Habarini wakuu ni mimi tena kijana wenu humu jamiiforums, leo nimeamua kutoa ujumbe wangu kwa vijana wenzangu kama mimi
Unajua nini,, hizi smartphone nowadays zinatupotezea muda wa kufanya mambo ya umuhimu katika maisha. Unakuta vijana wengi tunapoteza muda kwenye social media (facebook, instagram, whatsapp, youtube na hata humu jamiiforums), nimeshatumia sana hii mitandao ya kijamii hakuna faida yoyote ninayoipata zaidi ya kupoteza pesa kwenye mabando, kucheza kamari na mambo mengine mengi hasa kucheck porn.
Isitoshe naona matumizi ya smartphone yanatutoa kwenye reli ya kupambana na maisha, vijana tunakuwa malazyness, na hatufocus kwenye future, hizi smartphone kwakweli zinatufelisha sisi vijana tunapoteza muda wa kufanya mambo ya maana kutwa nzima tuko mitandao ya kijamii na hatupati faida yoyote
Kuanzia leo mimi naacha matumizi ya smartphone nifocus na maisha yangu, hivo wakuu mkiniona nipo kimya humu jamiiforums jueni tu kuwa nimeshauza simu yangu ili ni concentrate na maisha seriously ungana nami kijana mwenzangu tuache kupoteza muda na haya masocial media yasiona umuhimu wowote kwenye maisha yetu ya kesho
#natanguliza shukurani wakuu