Kwa msiojua na mnaoshangaa UTT haipo sana agressive kutafuta faida kubwa ila wanaplay safe ndo maana wanarange kwa faida ya 10-13% PA ila kwa hisa hususani za CRDB kuna zaidi ya hapo nitatoa mifano michache kwa wepesi kabisa ili nieleweke.
Binafsi ni mwanahisa wa CRDB kwa miaka kadhaa sasa na nitayoyasema hapa yanatokana na uzoefu wangu sokoni kwa nyakati tofauti. Pia nipo UTT-Ukwasi Fund.
1. Katika hisa zipo faida aina 2 (Gawio na ongezeko la thamani) Gawio ni pale bank itakavyopata faida na kupitia bodi kupitisha kiwango fulani kurudi kwa wawekezaji kama gawio. Mwaka jana CRDB tulipokea Tsh 50 kwa kila hisa 1 unayomiliki. Unaweza kuona Tsh50 ni pesa ndogo sana ila iko hivi ni ndogo au kubwa kutegemeana na wakati uliowekeza. Ninazo hisa ambazo nilinunua kwa Tsh 95 4yrs ago, Leo nikipokea Tsh 50 kwa kila Tsh 95 niliyowekeza hiyo ni zaidi ya 50% ROI.
2. Kuna capital gain au ongezeko la thaman hii ni pale hisa za Bank zinapopanda bei sokoni kutoka 100 to 200 ina maana kama uliwekeza 60m zikiwa zinauzwa kwa 100/share leo zimefika 200/share ukiuza zote tayari umetengeneza 120M bila kuweka magawio utakayokua unapokea kila mwaka. Mfano rahisi 2019/20 nilinunua hisa kwa Ths95 ila leo hisa hizo hizo zinauzwa kwa Tsh 700 sokoni.
Nikiangalia portfolio yangu tarehe kama ya leo 2023 imependa thamani kwa 49% kutoka thamani iliyokua mwaka jana. wakati huo huo UTT napokea 12% kwa mwaka mzima.
Ushauri wangu ni huu kwa wewe ambaye unataman kuwekeza katika hisa. Hakikisha unawekeza katika kampuni unayoielewa na kupitia brokers watakusaidia kuelewa ipi ni kampuni nzuri kuwekeza kulingana na malengo yako.
Pia ni muhimu uwe na malengo ya muda mrefu sababu huko ndo kweny mafanikio makubwa. Leo utanunua hisa kwa 700 utaona ni ghali ila niamini mimi baada ya miaka 5 utajilaumu sana kwa nini hukununua zaidi (mwenyew najilaumu leo kwa nini sikununua zaidi ilipokua 95) usifanye makosa kama yangu.
Hadi sasa CRDB imetengeneza faida zaidi ya 408B kwanzia January hadi Sept 2024 huu ni mwenendo mzuri kuelekea gawio lijalo May 2025.
Ikikupendeza tukutane Arusha AGM kwa story mbili tatu.