We Madelu
The Sunk Cost Fallacy sera mlizoweka ndio zinachochea watu kukwepa kodi. Kumekuwa na utitiri wa kodi, urasimu, ubabe, kuto kuwajibika na mambo mengine mengi ambayo kwa pamoja mtu anaona bora afanye ujanja ujanja ili aweze kuihudumia familia yake.
Tambueni ya kuwa wafanya biashara wadogo na wa kati hawatafuti utajiri katika hizo biashara zao, bali wanafanya kila liwezekanalo ili huhakikisha wanahudumia familia zao basi.
Badala ya kuja na maneno yenye maudhi kama haya kwa Watanzania, ilikuwa ni busara sana kama mngetumia jukwaa hili kujifunza kero zinazo wapata Watanzania katika shughuli zao za kila siku na pia mngeweza kupata mawazo mazuri na chanya ya namna bora ya kukusanya mapato ambayo kila mtu atatoa bila kuona kama anaibiwa au kunyanyaswa.
Tatizo mmejiweka kuwa wafalme/watawala badala ya viongozi, mfalme sikuzote hajali wewe unakula vipi, unalala vipi au unapataje kuishi! anachohitaji yeye ni watu kulipa kodi na tozo ili yeye na familia yake waweze kula na kusaza. Kumbukeni yaliyotokea kwa mtoto wa mfalme Sulemani.