Ukitaka Ndoa yako iwe na Furaha; lazima uzingatie hili

Utafiti wa kisayansi unaonesha kuwa wana ndoa wanaosali pamoja Mara kwa mara, wana chance kubwa ya kudumu kwenye ndoa kuliko wale wa upande mwingine.
 
Utafiti wa kisayansi unaonesha kuwa wana ndoa wanaosali pamoja Mara kwa mara, wana chance kubwa ya kudumu kwenye ndoa kuliko wale wa upande mwingine.

Huyo hajui hata kuoa/kuolewa na mwenza unayefanana naye pia ni HEKIMA
 
bandiko jema sana. umesahau na kupishana umri pia
 
Yan huwezi amini mimi ni Mshamba wa Simu vibaya mno, aina ya simu nayotumia Sahiv hata sielewi maana nikisave link sijui PA kuipata, Nielekeze tafadhali

Hahahaaa link mara nyingi nasave kama bookmarks kwenye browser(Firefox or Chrome).
 
Ndoa inahitaji Mfanano

Unaweza ukawa masikini ukaoa masikini lakini msifanane kifikra, kimaumbile, kihisia, kimtazamo, nk.

Pia mnaweza kuwa wote matajiri na msifanane.

Wewe ndio umekurupuka umesoma bila upeo
Ufanano kama huo unaohusema haupo kwa binadamu wa kawaida....Yaani mtu mfanane kifikra, kimaumbile, kihisia, kimtazamo...hapo labda ujiumbe mwenyewe wa pili sasa......
 
Ukitaka kuwa na mke wacha moyo ukuongoze, kuna mtu unakutana nae popote unapomtazama straightforward unajisikia amani moyoni, unajihisi umefika nyumbani, unajisikia kabisa from inside huyu naweza kuwa nae muda mrefu.

Appearance yake, tabia, anavyoongea, vyote unaviona vinaendana na wewe, haya yote unayaona bila kuwepo hisia za mwili lini utalala nae, hata usipolala nae lakini kitendo cha kumpata unaridhika moyo, unajiona kuna kazi umeikamilisha.

Inshort ili muishi vizuri kwenye ndoa, tabia ya mwenzako lazima isitofautiane sana na ya kwako, utamvumilia hata akikukosea kwasababu makosa yake yatakuwa ndani ya uwezo wako, sio mageni sana au makubwa sana kwako, lakini mkitofautiana sana tabia jiandae kukutana na mitihani ambayo hukuwahi kuifikiria na usipokuwa makini unaweza ua mwenzako au kujiua kabisa.
 
Asa
Asante kwa mawazo sawasawa na yangu,ndoa haina formula mkuu imeisha hiyo...
 
Maisha ni kama movie na MUNGU ndie director. Sisi wanadamu huwa tunaamini tunajiamulia maisha yetu kwenda vile tunataka ila si kweli.

Maisha MUNGU anayaunda mwanzo hadi mwisho, kazi yetu ni kuplay role anazotupa. Ukijipangia roles zako lazima maisha yako yawe full of complications na pain.

Ni kama movie , director anapompa actor movie huwa anataka afuate script aliyo muandikia. Actor akileta ujuaji na kuigiza anavyotaka na kuwa na script yake kinyume na ile ya story ya director then hiyo movie itaharibika.

Maisha especially ya mahusiano yanataka matumizi ya hekima ya asili ingawa watu hutumia busara eneo la hekima. Ushawahi kutana na binti mzuri kwa muonekano anakazana kwenda kanisani kufuata maombi ya ulinzi wa kupata mume mwema kwaajiri yake?!

Dhamira yake ni nzuri ila mbinu zake ndizo zina walakini. Swala hapo hajatumia hekima bali katumia busara kufanya maamuzi. Hekima inakulinda katika nyakati, busara inakusaidia usipokuwa na hekima. Hekima inataka utulivu wa akili na hakuna mwanadamu atakupa hekima ila MUNGU pekee ndio atakupa hekima. Mwanadamu mwenye hekima atakupa busara ukifuata hekima yake, ila busara haidumu vizazi na vizazi sababu ni zao la hekima ya wakati au nyakati fulani.

So kwa kumalizia, mleta mada, jifunze jambo moja, hayo uliyosema ni maneno ya busara sana tena sana. Ila yamekosa uhalali wa hekima ndani yake. MUNGU hafundishwi wala kupangiwa utendaji wake. Akishakuletea mtu wewe ukaleta ufundi matokeo yake ndio yale ya kusema wanaume ni wanyama, au siku hizi hakuna wanawake wa kuoa.

By the way.... First love wako unatakiwa umjue kuanzia miaka 16 hadi 20. Hapo baada ya 20, experience za vurugu za kimahusiano zinakuondoa katika nafasi ya kuielewa asili ya mwanadamu katika mapenzi na mahusiano. Imagine leo kuna mwanamke ukimpenda na kumjali anakuona mjinga na kilaza atatafuta mwanaume wa kumpa stress kisha aje kuomba ushauri.
Pia unaweza mpenda mwanaume kuliko chochote ila akakuona mzigo na kero muda mwingine sababu ya attention unayompa. Haya yote ni matokeo ya kujihusisha na watu wengi kimahusiano katika safari ya maisha.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…