Ukituma sms yeye neno "SEX" kwa mtandao wa TIGO ujumbe haziendi/kumfikia mlengwa nani kuruhusu hili?

Tigo kuna maneno wameya-censor hilo linajulikana. Kuna muda nilikuwa najua kabisa list ya maneno ambayo siwezi yatuma kwa SMS ya Tigo. Na niliwahi kuwapigia simu kuwaeleza ila wanakula kona. Mwishowe hasa gf wangu namtumia text WhatsApp angalau iko end to end encrypted.
 

End to end encryption ni uongo mtu
 
Kwani end to end encryption ndo nini mkuu
Nikituma ujumbe ukawa end to end encrypted unakuwa hauji waziwazi. Nakuandikia "nitumie laki moja" ila ujumbe unakuwa coded kwenye keys unakuja unasoma labda "£@5ghdlh ...gjtl".

Ukipokea ujumbe huo unakuwa na encryption keys zinafungua ujumbe na kwako unasomeka "nitumie laki moja" ila kama kuna mtu katikati labda mtandao au spy kwa bahati mbaya amenasa mawasiliano atasoma zile codes haelewi.

Kuvunja security hiyo ni kazi ngumu, kampuni moja ya Israel inaitwa NSO Group ilitengeneza spyware ilitwa Pegasus ya kupenya mifumo ya ulinzi ya WhatsApp na kujua taarifa za mtumiaji.

Hata hivyo hakuna muuza mitumba angefuatiliwa na spyware hiyo. Gharama za kununua mfumo ilikuwa ni zaidi ya bilioni 1.5 TZS, gharama za kufunga kwa simu 10 tu ilikuwa ni zaidi ya bilioni 1.1 na kuna gharama za uendeshaji kwa mwaka ni kwenye milioni 100+.

Na si kila nchi ingeuziwa, mfano bongo tusingeuziwa sisi hatuna siri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…