Ukisikiliza audio ya kocha wa Yanga, ameongea ukweli mtupu. Uongozi wa Yanga haupendi kuambiwa ukweli

Nyinyi ndio walewale hivi unapomchezesha mchezaji kwenye viwanja vibovu unategemea nini hujali afya ya mchezaji. Kwanza hata mpira wenyewe hauna ladha ya kuangalia ni siasa ndio inafanya mpira uchezwe viwanja vibovu jiulize ni viwanja vingapi vya mkoani vinaweza kupitishwa kuchezewa michuano ya kimataifa
 
Wakati unadai sie ndo wale wale; jibu maswali niliyokuuliza:

1. Wakati anafikiria kufundisha soka Tanzania alidhani viwanja ni kama vya Ulaya wakati tayari alishakuwa na uzoefu na viwanja vya Afrika?!

2. Suala la viwanja Yanga anahusika nalo vp?!

3. Na huko kwingine ambako na kwenyewe hakuwahi kutulia, ni kipi kilimwondoa?! Viwanja vibovu, wi-fi, gari au nini hasa?!

NOTE: Wakati unadai mie ndo wale wale tu, ninachoona wewe ndie wale wale tu... watu mnaojaribu kutafuta sababu za ku-justify lugha za hovyo za Eymael!

Na unathibnitisha kwamba nawe ni wale wale tu kwa sababu nimekuwekea maelezo hadi ya Agent kutoka South Africa aliyesema wazi kwamba Luc sio mtu wa kutulia sehemu moja, na hata ukiangalia CV yake inaonesha hivyo!

Sasa na wenzako mnaojaribu kutafuta sababu za ku-justify alichofanya Eymael, unataka kusema wewe ndo unamfahamu sana Luc kuliko mtu ambae amefanya nae kazi, na mtu mwenyewe wala hana ushabiki wa Simba vs Yanga?!

Na wakati mnajaribu ku-justify kwa hoja zisizo na kichwa wala miguu, Luc Eymael mwenyewe anawaambia Yahoo Sports kilichomfanya a-panic ni kwa sababu alikuwa harrassed na shabiki wa:-



Ambapo anaendelea:-

“I didn't go for the interview, just went straight to my hotel. All people were calling me [names] but I did not want to respond.

“Then there is this one guy from Simba who kept harassing me, and I reacted.”
Sasa kama alikuwa harassed na Shabiki wa Simba, how come povu awatolee Yanga, na kuita mashabiki wa Yanga wanabweka kama Monkey or Dogs?

Ajabu ya nchi hii, habari ya Luc Eymael imeripotiwa na media mbalimbali duniani... hadi Uhindini lakini ni Watanzania peke yao ndio wanaojaribu kutafuta sababu za ku-justify kitendo cha Luc Eymael!
 
Nina wasiwasi sana na afya ya akili ya huyo kocha. Anaonekana ni mtu mwenye msongo sana wa mawazo na hili liko wazi pale utakapoamua kusikiliza taratibu ile "audio" bila kuweka ushabiki wa Simba na Yanga. Kwa sababu kachanganya mambo mengi kwenye chungu kimoja. Ukichambua vizuri ametukuna/kutuhumu kuanzia viongozi wa Yanga, viongozi wa TFF, mashabiki wa Yanga, Simba kama timu kwa ujumla wake, chama na serikali (juu ya ubovu wa viwanja vya mpira) na watanzania wote kwa ujumla. Na mbaya zaidi katuletea mpaka mambo yake ya binafsi kuwa mke wake "haienjoy" kuwepo hapa nchini Tanzania. Kimsingi hapa kama huyu kocha angekuwa timamu kichwani hizo tuhuma zake zote angeziwasilisha kwenye uongozi kupitia ripoti yake baada ya ligi kumalizika. Na uongozi baada ya kupata ripoti ya kocha ungefuata taratibu katika kuyatafutia ufumbuzi malalamiko yake kuanzia yale uongozi wenyewe wa Yanga wangemalizana huko ndani, yale TFF na serikali viongozi wangeyawasilisha kimya kimya kwenye ngazi husika huko serikalini na mwisho zile kelele za wanachama/mashabiki hapo ndio kazi ya afisa habari kumalizana na wanachama/mashabiki wa Yanga. Lakini njia ya huyo kocha kubwabwaja kwenye vyombo vya habari moja kwa moja anakuwa sio mstaarabu na hana weledi na kazi yake kwa hiyo hafai kabisa kuwa mwajiriwa kwenye taasisi kubwa kama Yanga.

Kwanza niwapongeze sana viongozi wa Yanga pamoja na baadhi ya mapungufu yao waliyonayo lakini kwa hili wamechukua hatu zinazostahili kwa haraka sana. Hongereni sana viongozi wa Yanga.

Ila suala la huyu kocha na la mchezaji Morison liwazindue sasa viongozi wa Yanga wachukue hatua ya kukaa chini na mdhamini wao GSM. Badala ya mdhamini kuleta kocha au mchezaji na kuja kuwabwagia angalau wakae wajadiliane ili waweze kupata watu sahihi kwa ajili ya kuja kuzipigania "brand" za GSM na Yanga kwa pamoja. Kwa sababu nikiangalia ajira ya kocha na usajili wachezaji mpaka ligi ilipoisha wiki iliyopita naona ni hasara tupu kwa usajili wa wachezaji takribani 20 ukiondoa Haruna Niyozima pekee ndiye mwenye manufaa kwa timu. Na GSM asione aibu ajifunze jinsi Simba inavyopitia mchakato wa kupata makocha kwa kutumia jopo la wataalamu wa ndani wa kina Kayuni, Madadi, na wengineo.

Mwisho vilabu vyetu viwe makini vinaposajili wachezaji hasa wa nje kwani wa ndani wanafahamika tabia zao. Naamini kabisa iwapo "GSM" angefanya "homework" kidogo tu mtandaoni wa kupitia "CV" na habari kuhusiana na Eyamel na Morison hakika asingepata hii hasara na aibu. Siku hizi kila kitu kipo mtandaoni ni suala la kutenga muda tu ili kupata unachokihitaji. Ukiingiza tu jina la mtu zinakuja habari na historia yake yote. Kama mimi mtu wa kawaida tu nikiangalia tu historia na habari za Eyamel na Morison naona ni watu ambao hawafai kuajiriwa mahali kwa malengo ya muda mrefu vipi huyo GSM ambaye ana wataalamu wengi karibu yake (kutokana na aina ya biashara zake) ambao wangeweza kumsaidia kitaalamu kabla hata ya kuwasiliana nao sembuse kumwajiri huyo Eyamel na kumsajili Morison Yanga.
 
Kwani uongo??? SASA chura si manyani tu nyieee??
 
Sawa nyani
 
Kaka siamini kama hili unaongea wewe, hivi Dstv haizidi laki na nusu, unalipwa mshahara Mil 10 unashindwa kujiwekea kweli mpaka usubiri viongozi?
Luc kweli kazingua ila Yanga nayo ibadilike hivi kweli unashindwa hata kumpa kocha DSTV, wifi,gari?
 
Kwa hiyo hata kauli yake kuwa TFF ipo kwa ajili ya Simba ni sawa siyo?!?!?!
 
Huyu kocha bwege sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…