Ukitolewa CAF Champions league hakuna kuingia shirikisho, Dezo yafutwa

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
CAF katika kikao walichokaa jana mjini Rabat, Morocco wameamua kuanzia msimu huu wa 2023/2024 na kuendelea zile timu 16 ambazo huwa zimetolewa katika hatua ya timu 32 katika ligi ya mabingwa wa Africa hazitapata fursa tena ya kuingia katika hatua ya mtoano (Play-Off) ya kupambana na 16 bora za shirikisho.

Hivyo 16 bora za shirikisho zitaingia moja kwa moja kwenye makundi.
Naiona AZAM FC ikinufaika na uamuzi huu, ina nafasi kubwa ya kuingia makundi shirikisho, hata Singida Foundation Gate.

 
Hivi CAF na UEFA nani anajuwa mpira?
 
Hii inawahusu Simba
 
Young Africans walijua hili ndio maana wanafanya mambo yao professionally. Tuko paleeeee[emoji16]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…