Ukitaka kufanya mambo yako kwa Amani, usiamini Mtu.

Ukitaka kufanya mambo yako kwa Amani, usiamini Mtu.

Surya

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2015
Posts
8,774
Reaction score
13,566
Ni bora ukakaa na Mchawi kuliko kuwa na mtu ambaye sio mchawi ila muongo muongo na tapeli

Nitoe ushuhuda tu wa matukio mawili yalio nikuta jana
- Kuna sehemu nilikwenda kwenye pita huku na huku na kijana wangu, tukafika sehemu kupata Juice (Juice Point)
Kwa amani ngoja niulize bei ya juice tukaambia 5k nikaagiza passion embe, zikawa zimeisha, kijana wangu akaagiza juice ya Tende na mamichanganyo mengine mim hayo siyawezi
Basi kwenye kukosa nilichokitaka, kwa kubembelezwa sana kuwa ni nzuri, ikabidi nikubali waniletee juice ya matikiti, aloooo acha nikute ni lile tikiti lina manyuzi nyuzi, mixer na juice haijachunjwa..
Kiukweli mazingira ya juice Point ni mazuri ila juice ilikua mbaya, hata sikuimqliza nikaacha.

Nikawaza elfu yangu, ukute nakunywa na juice maji ya bomba 😮‍💨😮‍💨😮‍💨
Moyoni nikasema kizur pika kwako

- Tukio la pili
Nikamuamini fundi simu, kiukweli nikua nimechoka na sikutaka usumbufu,
nokia kitochi kubadili system charger ni sh. ngap ? fundi akasema 5k, nikampa
Kiufupi jamaa hakutengeneza simu, niliondoka na simu bado haipelek
kesho yake narud, nikachomeshwa mahind masaa 2 bila kupewa maelezo.

Sikutaka kumfatilia nikamuacha afanye kazi kwa uhuru nikijua ni kazi nyepesi. Nikakutana na kitu kizito.

Mchawi wa Ujasiriamali kwa sasa ni Uaminifu.
wafanyabiashara wengi uaminifu zero, inabidi hata kama kazi niya buku mtu hadi asimamiwe kweli ???

Aisee bora kuwa mkali muda wote, ukiwa mpole na hutaki kufanya mambo yako mwenyewe, utampa hata mtu nguo akufuri zirudi zimeingiliana rangi 😃😃😃😅

Nikimuamini tena binadamu hasa Mwanamke mnii Happiness nimekaa pale 👉👉👉
 
Back
Top Bottom