Ukitaka kujua hii nchi kuna huduma mbovu, nenda Hospital ya Serikali.

Mimi nawashangaa sana hawasema sijui tutafute pesa sana, sasa hizo pesa zinakuwezesha wewe na familia yako kupata matibabu ya uhakika kwenye hospital nzuri.

Je, wale ndugu zako uliowaacha kijijini wao wanatibiwa wapi kama sio kwenye hospitali hizi hizi za kayumba? Nilichojifunza watanzania wengi hawafikirii kingine zaidi ya wao wenyewe binafsi na familia zao kwenye jambo lolote lile la kijamii.

Ukienda hapo Rwanda tu hospital za serikali na binafsi zinatoa huduma almost sawa, yaani mgonjwa akishindikana kwenye hospital ya serikali wanampeleka nje ya nchi...

Kwetu sisi hapa tumebaki kuendekeza ubinafsi tu na wizi wa pesa za umma.
 
Sahivi wamejazana hawa vijana wa ajira mpya, na hawa wa Intern, yanayofanyika huko ni hatari tupu.

Cuzzo angu ni mlemavu, ko huwa anajifungua kwa Op, safari hii, tume. muwahisha hosp, nurse na Dr wanasema eti bado muda wa kujifungua, akati mgonjwa analalama uchungu, siku ikaisha, siku ya 2 bado wanaleta ujinga ule ule, afu nurse ka binti tUh kanajibu anaweza kujifungua kawaida, akati mtu watoto 3 wote alijifungua kwa OP. nikasema huyu analeta utani ktk maisha ya watu, nkamuambia huyu mgonjwa na mtoto tunaetegemea kumpokea, wakifariki utajua vizuri nini kinakuweka hapa na majukumu yako ni yapii, nkaona haitoshi panda kwa ma Dr nawaweleza kwa jazba, ndo wanaanza kuandaa docs za OP eti nisaini, pumbavu kabisaa.

Nilishapanga. Ingetokea tofauti mbona ningewafurahisha haswaa.
 
Juzi nilikuwa mloganzila, ngoja ninywe maji kwanza
 
Aisee tena hao madaktari na manesi vijana ndio wa ovyo sana, hawana kauli nzuri na wamejawa na mihemko kweli, na hata kwenye utendaji wao hawako makini kabisa...wao suala la kurudia operation ni kawaida kabisa, mbaya zaidi ndio wamejaa kwenye hospitali kubwa kubwa zote zikiwemo za kanda.
 
Wamejazana vijana na mabinti, wanachojua wao kufokea wagonjwa na wauguzi wao, kuchat na kusogoa hovyoo.
Nasemajee mie nitawabaruza kila ntapokua ktk sehemu zao za kazi nikihitaji huduma.

Pumbavu zao.
 
Kidogo zinajitahd wale manesi wa zamani wanazidi kustaafu....
Hao ndio walikuwa wauguzi sasa, sio hawa wa sasa hivi ambao muda mwingi wanashinda instagram kuangalia umbeya wa akina Aziz Ki na mabeto.
 
Wamejazana vijana na mabinti, wanachojua wao kufokea wagonjwa na wauguzi wao, kuchat na kusogoa hovyoo.
Nasemajee mie nitawabaruza kila ntapokua ktk sehemu zao za kazi nikihitaji huduma.

Pumbavu zao.
Vipumbavu sana halafu ukivifokea unakuwa umeamsha moto sana, kuna kamoja kaliniambiaga eti "kaka hata mimi pia ni binadamu, kwanza bora yako hata wewe umekula" nilikasirika sana nikataka kukajibu dingi mdogo niliyekuwa nae ananituliza kwamba nisiongee chochote.
 
Wajaribu kunijibu vibaya mie, mbna watafurahi, nilimkomesha afisa mtendaju wa kata, tena kakijana, eti ooh ntakushitaki, nkampa darasa la sheria, mbona alinyweaa mwenyewe, khaaah
 
wana vburi sana na dharau kkenge hao.
 
Hospital za Serkali ni uharo+ Mavi ya nyoka. Nilienda Hospt ya manispaa fln tangia saa3 tuna msubiri Dr kaenda kunywa chai hadi7 halafu akatibu lisaa tu akasema Musa umeisha kama utani akatokomea walaaniwe wote
Pole sana ndugu, mimi nakumbuka ilikuwa siku ya Idd tulimpeleka mgonjwa wetu afanyiwe vipimo vya CT scan kichwani ambapo lilikuwa ni hitaji la haraka, tukaambiwa eti daktari anayehusika ameenda kula sikukuu mpaka kesho na ni hospital ya mkoa.

Yaan binafsi mpaka kuna muda huwa naona kuzaliwa bongo ni moja wapo ya laana.
 
Nilienda kucheck Hepatitis B ili nianze chanjo ilikuwa 2022!

Kipimo ni kama cha ngoma tu ni rapid test na nilikuwa mtu wa kwanza pale Lab,kupewa majibu ilikuwa mtiti hadi nikawa mbogo.

Watu wako busy na simu asubuhi saa 2 na dakika tena Jumatatu,imagine!
 
Kwamba eti watumishi wa afya nao ni binadamu hivyo ni sahihi kutoa huduma mbovu kwa vile hawana allowances za kuridhisha?

Aisee nikukutana na watu wenye reasoning kama hii huwa naghafirika sana, yaan kabisa watu mna justify watumishi wa afya kutoa huduma mbovu kwa sababu nyepesi hivi? Daah.

Kama suala ni maslahi kwanin wasiache kazi, waje wengine watakaokuwa fully committed kwa hayo hayo maslahi?

Mbona wewe uliacha kazi ya utabibu na kufanya mambo mengine..!! Kwanin na hao kuliko kuwatetea sijui wanafanya uzembe wa makusudi sababu ya uduni wa allowance wasiache kazi tu.
 
Daah... na wengi wa watumishi wanaompenda sana Samia na kupayuka payuka ovyo sijui mitano tena ni kwa sababu kama hiyo hapo mwisho, wana uhuru wa kufanya upumbavu bila wasi wasi wowote wa kutumbuliwa.
 
Sawa nimekuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…