Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Saa nyingine hizi huwa sio fedha kama fedha
Marekani ni ngumu sana kukupatia fedha, anachofanya ni kukupa ARV au chanjo zikiwa overpriced ndo maana utaona kwamba wametoa kiasi kikubwa cha pesa ila sivyo ilivyo
Same same wanachofanyiwa Ukraine, wanapewa silaha obsolete halafu Marekani wanaweka high price ionekane ni mabilioni ya fedha
Inawezekanaje kwamba tulipewa msaada wa USD Milion 512 ndani ya mwaka mmoja kwenye sekta ya afya pekee alafu bado wagonjwa wanalala chini? Hizi hela zilienda wapi?🥺🥺😭😭Wakuu,
Wakati napita pita zangu mitandaoni nimkeutana na hili bandiko linaloonesha kiasi cha pesa ambacho Marekani iliipa Tanzania mwaka 2023 kama msaada.
Inawezekanaje kwamba tulipewa msaada wa USD Milion 512 ndani ya mwaka mmoja kwenye sekta ya afya pekee alafu bado wagonjwa wanalala chini? Hizi hela zilienda wapi?
Hii chati inaonesha kuwa kwa mwaka 2023 Tanzania ndio iliongoza kupokea fedha nyingi Afrika kutoka Marekani kwenye sekta ya Afya, hizi zilienda kwa nani?
Yaani Mkuu wa Mkoa anajitokeza hadharani kusema wanawake ambao hawana hela ya kununua gloves wakajifungulie nyumbani meanwhile kuna kiasi kingi hiki cha fedha tulipewa na Marekani?
Naomba kusaidiwa nani alikuwa ni Waziri wa Afya mwaka 2023 na kwanini bado tunalipia huduma za afya wakati tulishapokea kiasi kingi hivi cha pesa kutoka kwa wahisani.
Pesa nyingi sana hio..Kuna muda unaanza kuona anayofanya Trump ni sawa.
Hivi pesa yote hii si ingetosha kumaliza masuala ya afya
Hatutakiwi kuwapa nafasi hiyo ya kujitafakari. Wanatakiwa kuondokaCCM wajitafakari sana!
Hizo hela zitakuwa ziliishia kwenye kulipa wasanii, kufanyia service ma V8 yao na kuwalipa kina mwijaku na Machawa wengine na viongozi wa dini wachumia tumbo
Hv Kuna wakati mmemuona trump hayuko sawa, kama upo wakati huo basi jueni mna matatizo makubwa mno, haiwezekani miaka 60 ya uhuru nchi ambayo imebarikiwa kila aina ya rasirimali bado haziwezi hata kujenga matundu ya choo..achilia mbali madawati ya wanafumzi, wanachoweza ni kuhonga rasirimali Kwa wageni Kwa mikataba ya kipuuzi, pamoja na kumiminiwa misaada lkn wamekosa vipaumbele na kuendekeza anasa za watawala huku huduma za kijamii zikizorota! Hata kama ni wewe unatoka hela zako kumsaidia mtu unaedhani ni maskini lkn kumbe mtu huyo anatumia kidogo anachokipata kuhonga na kunywa pombe sijui kama utaendelea kutoa msaada.Kuna muda unaanza kuona anayofanya Trump ni sawa.
Hivi pesa yote hii si ingetosha kumaliza masuala ya afya
Mimi nimefanyakazi kwenye USAID Funded Projects pesa nyingi hubaki huko huko Marekani. Kwanza viongozi wa ngazi za juu za project lazima wawe Wamarekani na wanalimpwa mara 10 zaidi ya Mtanzania pia kuna wafanyakazi ambao wako based US lakini wanakuwa wanalipwa pesa hizo za project na pesa hizo zinalipwa kwenye account za mhusika huko huko USA, vifaa vyote vinatoka Marekani kwa bei ya juu sana. Pia mkiwa mnasafiri lazima mtumie ndege za US flag. Hivyo pesa ambazo zitakuwa zimewanufaisha watz kati ya hizo ni asilimia robo tu lakini kwenye matangazo wanatoa pesa zote wameleta TZ. Wamarekani ni matapeli sana.Kuna muda unaanza kuona anayofanya Trump ni sawa.
Hivi pesa yote hii si ingetosha kumaliza masuala ya afya
Inawezekana wakasema wametoa hicho kiasi lakini kwa masharti kwamba asilimia fulani ielekezwe kwenye kampeni fulani.
Mfano kama zile kampeni za dondosha mkono sweta.
Au asilimia fulani itafanya trainings kwa kipindi hiki mpaka hiki.
Au hii asilimia nyingine mtanunua kondomu (ambazo ndiyo unazikuta vyooni za bure)
So siyo kwamba unagewa mpunga ujipangie matumizi
masheitwani!Nchi iko mikononi mwa mafisi
Dodoma sahv wanakata mauno na wasaniiNchi iko mikononi mwa mafisi