Nakubaliana na wewe.
Ila kama kweli una pesa na unataka huduma nzuri nenda huko huko kwenye hospitali za serikali.
Yaani mtu awe na pesa au premium health ensurance coverage halafu aende akatibiwe kwenye government hospital ambapo daktari anaenda kunywa chai saa tatu anarudi saa tano? Yaani kabisa unawaambia watu hapa eti wakitaka huduma nzuri waende kwenye hospitali za serikali?
Shida mkiwa na pesa mnaenda hospitali za binafsi mnatoa pesa bila kushurutishwa tena mkiwa wapoleee.
Kwa hiyo wakienda huko government hospitals ndio huwa hawatoi pesa na wakitoa wanatoa kwa kushurutishwa tena kwa ukali au?
Ila mkienda hospitali za umma, hamna hata 100 ila mnabweka kama mbwa koko kwasababu kuna mwanasiasa kawaambia matibabu ni bure.
Mbona unaandika ujinga wewe jamaa? Ni hospitali gani sasa hivi ya serikali ambayo inatoa huduma bure? Watu wanalipia mpaka bomba la sindano halafu wewe unasema nini hapa? Hivi si ni juzi tu hapa kuna mtu aling'atwa na nyoka akafia hospitalin bila kupewa huduma sababu alikuwa hana 150k ya kulipia matibabu? Na pia kati ya mgonjwa na watoa huduma hasa manesi ni nani anayeongoza kwa kubweka?
Huko private wewe waoneshe pesa uliyonayo, watahakikisha wanakuandikia vipimo na matibabu yote kulingana na pesa yote uliyonayo wahakikishe wanaongeza mapato.
Hebu acha exaggerations za kipumbavu hapa, ni hospitali gani ya private wakakuuliza kwanza hela uliyonayo ndio wakaanza kukupa matibabu? Ndio tunafahamu kwamba private hospitals ziko kibiashara zaidi lakin si kwa namna ulivyoelezea hapa.
Na vipimo vitaonesha unaumwa kila kitu, na dawa utaandikiwa zote, zigo la dawa.
Upuuzi kama huu unafanyika kwenye hivi vidispensary na vipharamacy uchwara ambavyo vinamilikiwa na hao hao manesi na madokta walioajiriwa kwenye hospitali za serikali kwa sababu ya uduni wa mishaara wanayolipwa na serikali na hivyo basi wanaamua kujiongeza pembeni huku wakitumia afya za watu kama mitaji ya kujiongezea vipato hili waweze kulipa madeni kibao wanayodaiwa. Upuuzi kama huu unaousema hauwezi ukaukuta hospitali kama Agakhan.
Na kibaya zaidi unaweza hata usipone.
Wote tunafahamu kutibiwa kwenye hospital bora haikupi guarantee ya 100% kwamba utapona tu, watu wanaenda kutibiwa India lakin bado wanarudi maiti.
Ila iko wazi huduma bora ya kiafya inayotolewa private hospitals inakupa assurance kubwa ya kupona tatizo lako na kupunguza probability ya kupoteza uhai, kinyume kabisa na huduma zitolewazo na government hospitals ambapo hata ukimpeleka mgonjwa wa malaria tu kupona ni 50/50 sababu ya uduni wa vifaa na uzembe wa makusudi kutoka kwa watoa huduma.
Wewe jamaa umeadika hii comment kwa minajiri ya kutetea huduma zitolewazo na hospitali za serikali na kuonesha kuwa ni bora kuliko hospital binafsi, ila mwisho wa siku umeishia kuandika upuuzi mtupu.