Ukitaka kuijua kesho ya Watanzania wasikilize viongozi wake, unaweza kulia

Ukitaka kuijua kesho ya Watanzania wasikilize viongozi wake, unaweza kulia

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Hii ndio Tanzania unayo ijuwa Hayati baba wa Taifa huko kaburini ana wish afufuke aje awachape viboko. Taifa alilo lijenga na kuweka misingi yake limetumbukia zama mpya zama zinatisha kuliko zama za ukoloni.

Mwalimu ktk moja ya hotuba zake kuna wakati alilisema hili nadhani watu wachache sana walimuelewa wengine wapo wengine walisha lala mauti. Mwl aliwahi sema anashanga serikali inaongozwa na watu wasomi wengi ila mambo nikama miaka ya 61 wakati tunapata uhuru" mwisho wakumnukuu. Mwl alikuwa akisema maono ya leo na alikuwa akionyesha haya yanaendelea sio dira wala muongozo aliwaachia wana CCM.

Alienda mbali kwa uchungu sana ktk hizi hotuba zake akasema ccm sio baba wala mama yake na kwa bahati mbaya sana Mungu hakumpa nafasi kuwepo leo uwenda kwa mtazamo wangu ccm2 ingeshakamata nchi.

Unaweza ukajiuliza nakuwaza sana why nina andika huu uzi ila nitaomba nikurudishe nyuma kidogo kwenye dira na mpango mkakati wa Mwl kulijenga taifa hili ndipo ujuwe hiki kiumbe hakikuwa cha kawaida na ndio maana wazungu walitaka fuvu lakichwa wwmchunguze uwezo wake ulikuwaje.

Kama ulikuwa hufaham basi leo bora ufaham mwl alichukuwa hili taifa kipindi dola mbili duniani zikivutana ujamaa na ubepari na pia ikimbukwe taifa hili lilikuwa chini ya wakoloni Waingereza na hawa walikuwa mabepari how alipewa kiti yeye ambaye alikuwa na koti la ujamaa ila moyoni akiwa na siri nzito sana.

Pili ilikuwaje katikati ya waswahili walio kuwa wengi yeye mkristo akatoboa na kuwa Mwanzilishi na Rais wa kwanza wa Taifa hili utabaki mdomo wazi.

Tatu akaondoka madarakani watanzania wakimpenda akakiongoza chama akiwa sio mwenyekiti wala katibu wa ccm yani ndipo utamuita mchawi. Ktk yote siri ni moja akili. Mwisho wakunukuu.

Leo tumeweka mifumo mizuri yakielimu na kiserikali ila tunazalisha majizi kama yale ya ilala.

Leo tuna wasomi ukiwasikiliza hotuba zao unazima redio nimajigambo vijembe na pozi yes mm ndio nipo hapa mfalme. Ndugu zangu kesho yetu niyamashaka.

Nenda kwenye mataasisi ndipo unaweza kutoka machozi. Watengenezaji wa sera. Sera zakukamua nakutoana machozi. Unamsikia mtu kiongozi mkubwa tu anasema msipime viwanja vya sq 400m. Unakaa unajiuliza je huyu anajuwa vipato na mifuko ya wa Tz au anataka watu fulani tu wajenge same mtu yuko kwenye mifumo ya serikali. God have a mercy on us.

Unamsikia mwingine anasema Royo towa imekuza utalii toka uhuru jamani PH holder.. baba natubu kwa Taifa langu.

Kiongozi mwingine akaibuka akasema tunataka bot iingie crypto currency unajiuliza huyu mtu anajuwa anachokisema ama kunajizi lipo nyuma linataka afanye jambo hata yeye akijisikia ajikane. Unajiuliza huyu mtu anajuwa uchumi wetu kweli anajuwa balance of payment au anataka amke asubuh ambiwe hana hata usd pale bot ndipo Siri Lanka.

God have a Mercy on Us.
 
Hakuna mtu anawajibika kwa ajili ya maisha yako, amka mlamu.
 
Unasema Nyerere alikuwa anapendwa?

Unajua alipona majaribio mangapi ya kutaka kupinduliwa?

Unajua hali ya kiuchumi ya Tanzania miaka yake ya mwisho ya utawala ilikuwaje?
 
Unasema Nyerere alikuwa anapendwa?

Unajua alipona majaribio mangapi ya kutaka kupinduliwa?

Unajua hali ya kiuchumi ya Tanzania miaka yake ya mwisho ya utawala ilikuwaje?
Kwa hiyo anaependwa ni Samia tu?
 
Inawezekana Mwalimu Nyerere alichangia kwenye hilo,
Taifa la "Ndio Mzee, Ndio mheshimiwa, ndio Mama"

na hii Kaulimbiu

"Zidumu fikra za Mwalimu"

(Wazee mtatusahihisha, sisi wengine ni Vijana hatukuepo.)

Mi nadhani mambo kama haya pamoja na kumpa kiongozi mmoja madaraka yote ndio yanachangia kudumaza ubunifu, matumizi ya akili na uwajibikaji.

Viongozi wa Chini wanajua hata wakivuruga lawama Asilimia kubwa zitaenda kwa Rais.
Si unaona watu walivyomkana JPM.
 
Mkuu

Ndio màana Warioba alijitosa kwenye katiba Mpya Angalau kupunguza madaraka ya Rais akiwa madarakani!!
Ameona ajotose mapema KWENYE hilo kabla Baba mwenyezi hajamwita!!

Tuombe katiba IPATIKANE angalau tuokoe Taifa japo tumechelewa!!

Hili Taifa linahitaji mtu Mwenye zero moyoni ya kutotaka kutajirikia Ikulu ndio atwae madaraka!!
Tatizo the state imejilimit KWENYE vetting haiwezi kuniona mtu kama mimi nosie waza kutajirikia Ikulu bali kutumika na kuchangia hata kile kilocho nacho KWA ajili ya maendeleo ya Taifa hili!!
Nilihitajika Mimi lakini nitapenyea wapi mimi Ili wanione hao the state!!??vyama vya SIASA rushwa imetamalaki sisi tusiotaka kuhonga Ili tuwe VIONGOZI tunapitia WAPI!!!?

TATIZO DEEP STATE IMEJILIMIT KUFANYA VETTING PIA WALICHELEWESHA KATIBA MPYA NA MADHARA YAKE NI MAKUBWA NA HADI SASA NASIKITIKA SANA ETI HADI 2026 NDIO KATIBA IPATIKANE!!WAKATI MIMI NIPO HAPA NINGESIMAMIA KATIBA MPYA IKAPATIKANA NDANI YA WIKI MOJA AU MBILI TU NA WARIOBA TAYARI KESHAIZINDUA NA KUANZA KUTUMIKA!!!
DEEP STSTE INAFANYA TARATIBU SANA MAMBO YAKE NA MADHARA YAKE NI MAKUBWA SANA INAVUMILIA UJINGA MWINGI MNO HADI SASA!!!
KAMA DEEP STATE MPO HUMU MNIPE MIAKA MITATU TU YA KUMALIZIA AWAMU YA JPM NAKAMILISHA KATIBA MPYA NA KUIRUDISHA NCHI MAHALI PAKE!!!
MIMI NI TAJIRI MOYONI SITOINGIA IKULU KUCHUMA UTAJIRI BALI KUCHANGIA HATA MSHAHARA WANGU KWA AJILI YA MAENDELEO YA NCHI HII!!!
NASHANGAA WANASIASA WANAJILIPA MAHELA MENGI WAKATI WANANCHI HAWANA HATA HUDUMA ZA KAWAIDA KABISA KAMA UMEME NA MAJI!!MIMI NISINGE KUBALI MISHAHARA MIKUBWA KWA WANASIASA KABLA WANANCHI HAWAJAPATA HUDUMA ZA MAJI,UMEME NA AFYA HAPA NCHINI!!
HAKI YA MUNGU TENA AISEHHHHH!!!
DEEP STATE MNANIKERA SANA MNAACHAJE HAYA HAP NCHINI!!!
NJOONI MNICHUKUE NIANZE KAZI!!!
 
Deep state kwa sasa iko msoga unatarajia nini?
 
Viongozi wa nchi mara nyingi huwakilisha aina ya wananchi wao walio wengi.
 
unapolaumu vijana wa sasa au Taifa la leo, unapaswa kuanza kulaumu wazee/mababu nk ambao ndio walikuwa walezi wa hili Taifa la leo. Tena walezi wengi bado wako hai na wanaona kila hatua ya vijana wao bila kupaza sauti kama kuna makosa yanatendeka.

Tabia ya leo ni matokeo yamalezi ya Jana.

Unayemtaja ndio alitengeneza mfumo na kukuza vijana kwa wazee ambao ndio hawa tunaowalaumu, Bila shaka kwa tafsiri hiyo naye hakuwa mlezi bor.
 
Inawezekana Mwalimu Nyerere alichangia kwenye hilo,
Taifa la "Ndio Mzee, Ndio mheshimiwa, ndio Mama"

na hii Kaulimbiu

"Zidumu fikra za Mwalimu"

(Wazee mtatusahihisha, sisi wengine ni Vijana hatukuepo.)

Mi nadhani mambo kama haya pamoja na kumpa kiongozi mmoja madaraka yote ndio yanachangia kudumaza ubunifu, matumizi ya akili na uwajibikaji.

Viongozi wa Chini wanajua hata wakivuruga lawama Asilimia kubwa zitaenda kwa Rais.
Si unaona watu walivyomkana JPM.
Nyerere hii katiba mbovu iliandikwa ktk kipindi chake na Msekwa na wenzie.

Nyerere alitawala kwa katiba hii kwa kuwaadhibu wapinzani wake kwa kuwaweka kizuizini na wengine kuishi uhamishoni nje,

Nyerere alivyoona hali ya uchumi inazidi kuwa ngumu, chakula, mavazi pia karibia kuishiwa mafuta ya petrol, (magari jumapili yalitembea kwa vibali,) akajiuzulu,
Kupoza makali ya neno kujiuzulu ni kushindwa, akaja na neno kungatuka

Kama aliona katiba ni mbovu kwanini hakifanyia marekebisho? Badala yake anatuambia ooh hii katiba inaweza kumfanya Rais kuwa dicteta,

Hii ya watu kuwa chawa, kusifia ujinga, kuunga mkono juhudi, fitna, majungu hayajaanza sasa, yapo ila kila wakati na kiasi chake,
 
Back
Top Bottom