Ukitaka kujua ufisadi wa CCM angalia kiasi hiki walichotoa USAID mwaka 2023. Kwanini bado tunalipia huduma za afya?

Baba tirampu mi 5 tena wacha tukose wote,CCM ni shimo la rushwa na ufisadi ni adui wa Tanzania
 
Na hizo NGO hulazimishwa kununua vifaa vyao vya utafiti huko Amerika kwa bei ya juu. Hela za USAID hurudi nyingi nchini kwao kihuni.
Kwa uzoefu wangu mdogo sio kweli kwamba wanalazimishwa kununua vifaa toka 🇺🇸. Ila wanalipwa mishahara kwa standard ya juu, wanakuwa monitored sana sana.
 
Halafu kuna mafisi yanasema eti TUJITETEE kisa Trump kakata mirija
Haya majizi yafunguliwe nyuzi hata 100 kwa siku
 
Kwa uzoefu wangu mdogo sio kweli kwamba wanalazimishwa kununua vifaa toka 🇺🇸. Ila wanalipwa mishahara kwa standard ya juu, wanakuwa monitored sana sana.
Mimi nimefanya tenda iliyokuwa financed na USAID.. Kwenye tender document kulikuwa na majina ya maduka waliyopendekeza tununue huko. Ukileta tofauti na hiyo brand hawapokei. Mbaya zaidi kulikuwa na taasisi nyingine katikati kabla ya taasisi ya kitanzania.
 
Afadhali,maana hospital kwenyewe watoto pesa,wajawazito pesa, hizo pesa zinawatajilisha wao wakuu tu,bado dawa zenyewe hakuna,Trump kwa hili yupo sawa tu,kama kufa tufe tu kuliko pesa zinazowanufaisha watu wachache
 
Sio kweli
 
Watanzania tuko wapumbavu sana aisee.

Hii misaada na ikome mara moja.

Tutakuwa wapokea misaada mpaka lini?

Sisi hatuna akili ya kujisaidia wenyewe?

Naunga mkono misaada yote kusitishwa.
Rudi tupambanie wote kujisaidia wenyewe kama nchi
 
Mawachawa na waimba mapambio wakishapewa chakula wanajiona wapo mbingu ya 8!
Yani naona kuna shida kwenye taifa. Hivi wewe kama kiongozi huwezi kung'amua kwamba hawa watu wanaonizunguka ni machawa ata ushauri wanaonipa niweke kwenye dustbin. Kama kiongozi hawezi kung'amua hilo yeye na chawa akili zao zinafanana.
 
Wewe umeandika utenzi mreefu. Mimi nimekupa hesabu hapo. Kua huo misaada tunatoa shukurani lakini Bado ni kama tone katika bahari. Kuhudumia watu milioni 60 kuwapa huduma ya wastani inahitaji pesa nyingi sana ambapo Tanzania pamoja na misaada na bajeti yake Bado haitoshi.
 
Kwa hiyo tunahitaji USD Bilioni 10 ili tuwe na huduma bora za afya?

Hapo unahudumia pamoja na mende na wanyamapori au ni binadamu peke yake?

Una elimu gani?
Wewe ni mihemko tu piga hesabu acha porojo za magengeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…