Ukitoka kidogo nje ya nchi na ukarudi kwenye viwanja vyetu vya ndege utatamani kulia machozi

Mtoa mada.. nakushaur ufatilie statistics za Watalii je wanakuja wangapi nchini? Kisha ndio ujue kuna wingi wa ndege au uchache?....

Nchi yetu asilimia 70 wasafiri ni watalii.

Nakupa hiyo homework.
Duuh mtihani
Kwa hiyo ndege ni kwa ajili ya watalii tu.
 
Mara ukija Tanzania Yale mabati ya Buza Buguruni na vingunguti yanatia aibu!
Mara oooh uwanja hauko busy...
Matajiri mna nongwa sana....
Anyway ngoja nikapande Saratonga mimi ni enjoy nature
 
Nakumbuka miaka ile ya 90 nilikuwa naenda airport dar kuangalia midege ya KLM, BA,SWISS Air, SABENA nk. Sijui kama yote yanakuja
Inawezekana tulikuwa tunakutana, muaka hiyo nakaa majumba sita nikichoka zangu napanda kule juu. Nasikia baada ya matukio ya ugaidi hizo mambo zilizuiliwa.
 
Mashirika ya ndege yaje Tanzania, kufuata nini? Halafu kwa umaskini huu wa watanzania hizo ndege atapanda nani?

Angalia mtaani kwako tu. Kuna kijiwe cha bodaboda hapo jirani? Basi kama kipo, hiyo ndiyo hali ya maisha ya wabongo.
Ni ulimbikaji wa kodi na ubepari tu, mbona fastjet alikuwa na nauli ambazo haziumizi? TZ ukipanda ndege ni kama anasa lkn ndio usafiri unaotakiwa kukuza uchumi wa nchi kwa kuwa ni wa haraka.
 
Kuna hivi visiwa mashariki ya msumbiji kila baada ya dk 10 kuna ndege inatua au kuondoka, sijui kuna biashara gani huko ambayo wametuzidi.

 
Huduma ya ndege ni biashara,wenye ndege nao wanaangalia faida,huwezi kuileta ndege tu Tanzania wakati hakuna abiria wa kutosha,ukuaji wa uchumi wenu ndio utaka determine idadi ya ndege zitakazotua nchini kwenu,na kwa hali hii ya kila mtu kupiga kadri awezavyo kwa Tanzania itakuwa ni muujiza...
 
Free wifi ipo JNIA. Unafeli wapi?
 
Ndege haziji Kwa Ajili ya kuonekana Bali demand ikiwepo ndio zitakuja.

Zaidi ya raia mili.40 ni maskini wa kutupwa ,unatagemea watapanda ndege?

Naona umetoka Nje Kwa mara ya kwanza
 
Mwaka huu free wifi Wataweka na maeneo mengine mfano stendi za Mabasi.
 
Kuajiri watu competent ni suala ambalo wameshindwa kbs is why hizo sehem zinayumba. People dont think outside the box, no creativity at all
 
Angalia sasa mapaa ya nyumba ukiwa angani..!! Hatari. Mapaa ya nje yamekaa mstari ulionyooka na hayana kutu. Huku kwetu utadhani upo juu ya jalala..!!
 
Mfumo wetu wa ajira ni tatizo Sana. Niliwahi Kuwa afisa HR taasisi fulani. Simu za mpitishe mwanangu, ndugu yangu, shemeji yako zilikuwa nyingi Sana. Kwa mfumo huu utapataje watu wazuri?. Nadhani hata kwengine mambo ni haya hata. Matokeo ya ajira za hivi ni wizi, fitina, uzembe, mapuuza, majungu nk.
Naamini Tanzania watu wenye uwezo wa kuendesha mambo Kwa ufanisi wapo wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…