Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Waswahili waliposema ukivuliwa nguo chutama hawakuwa wamekosea kabisa.
Muda mchache ujao Msemaji wa Serikali anaenda kuongea na Waandishi. tena baada ya CNN kutoa habari ya kutisha kuhusu mauaji yaliyofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama wakati na baada ya Uchaguzi wa mwaka huu.
Tuhuma zilizotolewa na CNN dhidi ya Serikali ya Tanzania na vyombo vyake vya ulinzi na usalama ni tuhuma nzito sana zilizopelekea hadi viongozi mbalimbali duniani kudai kuwe na uchunguzi huru wa kimataifa pamoja na kuwajibishwa kimataifa kwa wahusika wote.
Press ya Msigwa muda mchache ujao inafuatiliwa sio tu na CNN bali Nchi zote duniani zilizoguswa na suala hili.
Ikumbukwe Press hii ya Msigwa inafanyika huku Watu wakiwa hawajaona miili ya ndugu zao iliyopelekwa mochwari wakishuhudia hadi kulazimika kufanya ibada ya kuzika nguo za ndugu zao. Hili tu linathibitisha kuwa Serikali ya Tanzania ilizika watu kwenye makaburi ya siri kujaribu kuficha ushahidi. Sasa kwenye hili Msigwa ana lipi la kuieleza dunia na ikaelewa?
Ikumbukwe pia, haya yanafanyika hadi leo hii Serikali ikiwa haijatoa idadi rasmi za watu waliokufa. Kama Serikali haina hatia kwa nini haikuwahi kutoa idadi rasmi ya watu waliokufa? Hapa Msigwa ana lipi la kuiambia Dunia na ikamwelewa zaidi ya kuzidi kujitia hatiani?
Ikumbukwe pia, Wakati wa Uchaguzi, Serikali walizima mitandao, na baada ya Mitandao kurudishwa Jeshi la Polisi lilituma sms kwa watu kuwakataza kutuma video za matukio ya Uchaguzi. Kwenye hili huu ulikuwa ni mkakati wa kutisha watu wasiseme na kusambaza ukweli kuhusu kilichotoea. Messages watu wanazo hadi leo na wameshare CNN. Kwenye hili Msigwa ana lipi la kuiambia dunia ili imuelewe?
Rai yangu kwa Samia na Serikali yako isiyo na kibali cha Wananchi.
Kwa hali ilipo sasahivi kukaa kimya ni busara kuliko kujaribu kuongea. Maji yakishamwagika hayazoleki.
Mmeshachafuka vibaya sana na kilichobaki sasahivi ni dunia kuwachukulia hatua tu. Hakuna lolote la ziada.
Chochote mnachokifanya sasahivi kisheria kinachukuliwa kama afterthought. Muulizeni huyo AG wenu wa mchongo kama anaelewa maana ya Afterthought?
Hakuna aliyewahi kumwaga damu ya watu wasio na hatia hapa duniani na akabaki salama. Ni suala la muda tu.