Ukistaajabu ya tozo, tazama wafanyabiashara tunavyoumizwa na serikali

Biashara TZ ina siri zake kutegemeana na aina ya biashara. Sasa ww mtu mpya kimbilia maleseni ya taasisi zote za serikali badala ya kufanya biashara uone kama huo mtaji utabaki. Utailisha nchi ila familia yako itakufa njaa.

Tumia akili kama huna Tafuta mtu anayefanya biashara kama unayotaka kufanya umuazime akili zake za kukwepa mishale.

KUNA MSEMO"UKIONA TAASISI ZA SERIKALI ZINAKUANDAMA BASI USHAKUWA MKUBWA, KAA NAO NA UTII SHERIA BILA SHURUTI".
Ni sawa
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Biashara mbona hua nasema kila siku nitafanya magendo hadi nakufa, nitakwepa kodi hadi kieleweke haiwezekani mrundikano wa kodi zote hizo wakati hawanichangii hata mia kwenye kutafuta mtaji haipo hiyo angalia maeneo unayotakiwa upeleke pesa TRA, TMDA , TBS, FIRE, OSHA , HALMASHAURI, ULINZI SHIRIKISHI, USAFI, BIASHARA UJILINDIE MWENYEWE, hapa ni gendo mwanzo mwisho unawasoma unatoboa kama kawaida
 
Halafu makadirio yao una mtaji laki tano unakadiriwa milioni moja na mtu ambaye sio mfanyabiashara kakaa tu ofisini ametulia hajui hata biashara ni nini, mfano Taasisi moja ichukue hela mara mbili kwenye bidhaa ileile mfano bidhaa inaingia nchini TBS na TRA na wenzao bandarini wanavuta chao halafu haohao dukani wanataka walipwe tena yaani unakabwa hadi unakubali mziki mazingira hovyo sana Tanzania biashara nyingi zinakufa kila siku, bidhaa zinakua juu sababu ya ujinga wao
 
Bunge kimyaaaaaa kabisa, nasikia hata kodi hawalipi na mishahara wanajilipa kuliko hata maseneta wa nchi tajiri kuliko zote duniani, tuna wahuni tuu na wezi pale mapinduzi yanahitajika
 
Fikiria kwa akili ya kawaida ununue gari milioni kumi kodi peke yake na malipo yao mengine milioni tano hadi saba halafu wanaolipwa kwenye gari hawana mchango wowote sio wazalishaji yaani wapo tu ndio maana magari bei juu, mzunguko wa mafuta na vipuri bei juu, na wanaomiliki magari wachache sababu serikali haiwazi mbele inajua magari ni anasa na starehe wakati ni vyombo vya huduma vilitakiwa kuwekewa kodi himilivu ili watu wengi wamiliki,
 
Soma hii ripoti kwanza [emoji116]
We Madelu The Sunk Cost Fallacy sera mlizoweka ndio zinachochea watu kukwepa kodi. Kumekuwa na utitiri wa kodi, urasimu, ubabe, kuto kuwajibika na mambo mengine mengi ambayo kwa pamoja mtu anaona bora afanye ujanja ujanja ili aweze kuihudumia familia yake.

Tambueni ya kuwa wafanya biashara wadogo na wa kati hawatafuti utajiri katika hizo biashara zao, bali wanafanya kila liwezekanalo ili huhakikisha wanahudumia familia zao basi.

Badala ya kuja na maneno yenye maudhi kama haya kwa Watanzania, ilikuwa ni busara sana kama mngetumia jukwaa hili kujifunza kero zinazo wapata Watanzania katika shughuli zao za kila siku na pia mngeweza kupata mawazo mazuri na chanya ya namna bora ya kukusanya mapato ambayo kila mtu atatoa bila kuona kama anaibiwa au kunyanyaswa.

Tatizo mmejiweka kuwa wafalme/watawala badala ya viongozi, mfalme sikuzote hajali wewe unakula vipi, unalala vipi au unapataje kuishi! anachohitaji yeye ni watu kulipa kodi na tozo ili yeye na familia yake waweze kula na kusaza. Kumbukeni yaliyotokea kwa mtoto wa mfalme Sulemani.
 
Halafu makadirio yao una mtaji laki tano unakadiriwa milioni moja na mtu ambaye sio mfanyabiashara kakaa tu ofisini ametulia hajui hata biashara ni nini, mfano Taasisi moja ichukue hela mara mbili kwenye bidhaa ileile mfano bidhaa inaingia nchini TBS na TRA na wenzao bandarini wanavuta chao halafu haohao dukani wanataka walipwe tena yaani unakabwa hadi unakubali mziki mazingira hovyo sana Tanzania biashara nyingi zinakufa kila siku, bidhaa zinakua juu sababu ya ujinga wao
Bado malipo ya kumlipa editor firm kwenye kufile annuall return
 
We Madelu The Sunk Cost Fallacy sera mlizoweka ndio zinachochea watu kukwepa kodi. Kumekuwa na utitiri wa kodi, urasimu, ubabe, kuto kuwajibika na mambo mengine mengi ambayo kwa pamoja mtu anaona bora afanye ujanja ujanja ili aweze kuihudumia familia yake.

Tambueni ya kuwa wafanya biashara wadogo na wa kati hawatafuti utajiri katika hizo biashara zao, bali wanafanya kila liwezekanalo ili huhakikisha wanahudumia familia zao basi.

Badala ya kuja na maneno yenye maudhi kama haya kwa Watanzania, ilikuwa ni busara sana kama mngetumia jukwaa hili kujifunza kero zinazo wapata Watanzania katika shughuli zao za kila siku na pia mngeweza kupata mawazo mazuri na chanya ya namna bora ya kukusanya mapato ambayo kila mtu atatoa bila kuona kama anaibiwa au kunyanyaswa.

Tatizo mmejiweka kuwa wafalme/watawala badala ya viongozi, mfalme sikuzote hajali wewe unakula vipi, unalala vipi au unapataje kuishi! anachohitaji yeye ni watu kulipa kodi na tozo ili yeye na familia yake waweze kula na kusaza. Kumbukeni yaliyotokea kwa mtoto wa mfalme Sulemani.
Hatari
 
Lipa Kodi acha porojo,sera zimekuwepo hivyo miaka na miaka.
 
Attachments

  • Screenshot_20220824-141037.png
    Screenshot_20220824-141037.png
    86 KB · Views: 6
Hakuna tofauti na wale wezi wengine
Tofauti ipo dmkali hawa wanalindwa na sheria wale dhamana za mahakamani...yaani mtu anatoka huko kwenye kikao eti cha Tozo ya bando akiamka bank akiamka sijui viingereza vya Railway Levy hawataishia hapo hawa...
 
Back
Top Bottom