Ukitaka kujua hii nchi kuna huduma mbovu, nenda Hospital ya Serikali.

Ukitaka kujua hii nchi kuna huduma mbovu, nenda Hospital ya Serikali.

Umeandika ukweli mtupu hospital binafsi nyingi pia majanga Wana kauli mbiu Yao wanasema " muwashie moto" ukisikia hivyo ujue unaweza Kuta laki 3 imeishia kwenye vipimo tu hujapata hata panadol .

Hospital za serikali ni nzuri maana hawana haja ya ku fake vipimo Wala dawa kama private changamoto Yao kubwa ni kwamba ziko congested sasa wagonjwa wengi subra inawashinda.
Private ni pesa kwanza.

Suala la kupona utajua mwenyewe.

Na ndio maana kwa PRIVATE hata siku moja huwezi kufanya kipimo, kitatoka NEGATIVE labda iwe UKIMWI.

Vipimo vyote lazima vitoke POSITIVE ili ununue DAWA.
 
ila wa tz kwa kulalamika wewe unafikili zile dawa na vifaa tiba vilanunuliwa kwa karatasi? unataka upewe huduma bure tu au vipi /serikali imejitahidi walau watoto wa chini ya miaka 5 na wajawazito huduma zao ni bure na wewe mtu mzima unataka utibiwe bure
 
Yaani uwe na bima usiwe nayo ,ila huduma ni mbovu kwenye hospitali za serikali. hili sikupingi. Wajati tunaomba Mungu atupe mkate ,pia tusisahau kuzikabidhi AFYA zetu kwa Mungu. Maana AFYA ndio mtaji.
 
Umesahau vyoo vya kulipia vya serikali pia
 
ila wa tz kwa kulalamika wewe unafikili zile dawa na vifaa tiba vilanunuliwa kwa karatasi? unataka upewe huduma bure tu au vipi /serikali imejitahidi walau watoto wa chini ya miaka 5 na wajawazito huduma zao ni bure na wewe mtu mzima unataka utibiwe bure
Nadhani mleta mada nilivyoumuelewa hajamaanishq watu wanataka kutibiwa bure. Anazungumzia ubovu wa huduma zinazotolewa hata kama gharama za matibabu unagharamia wewe.
 
Umesahau vyoo vya kulipia vya serikali pia
Vyoo vya kulipia ni mapato ya halmashauri.

Sheria za halmaahauri zinatungwa na madiwani.

Nyie hamhusiki kila mtu yuko busy kutafuta hela anunue bando aje kulalamika mitandaoni, wakati ambao wakati sheria inatungwa hakuona maana yoyote
 
Sisemi uende fisi za halmashauri, manispaa au wilayani. Najua huko kuna matakataka yake, but atleast hawadeal na afya na uhai wa binadamu.

Nenda hospital za serikali. Unakufa wanakuangalia. Tukipata hela twendeni hospital kubwa za private.

Ukiweza kua na "daktari" wako. Ninayoyaona hapa niseme umasikini ni laana.
Naam
 
Tatizo la Hospitali nyingi za serikali ni la kiongozi zaidi. Hospitali za serikali zenye huduma nzuri ni kwa sababu kiongozi wa hiyo hospitali anaishi vizuri na watumishi wake na anawasimamia vizuri katika majukumu yao. Ukiona hospitali huduma ni mbovu ujue shida ni ubinafsi wa viongozi.
Hakuna mahali ambapo watumishi wana motisha nzuri halafu kuwe na huduma mbovu
 
Hatari mkuu!! Week iliyopita nilikuwa hospital ya serikali pia,,

Tuyaache tu....Tupambane tupate pesa
Utatafuta pesa utapata lakini ndugu jamaa na marafiki wapo ambao hawatazipata na mwisho wa siku utalazimika kwenda kuwaona wakipelekwa huko kwenye hizo hospital. Huwezi kukimbia hizo kero,, Jambo la muhimu no kuhimiza serikali kufanya kazi yake kupunguza huduma mbovu
 
ila wa tz kwa kulalamika wewe unafikili zile dawa na vifaa tiba vilanunuliwa kwa karatasi? unataka upewe huduma bure tu au vipi /serikali imejitahidi walau watoto wa chini ya miaka 5 na wajawazito huduma zao ni bure na wewe mtu mzima unataka utibiwe bure
Kakudanganya nani watoto bure wewe????????? Mi nilienda na mtoto wa miezi nane uji ulipita kwenye njia ya hewa...imetughalimu zaidi ya laki mbili....(Silaumu ila ukweli watoto nikulipia mkuu..usije peleka mtoto hauna mia mfukoni itakula kwako,labda uwe fukara kwelikweli ndio utaenda ustawi wa jamii wakusaidia

Na jamaa mleta thread hajalalamika kuhusu huduma kulipia ..bali kalalamika huduma zipo mbovu hawakujali
 
Nchi tajiri yenye matajiri kibao iweje huduma za afya ziwe mbovu?

Acha uongo wewe.
 
Nakubaliana na mtoa mada.
Kuna siku ilikuwa jumamosi kuna jamaa yangu alipata ajali hivyo tukampeleka hospitali ya serikali iliyopo karibu, kufika hospitalini tunaambiwa eti daktari yupo kwenye jumuiya anasali. Hivyo kulikuwa na manesi tu kwenye ile hospitali na manesi wenyewe walikuwa wanatupita kama hawatuoni. Nilikasirika sana ile siku Asee.
 
Nakubaliana na wewe.

Ila kama kweli una pesa na unataka huduma nzuri nenda huko huko kwenye hospitali za serikali.

Shida mkiwa na pesa mnaenda hospitali za binafsi mnatoa pesa bila kushurutishwa tena mkiwa wapoleee.

Ila mkienda hospitali za umma, hamna hata 100 ila mnabweka kama mbwa koko kwasababu kuna mwanasiasa kawaambia matibabu ni bure.

Huko private wewe waoneshe pesa uliyonayo, watahakikisha wanakuandikia vipimo na matibabu yote kulingana na pesa yote uliyonayo wahakikishe wanaongeza mapato.

Na vipimo vitaonesha unaumwa kila kitu, na dawa utaandikiwa zote, zigo la dawa.

Na kibaya zaidi unaweza hata usipone.
Chief unatumia soda gani? Umetema madini mazuri kweli
 
Back
Top Bottom