Ukitaka pesa fanya hivi kijana!

Ukitaka pesa fanya hivi kijana!

TAWIK

Member
Joined
Nov 6, 2018
Posts
60
Reaction score
87
Habari wanajamvi hili na poleni pia hongereni kwa majukumu yenu ya kila siku. Leo nimekuja kushika mkono vijana ambao kila kukicha wanahaha kuzitafuta pesa kila pande za dunia. Utakuta kijana anahangaika Mara kubeti Mara ajira Mara kuiba Mara hivi Mara vile miaka nenda rudi.

Sasa kijana naomba unielewe kama unataka pesa Fanya hivi
1)Anza kufanya kazi upate kianzio kama kuuza maji, kumpa fundi tofali, uza Karanga au matunda na pesa za mwanzo utakazopata anza kununua zana ndogondogo zinazotumiwa na jamii yako mfano mbao za lenta, matololi, spans, madeli, nk. Jinsi utakavyoviongeza ndivyo simu yako itakuwa bize kupigiwa yani Mara ngazi, toroli, tester, Mara hiki Mara kile.

2)Ukiona tenda uchwara zimekuzidi uza baadhi uongezee kwenye akiba uliyopata na nunua machine complicated kama welding, freezer, pikipiki, mitungi ya gesi machine za kudalizi, mipira ya kukodi nk. Endelea hivyohivyo mpaka kuna siku utajikuta unanunua fuso.

Pesa imejificha kwenye huduma za binadamu kuanzia unyayoni mpaka utosini na sio kubeti, kuokota, urembo nk. So Mara moja kijana kuhama toka jamii moja kwenda nyingine akitafuta unafuu wa maisha ilihali popote mfumo ni uleule. Nikuibie siri hii Hakuna kitu hakipendi Tajiri kama pesa. Yeye akipata pesa haraka sana anafanyia jambo anapeenda vifaa vinanampa vifaa Ila hapendi pesa.

Sasa ukitaka kuwa tajiri waza hivi,
'NITAPATAJE GHOLOFA?' na sio
'NITAPATAJE MILIONI MIA!
Ujue kutofautisha kati ya vitega uchumi na vistarehe.
Vitega uchumi# in vitu vyote vinavyokuwekea pesa mfukoni
Vistarehe # nivitu vyote vinavyokuchomolea pesa mfukoni

NIMENAWA NISILAUMIWE!
 
Nilidhani kichwani unazo hadi niliposoma gholofa badala ya ghorofa!
Maono yatotewayo kwa mipango ya Mungu wasiohusika hatakama wakiyaona hawaoni kitu huangalia maandishi n.k.... Hongera kwa kwakunirekebisha!
 
Nadharia ni Rahisi sana mkuu...kila mtu anaweza kusema...

Tunaomba ujitumie wewe kama mfano wa kufundishia, ili somo lieleweke zaidi...

Karibu, tunakusikiliza...
 
"Ceteris paribus"

Usiumwe, usiuguze, usipate janga hapo kati.

Watu wanafeli sio kua wanafanya sana starehe, ila ndo ivo majanga ndgu.
 
"Ceteris paribus"

Usiumwe, usiuguze, usipate janga hapo kati.

Watu wanafeli sio kua wanafanya sana starehe, ila ndo ivo majanga ndgu.
Kwanza nikukumbushe hakuna kiwango cha Mali ambacho mtu kinaweza kumkidhi akipatwa na mapito! Kuhusu yadunia hayo tuyaweke kando hapa tunashauliana kwenye hali ya kawaida! Yani tofauti yamawazo ya matajiri na masikini.
 
Nadharia ni Rahisi sana mkuu...kila mtu anaweza kusema...

Tunaomba ujitumie wewe kama mfano wa kufundishia, ili somo lieleweke zaidi...

Karibu, tunakusikiliza...
Kabla hatujabumba kitu Nadhalia kwanza hufikiliwa kisha tunaingia maabara kutoka na kitu... Sasa hapa vijana tunawapa nadhalia ili wasipoteze muda mwingi kutafuta njia na wakati mwingine hata njia isipatikane uzee ukamkuta
Mimi siwezi kujisemea ntaonekana najigamba kwa ukwasi nilionao na niseme tu ukwasi sina kivilee ila kwamajaribio ya sampuli zamwanzo majibu yake yanashangaza! Yani nirahisi mno!
 
Back
Top Bottom