Ukitaka kujua Watanzania wengi hawapendi kazi, zunguka maofisini muda wa lunch

Ila jamani wanawake asilimia kubwa ni wavivu makazini.. huo ndo ukweli.. mpaka kuna saa najiuliza kama wana add value kwenye biashara.
 
nimecheka sana mkuu ww umeajiriwa wapi???
Mkuu ,Mimi nafanya kazi kwenye kampuni moja ya maswala ya ujenzi ..so mara nyingi nazungukaga kupeleka invoices, kufuatilia P.O na kuchukua cheques Kwa makampuni tunayofanya nayo kazi so Huwa hii Hali nakutana nayo kila mara ..na Karibia kila ofisi ... ila kwavile nshazoea naenda nao hvo hvo
 
Yan mkuu kama huna moyo unaweza mpiga hata mtu ,Kuna baadhi ya watu kwenye hz ofisi wanakera mnoo
 
huu ni ukweli mtupu,vyuoni utakuta mwanafunzi anataka notes tu,enzi hizo nafundisha chuo kimoja nchini nilikataa kuwapa notes,nawapa vitabu tu vya kusoma walikua wanafeli sana hata ukitoa maswali ya mifano,nikaacha kazi ;
tubadilike;
Ungeenda na biti yao.. sasa ndo ukaacha kazi?
 
Kwa mishahara ipi? Hii inayolwisha baada ya siku 10 tu!?
Typically, tabia za kimaskini-kutopenda kazi!! Yaani hakuna namna nchi iwe na watu wasiopenda kufanya kazi halafu iwe na ustawi!
 
Watu wanatafuta mishahara walipe bills mzee [emoji28]

Kazi uipende ofisi ya babaako hiyo?
Kuna kampuni nilijitoa mpaka off zangu nikawa napiga mzigo bila malipo. Overtime no malipo. Full kuji over work.....

Malipo yake ni kuachishwa kazi. Nilicheka sana nikajiona mjinga wa mwisho.

Kampuni zetu hizi ukionekana unafanya kazi, watu wanakutengenezea picha mpaka hutaamini
 
Una point mkuu.. ila ukikosa motisha ya kazi kisa maslahi madogo, bado utakuwa unakosa professionalism.

Maana ni kama utakuwa sio productive kwenye kazi.. So mimi siku zote huwa nasema, ukikubali kufanya kazi fanya ile ile jitoe mpaka mwisho.

Ila kama unaona maslahi madogo, acha kazi kabisa na sio kufanya kwa kulega lega
 
Hao Wabunge wanaojilipa milioni 12 kwa mwezi na marupurupu manono na kiinua mgongo cha zaidi ya T shs milioni 300 kila mmoja kila baada ya miaka mitano hiyo pesa inatoka wapi!?
Na mishahara mizuri inatarajiwa kutoka wapi?
 
True.
 
Mimi nikimkuta mtoa huduma mwanamke kwanza akili tayari inaanza kuchoka.. maana lazima utakutana na excuse au huduma ya kivivu, kama sio benki basi tegemea kuambiwa njoo kesho.

Yaani mtu yupo kwenye kutoa huduma akikuona mteja umekuja anaanza kukasirika maana alikuwa anachati
 
Hao Wabunge wanaojilipa milioni 12 kwa mwezi na marupurupu manono na kiinua mgongo cha zaidi ya T shs milioni 300 kila mmoja kila baada ya miaka mitano hiyo pesa inatoka wapi!?
Hao wabunge ni asilimia ngapi ya waTz? Na watakapopunguziwa wakipatacho sasa ndio kitafanya sasa waTz tutoke uchumi wa 'kati chini kwenda kati juu'?
 
Sisi Wabantu ni wavivu na tunapenda kulalamika tu
 
Upo sahihi sana
 
Mkuu inashangaza sana Hawa dada zetu hawataki kujishughulisha kabisa. .. wao n kuchat na kusingizia system Iko low ..njoo kesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…