Ukitaka kufanikiwa kibiashara, kaa mbali na walioajiriwa, hawawezi kukushauri kitu

Ukitaka kufanikiwa kibiashara, kaa mbali na walioajiriwa, hawawezi kukushauri kitu

Uchuuzi? Yaani mtu atoe Mali dukani au store kwake au shambani kwake au ashushe mzigo toka china umuite mchuuzi, au unaongelea biashara za kina Mo, kama ni hivyo endelea kubwabwaja maana sidhani kama wanahitaji ushauri wako.
Ila deep down najua unawashauri unga mwana unga mwana wenzako wa kariakoo, afu unashangaa mmiliki wa frame mwenyewe mwajiriwa na mnamlipa Kodi.

Hayanaga mwongozo
Hizi ndio kauli za mwajiriwa
 
Biashara ni upambanaji, ukilala na biashara nayo inalala.

Ila kwa mwajiriwa, ata akilala mwisho wa mwezi utasoma.

Usitegemee mtu aliyeajiriwa akupe ushauri chanya kwa kitu ambacho yeye kimemshinda kufanya.

Jenga urafiki na wafanya biashara wenzako, hawa walioajiriwa watakupoteza; wanakauli zao za kijinga, chezea mshahara usichezee kazi.​
Upo sahihi 100%
 
Mnapenda kutiana ujinga. Kuna DC mmoja alitoa wimbo sitaki kazi.

Leo hii ni DC.

Kigwangala alisema ajira zipo nyingi tusisubiri kuajiriwa tuwaze nje ya box.

Mwezi uliopita na yeye anaomba ajira na wiki iliyopita akazungumzia ugumu wa maisha baada ya vyeo.

Mwana FA alisema hataki siasa anafocus na business leo hii kaajiriwa na jamhuri.

Waajiriwa hua tupo kimya ni nyinyi mnatufuata fuata. Mnakua kama wanandoa kulazimisha tusiooa tuoe.
Hapa tunazungumzia mfanyabiashara 'original' anayetegemea biashara yake bila kuwa na 'backup' ya ajira au nafasi yoyote ya kisiasa.
 
Jamaa waloajiriwa wana ujinga mwingi sana, kuna mmoja miaka 15 imepita baada ya kumaliza chuo ananiuliza kuhusu mitihani ya bodi, mara kile cheti muhimu sana. Sheeenz
 
Mkuu ukianza kuwatenga watu basi jua wewe sio mfanyabiashara aliyekomaa. Biashara inahitaji watu wa aina zote. Mtu unayemwona hawezi kukushauri utakuta ndo mwenye madini ya kutosha. Hata wale wakosoaji mara moja moja pata muda wa kuwasikiliza.
Hii takataka ya Samuya inasema nini
 
Back
Top Bottom