East Africa watu wenye akili wapo Kenya na Uganda
Fanya research ndogo tu kwa kuingia mtaani kuwahoji watu wa kawaida utapata majibu
Kwa tz Yale makabila yenye akili sana yanapigwa vita wanaenda mbali zaidi wanasema Nyerere alikataa yasitoe mtawala
Wakati nchi zilizoendelea zonawapa utaia watu wenye brain kubwa bongo inawapa uraia wakimbizi
Kudhihirisha haya eti Kuna watu wasomi eti wanailaumu cdm kwa maandamana wengi wanajiita wanaharakati wanadai elti chama kimeparalyse
Haha, kwanza kuhusu akili hili si suala la ukabila wala ukanda akili ni Tunu ya mtu binafsi, inachangiwa na uelewa wa vitu upambanuzi na kutafakari, watanzania ni watu wenye brain nzuri mno na wapo na reasoning nzuri, haimaanishi kukaa kimya kwa watanzania ndy ujinga wao.
Najua umeangalia ujasiri wa wakenya na wauganda juu ya kuzipinga Serikali zao pale ambapo kuna kitu hakiendi sawa, watanzania wanafikra pana ndy mana hadi leo amani ipo na utulivu licha ya mambo ya kutatanisha yanayotokea kila siku, wananchi wa Tanzania wanatamani kutumia njia bora ambayo haitosababisha vifo, majeraa, njaa, wala vita kwa maslahi ya maisha ya vizazi vijavyo.
Tatizo kubwa ni namna ya kupata majibu ya maswali magumu yaliyopo kwa watanzania.
Hapa kuna umuhimu wa kushirikiana na taasisi za haki za binadamu ili kuweza kuzungumza kwa amani na kupata masuluhisho ya matatizo yetu wala sio kustrike then baadae ndiyo tutambulike kwamba tunaakili sana kwasababu tuna ujasiri wa kuichallenge serikali na kuitishia kuiondoa madarakani.
We are very intelligent people as Tanzanians.
Na tutapata njia bora kuliko mataifa mengine katika kutatua matatizo yetu naamini hivyo.
Huu ndiyo wakati wa kutumia NGOs kutoa elimu juu ya haki ya binadamu na wananchi wote kwa ujumla na kuunda mifumo mizuri ya kuhoji serikali na kutatua matatizo yetu peacefully, habari za vita na maandamano tuwaachie wengine.
Nyerere kwa kutumia maarifa alimuondoa Muingereza kwenye nchi hii, bila bunduki wala panga ni kwa maarifa tu na kutumia majukwaa husika, sasa kwanini akili zetu tuzielekezee kwenye matendo kama ya wakenya na wauganda?