Ukitaka kujua ufisadi wa CCM angalia kiasi hiki walichotoa USAID mwaka 2023. Kwanini bado tunalipia huduma za afya?


Unaelewa maana ya neno DISBURSEMENT au tukurudishe shule?
 
Inawezekanaje kwamba tulipewa msaada wa USD Milion 512 ndani ya mwaka mmoja kwenye sekta ya afya pekee alafu bado wagonjwa wanalala chini? Hizi hela zilienda wapi?🥺🥺😭😭
 
Chama chakavu kimezitumia hizo pesa kuwanunulia makatibu wao waenezi wa wilaya zote V8 na nyingine wametumia kununulia mabasi ya kijani, boda boda na bajaji kwa ajili ya kusomba wananchi kuwapeleka kwenye mikutano wakati wa kampeni za uchaguzi wakati huo huo wanaomba msaada kutoka Japan kwa ajili kutengenezea matundu ya vyoo mashuleni. Aibu!
 
Inawezekana wakasema wametoa hicho kiasi lakini kwa masharti kwamba asilimia fulani ielekezwe kwenye kampeni fulani.

Mfano kama zile kampeni za dondosha mkono sweta.

Au asilimia fulani itafanya trainings kwa kipindi hiki mpaka hiki.

Au hii asilimia nyingine mtanunua kondomu (ambazo ndiyo unazikuta vyooni za bure)

So siyo kwamba unagewa mpunga ujipangie matumizi
 
Kuna muda unaanza kuona anayofanya Trump ni sawa.

Hivi pesa yote hii si ingetosha kumaliza masuala ya afya
Hv Kuna wakati mmemuona trump hayuko sawa, kama upo wakati huo basi jueni mna matatizo makubwa mno, haiwezekani miaka 60 ya uhuru nchi ambayo imebarikiwa kila aina ya rasirimali bado haziwezi hata kujenga matundu ya choo..achilia mbali madawati ya wanafumzi, wanachoweza ni kuhonga rasirimali Kwa wageni Kwa mikataba ya kipuuzi, pamoja na kumiminiwa misaada lkn wamekosa vipaumbele na kuendekeza anasa za watawala huku huduma za kijamii zikizorota! Hata kama ni wewe unatoka hela zako kumsaidia mtu unaedhani ni maskini lkn kumbe mtu huyo anatumia kidogo anachokipata kuhonga na kunywa pombe sijui kama utaendelea kutoa msaada.
 
Kuna muda unaanza kuona anayofanya Trump ni sawa.

Hivi pesa yote hii si ingetosha kumaliza masuala ya afya
Mimi nimefanyakazi kwenye USAID Funded Projects pesa nyingi hubaki huko huko Marekani. Kwanza viongozi wa ngazi za juu za project lazima wawe Wamarekani na wanalimpwa mara 10 zaidi ya Mtanzania pia kuna wafanyakazi ambao wako based US lakini wanakuwa wanalipwa pesa hizo za project na pesa hizo zinalipwa kwenye account za mhusika huko huko USA, vifaa vyote vinatoka Marekani kwa bei ya juu sana. Pia mkiwa mnasafiri lazima mtumie ndege za US flag. Hivyo pesa ambazo zitakuwa zimewanufaisha watz kati ya hizo ni asilimia robo tu lakini kwenye matangazo wanatoa pesa zote wameleta TZ. Wamarekani ni matapeli sana.
 

Hata kama

Yaani Trilioni 1 zote zitumike kwenye training na kununulia condoms?

Hizo hela zote zinazobaki zinaenda wapi?
 
Kilichokereketa kuliko yote ni kuiondoa bima ya afya ya watoto ambao hawafanyi kazi wala kibarua chochote..........hii ni mbaya sana..........sasa laana ya haya yote wacha Trump asimamie ukucha .........ili fukuto lake liwatoe madarakani kwa kujisahau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…