijinga.

Ukitoka nje ya Tanzania, ukiwa bado angani, unaanza kuona maana ya nchi yenye umaskini wa akili. Utaona mambo ya hovyo ambayo hayahitaji utajiri wa pesa ila akili tu, kuweza kuyarekebisha.

Unakatishwa tamaa zaidi na machawa, kama akina Lucas et al, licha ya kila kitu kuwa hovyo, wanavyowasifia watawala kwa unafiki, unaweza kufikiria Tanzania inaongoza kwa maendeleo Duniani.

Siku moja nilikuwa Dodoma, nikapark gari, nikatembea kwa mguu kwenye uchochoro, mbele yangu kulikuwa na vijana watatu, wawili inaonekana waliluwa ni Wanyarwanda, sikuwauliza wala kujibishana wao. Kwenye uchochoro, kulikuwa na uchafu, mmoja akaanza kwa kushangaa, 'Aah! Aah!, hii ndiyo capital, Kigali huwezi ona hii", mmoja akaongezea, "hata kule barabara kuu, Kigali huwezi ona vile. Itokee kuwe vile, Kagame atafunga kuanzia waziri mpaka yule mtu wa chini". Yule mmoja aliyeonekana ni Mtanzania, akasema, hapa uchafu ni kawaida tu. Tena kuna sehemu, afadhali ya hapa.

Nchi yetu imefikia kwenye kiwango cha juu cha uhovyo. Tunaijenga nchi kwa uchawa wa maneno, na siyo uhalisia. Kukitokea mafanikio kiduchu, kelele zitakazipigwa, utadhani tumegundua iliko mbingu. Kila kitu imekuwani hadaa tu. Na maskini Watanzania, kwa sababu wengi wao, hawajaenda nchi nyingine, wanaamini kila wanachoambiwa na hawa watawala malaghai.

Kwa ujumla nchi yetu bado ni duni sana. Na hata kwenye takwimu za Dunia, wala hatumo kwenye orodha ya nchi ambazo zina maendeleo ya kasi. Tunazidiwa na nchi ambazo ni ndogo kabisa, kama Botswana, Namibia au Rwanda, ambazo uchumi wake unategemea sekta chache kabisa.
 
Mkuu utasemwa unajiona sasa hivi.

Dar kwanza advertise unaiona kutoka juu, vibati vyenye kutu mji mzima.

Nilishangaa sana Oysterbay pale shuleni barabara ina mashimo kibao.

Mandela Road barabara kubwa inasafirisha malori kwenda bandarini, ilikuwa haina taa.
Hii ya mji kuonekana chakavu, mabat kutu ni tatizo kubwa kwa Jiji la Dar la Zanzibar kiasi kwamba mgeni anayeenda kulala ktk miji hiyo anajua anaenda kulala kwenye Jiji chakavu. Miji hizi ziboreshwe kwa sababu ndiyo uso wa nchi kwa wageni.
 
CCM wanafurahia sana watu wanapokuwa maskini kwasababu ni kwao inakuwa ni rahisi kuwahonga.

Fikiria mtu mwenye kipato cha uhakika, atakubali kuhongwa kanga, Tshirt, kibaba cha mchele, kilo ya sukari au sh 5,000? Ukimletea hongo ya namna hiyo mtu mwenye kipato cha uhakika, si atakutandika kofi kwa kumdhalilisha?
 
Nyerere road si inajengwa mwendokasi/brt!!,ukitoka tu usawa wa airport mbona pako fresh
Kuna "semblance" ya ujenzi miaka nenda rudi huwa inafanyika lakini hamna lolote la maana!.Yaani huwa ni vumbivumbi tu maeneo hayo utadhani Kuna kitu serious kinafanyika , kumbe ni hopeless na useless kabisa!
 
Back
Top Bottom