Ukituma sms yeye neno "SEX" kwa mtandao wa TIGO ujumbe haziendi/kumfikia mlengwa nani kuruhusu hili?

Ukituma sms yeye neno "SEX" kwa mtandao wa TIGO ujumbe haziendi/kumfikia mlengwa nani kuruhusu hili?

Pegasus mbona mwendazake aliinunua inavyoaminika!!??
Nikituma ujumbe ukawa end to end encrypted unakuwa hauji waziwazi. Nakuandikia "nitumie laki moja" ila ujumbe unakuwa coded kwenye keys unakuja unasoma labda "£@5ghdlh ...gjtl".

Ukipokea ujumbe huo unakuwa na encryption keys zinafungua ujumbe na kwako unasomeka "nitumie laki moja" ila kama kuna mtu katikati labda mtandao au spy kwa bahati mbaya amenasa mawasiliano atasoma zile codes haelewi.

Kuvunja security hiyo ni kazi ngumu, kampuni moja ya Israel inaitwa NSO Group ilitengeneza spyware ilitwa Pegasus ya kupenya mifumo ya ulinzi ya WhatsApp na kujua taarifa za mtumiaji.

Hata hivyo hakuna muuza mitumba angefuatiliwa na spyware hiyo. Gharama za kununua mfumo ilikuwa ni zaidi ya bilioni 1.5 TZS, gharama za kufunga kwa simu 10 tu ilikuwa ni zaidi ya bilioni 1.1 na kuna gharama za uendeshaji kwa mwaka ni kwenye milioni 100+.

Na si kila nchi ingeuziwa, mfano bongo tusingeuziwa sisi hatuna siri.
 
Hizo gharama kwa serikali ingemudu sema kwenye matumizi yake ingekuwa utata
 
Neno tigo👈
Kwampalange👈
Haifai👈kuona kama nineno la maana katika
mazungumzo😂
 
Hizo gharama kwa serikali ingemudu sema kwenye matumizi yake ingekuwa utata
Nani angeiuzia serikali ya Tanzania hii ambayo kila inachofanya kinajulikana kabla. Na hakuna serikali duniani ingeshindwa kumudu, sasa ndio kusema ingemfuatilia hata muuza maembe, kachori, mlima mapapai kisa tu inamudu. Waliokuwa wanafuatiliwa kwa nchi unakuta hawafiki 10 walewale kwenye package ya kwanza.
 
Pegasus mbona mwendazake aliinunua inavyoaminika!!??
Hatununua kabisa, niamini 100%. Kwa Afrika aliyenunua wa uhakika ni Rwanda. Si kila nchi ilikuwa na sifa ya kuuziwa, wenye midomo na wakurupukaji ambao hawana hata ujasusi wa maana hawakuwa wanauziwa.

Kwa sheria za Israel bidhaa zote za kijeshi/usalama zinazouzwa deal linapitishwa kwanza na serikali. Ndio maana kwenye wanunuzi hakuna nchi ya Ulaya, ni kina Saudia, UAE, Rwanda, India, etc. Sio nchi Rais anabadilisha mkuu wa Usalama wiki ijayo, tiyari mfyatua tofali leo anajua.
 
Back
Top Bottom