You can't be serious!! Yaani viwanja vya mikoani wamekuwa wakilazimisha mpira uchezwe kwa sababu za kisiasa au ni kwa sababu ndo viwanja vyenyewe vilivyopo?!
Hivi mtu ambae amefundisha mpira DRC, Rwanda, Gabon na hata Kenya bado alienda Tanzania huku akiamini viwanja vya Tz vitakuwa bora sana ukilinganisha na nchi zingine alizowahi kufundisha soka?! Ina maana alitarajia kukuta vyumba bora vya kubadilishia kuliko alivyoviona kwenye hizo nchi zingine?
According to Wikipedia, hapa chini ndio timu ambazo Luc Eymael amezifundisha kwa nyakati tofauti tofauti!
Over the past 10 years, hakuna club yoyote ambayo amekaa kwa zaidi ya mwaka mmoja... hivi huoni kwamba huyo mtu ana matatizo?! To be honest, mimi binafsi niliwashangaa sana Yanga kumchukua mtu mwenye CV ya aina hiyo! Hivi hata wewe kama ni HR, unapokea CV ya mtu ambae hatulii na ofisi moja; huwezi kuhisi there's something wrong with him/her?!
Na hilo wala halishangazi kwa sababi Agent mmoja kutoka South Africa amesema wazi kwamba:-
According to tovuti ya kickoff.com, huyo Agent anamfahamu vizuri Eymael kwa sababu amewahi kufanya nae kazi!
Kwahiyo mengine aliyosema ni porojo tu kwa sababu Eymael sio mgeni wa viwanja vya hovyo kwa sababu sehemu kubwa ya career yake amefanyia Afrika, tena South of Sahara!