Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Ukiangalia hizo sura, kuna hata moja ya mcha Mungu hapo? Halafu wauliza $ 512 zimekwenda wapi? Ebo! Magari ya Tamisemi hukuyaona?Kasongo mbona wewoo!!
View attachment 3226977
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukiangalia hizo sura, kuna hata moja ya mcha Mungu hapo? Halafu wauliza $ 512 zimekwenda wapi? Ebo! Magari ya Tamisemi hukuyaona?Kasongo mbona wewoo!!
View attachment 3226977
Baba tirampu mi 5 tena wacha tukose wote,CCM ni shimo la rushwa na ufisadi ni adui wa TanzaniaWakuu,
Wakati napita pita zangu mitandaoni nimkeutana na hili bandiko linaloonesha kiasi cha pesa ambacho Marekani iliipa Tanzania mwaka 2023 kama msaada.
Inawezekanaje kwamba tulipewa msaada wa USD Milion 512 ndani ya mwaka mmoja kwenye sekta ya afya pekee alafu bado wagonjwa wanalala chini? Hizi hela zilienda wapi?
Hii chati inaonesha kuwa kwa mwaka 2023 Tanzania ndio iliongoza kupokea fedha nyingi Afrika kutoka Marekani kwenye sekta ya Afya, hizi zilienda kwa nani?
Yaani Mkuu wa Mkoa anajitokeza hadharani kusema wanawake ambao hawana hela ya kununua gloves wakajifungulie nyumbani meanwhile kuna kiasi kingi hiki cha fedha tulipewa na Marekani?
Naomba kusaidiwa nani alikuwa ni Waziri wa Afya mwaka 2023 na kwanini bado tunalipia huduma za afya wakati tulishapokea kiasi kingi hivi cha pesa kutoka kwa wahisani.
Kwa uzoefu wangu mdogo sio kweli kwamba wanalazimishwa kununua vifaa toka 🇺🇸. Ila wanalipwa mishahara kwa standard ya juu, wanakuwa monitored sana sana.Na hizo NGO hulazimishwa kununua vifaa vyao vya utafiti huko Amerika kwa bei ya juu. Hela za USAID hurudi nyingi nchini kwao kihuni.
Tena watu wanazichapa pesa sio poa mkuu! Yaani kushawishi mtu mzima wa huko rorya akate govi lake watu wameandika proposal na 🇺🇸 wakatoa fedha na watu wakaenda mara kukata wazee na vijana magovi.Hii nchi bwana magovi nayenyewe yanaitaji project ? Aisee...
Ni kweli ni inte'l NGO ila nao walitegemea sana funds za usaid.JHPIEGO siyo NGO ya ndani hiyo. Ni ya Wamarekani hao hao! Asilimia kubwa ya fedha hizo huwa zinarudi Marekani kwa mlango wa nyuma!
Naunga mkono hojaCcm ni cancer kwenye hii nchi. Tuikatae.
Ndo maana musk akasema ni shirika la kiharifu!!!!Ni kweli ni inte'l NGO ila nao walitegemea sana funds za usaid.
Mimi nimefanya tenda iliyokuwa financed na USAID.. Kwenye tender document kulikuwa na majina ya maduka waliyopendekeza tununue huko. Ukileta tofauti na hiyo brand hawapokei. Mbaya zaidi kulikuwa na taasisi nyingine katikati kabla ya taasisi ya kitanzania.Kwa uzoefu wangu mdogo sio kweli kwamba wanalazimishwa kununua vifaa toka 🇺🇸. Ila wanalipwa mishahara kwa standard ya juu, wanakuwa monitored sana sana.
Afadhali,maana hospital kwenyewe watoto pesa,wajawazito pesa, hizo pesa zinawatajilisha wao wakuu tu,bado dawa zenyewe hakuna,Trump kwa hili yupo sawa tu,kama kufa tufe tu kuliko pesa zinazowanufaisha watu wachacheWakuu,
Wakati napita pita zangu mitandaoni nimkeutana na hili bandiko linaloonesha kiasi cha pesa ambacho Marekani iliipa Tanzania mwaka 2023 kama msaada.
Inawezekanaje kwamba tulipewa msaada wa USD Milion 512 ndani ya mwaka mmoja kwenye sekta ya afya pekee alafu bado wagonjwa wanalala chini? Hizi hela zilienda wapi?
Hii chati inaonesha kuwa kwa mwaka 2023 Tanzania ndio iliongoza kupokea fedha nyingi Afrika kutoka Marekani kwenye sekta ya Afya, hizi zilienda kwa nani?
Yaani Mkuu wa Mkoa anajitokeza hadharani kusema wanawake ambao hawana hela ya kununua gloves wakajifungulie nyumbani meanwhile kuna kiasi kingi hiki cha fedha tulipewa na Marekani?
Naomba kusaidiwa nani alikuwa ni Waziri wa Afya mwaka 2023 na kwanini bado tunalipia huduma za afya wakati tulishapokea kiasi kingi hivi cha pesa kutoka kwa wahisani.
Sio kweliSaa nyingine hizi huwa sio fedha kama fedha
Marekani ni ngumu sana kukupatia fedha, anachofanya ni kukupa ARV au chanjo zikiwa overpriced ndo maana utaona kwamba wametoa kiasi kikubwa cha pesa ila sivyo ilivyo
Same same wanachofanyiwa Ukraine, wanapewa silaha obsolete halafu Marekani wanaweka high price ionekane ni mabilioni ya fedha
Wanakwapua mahela wanatumbua maisha... Huoni toto la Mwigulu lilivyojazia?Interesting, very interesting. Na bado toto afya kadi nayo ikafutwa kwasababu eti mfuko umeelemewa; Tanzania, mmh!
Rudi tupambanie wote kujisaidia wenyewe kama nchiWatanzania tuko wapumbavu sana aisee.
Hii misaada na ikome mara moja.
Tutakuwa wapokea misaada mpaka lini?
Sisi hatuna akili ya kujisaidia wenyewe?
Naunga mkono misaada yote kusitishwa.
Mawachawa na waimba mapambio wakishapewa chakula wanajiona wapo mbingu ya 8!Viongozi wamezungukwa machawa kila wakati ni kuimba tu mapambio.
Yani naona kuna shida kwenye taifa. Hivi wewe kama kiongozi huwezi kung'amua kwamba hawa watu wanaonizunguka ni machawa ata ushauri wanaonipa niweke kwenye dustbin. Kama kiongozi hawezi kung'amua hilo yeye na chawa akili zao zinafanana.Mawachawa na waimba mapambio wakishapewa chakula wanajiona wapo mbingu ya 8!
Inaumiza sana. Sijui vizazi vyetu vitakuja kuishije tusipofanya mabadiliko hivi sasa.Ccm ni cancer kwenye hii nchi. Tuikatae.
100% Yupo sahihi!Kuna muda Trump anaonekana yupo sahihi.
Hata wewe umewageuka! Ama kweli siku ya mwisho kila goti litapigwaNchi iko mikononi mwa mafisi
Wewe umeandika utenzi mreefu. Mimi nimekupa hesabu hapo. Kua huo misaada tunatoa shukurani lakini Bado ni kama tone katika bahari. Kuhudumia watu milioni 60 kuwapa huduma ya wastani inahitaji pesa nyingi sana ambapo Tanzania pamoja na misaada na bajeti yake Bado haitoshi.Si ajabu ukakuta wewe ni ofisa mwandamizi ndani ya hii serikali iliyojaa wezi na matapeli.
Percival,
- Je budget ya wizara ya afya ni shilingi trillion ngapi kwa mwaka?
- Je hiyo budget inategemea tu msaada kutoka USAID peke yake?
- Je bila huo msaada wa USAID huduma za afya zingesimama nchini?
- Je misaada tunayopata kwa kutembeza bakuli kama matonya inaishia wapi?
- Je mapato yanayotokana na kodi na tozo lukuki ya kausha damu zinatumikaje?
- Je mapato tunayopata kwa kuuza mali asili zetu kama wenda wazimu zinatumikaje?
- na maswali mengineyo mengi tu.
Percival, kwa sasa nitaachia hapo ila nakukumbusha tu kuwa dola milioni mia tano inakaribia shilingi trilioni na nusu na hapo hapo madeni yetu yalizidi trilioni hamsini.
Je hii ina maana gani? Ngoja nikusaidie hii ina maana mikopo yetu peke yake ni zaidi ya mara hamsini ya huo msaada wa USAID na huo ni moja tu katika misaada lukuki tunayopata.
Percival, jitafakari.
Wewe ni mihemko tu piga hesabu acha porojo za magengeniKwa hiyo tunahitaji USD Bilioni 10 ili tuwe na huduma bora za afya?
Hapo unahudumia pamoja na mende na wanyamapori au ni binadamu peke yake?
Una elimu gani?