Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Ukitumia internet vizuri kufanya utafiti wako binafsi utagundua Uchawi haupo. Hakuna mganga wala nabii atakayekutapeli. Wajinga ndio waliwao

Nakwenda na hiyo statement yako ya mwisho si kwa sababu nimeshindwa kujibu maswali yako, bali kwa sababu nataka kuonesha logical fallacy ya non sequitur.

Tuseme sina uwezo wa kujibu maswali yako yote ya kuungaunga hayo.

Wewe bado hujathibitisha uchawi upo.

Niloge nishindwe kukujibu hapa JF tu tujue uchawi upo.

Nimekupa mtihani mdogo tu ku prove uchawi upo.
nikikupa conditions ili ombi lako lifanyike utaweza ?
 
nikikupa conditions ili ombi lako lifanyike utaweza ?
Ukishaanza kunipa conditions maana yake uchawi wako umeshindwa kufanya kazi.

Chukua maandishi yangu uniloge, ukianza kunipa condition ndiyo mwanzo wa kuniuliza jina langu na kunitumia majambazi waniue, huo si uchawi.
 
Umejionea nini?

Kujionea kwa macho yako si uthibitisho kwamba kitu kipo.

Unaweza kuona chemchemi ya maji jangwani, kwa mirage, wakati haipo.

Lakini pia, ukisema tu "nimeona kwa macho yangu" hilo hallithibitishi hata kama umeona kwa macho yako.

Thibitisha uchawi upo. Inaonekana hata huelewi uthibitisho ni nini.
tunarudi kule kule nmekuuliza unaelewa nini kuhusu binadamu namna anavyojifunza na jinsi anavyo correct old belief hujajibu unaleta story za mirrage jangwani nkikuuliza tena utakuja na habari za illusion, hallucination au mazigazi
 
Hujathibitisha uchawi upo.

Unaleta habari za kuona mara kumi, huko kuona kwenyewe, kicha ya kwamba kuona si uthibitisho, hata kuona kwenyewe hujatuthibitishia umeona.
 
Ukishaanza kunipa conditions maana yake uchawi wako umeshindwa kufanya kazi.

Chukua maandishi yangu uniloge, ukianza kunipa condition ndiyo mwanzo wa kuniuliza jina langu na kunitumia majambazi waniue, huo si uchawi.
basi endelea kudebate na wengine ungekua unajiamini ungekubali
 
Kama wewe ni passionate learner tutaanza safari na utajifunza mwenyewe hadi utapata kuelewa uchawi upo na tena kuna parallel unseen world. Ila uwe open minded na unyenyekevu wa kutaka kujifunza.
I’m open minded and that’s why I’m asking for proof.

Just show me that sorcery and black magic are real.

Why is it so hard to prove it?
 
Visingizio vipi nimeweka hapo?
Vyote ulivyoandika kwenye bandiko nililokunukuu ni visingizio tu.

Mimi nimeshajitolea mniroge ili mthibitishe kuwa uchawi upo.

Mnaleta visingizio. Mara sijui inategemea na mazingira. Mara sijui inategemea na ukoo. Mara sijui huwezi kurogwa bila sababu!

Hivyo visingizio ni ushahidi kwamba uchawi haupo.

Ingekuwa kweli uchawi upo na mna uwezo wa kuthibitisha, mngekuwa mshathibitisha siku nyingi sana na huu ubishi leo hii wala usingejuwepo.
 
Ni kweli mkuu.

Hakuna uongo rahisi kumdanganya mtu kama uongo ambao yeye anataka kuusikia.

Kwa hivyo hao waganga wanatumia saikolojia ndogo tu kujua udhaifu wa mtu na kumdanganya humo humo.

Kuna watu wawili walikutwa wanacheza uchi pembeni ya gari Mombasa Kenya.

Watu wakajaa kuwatazama.

Habari ilikuwa ni kwamba wale watu wawili waliokuwa wanacheza uchi, walikuwa ni wezi walioiba gari yenye "alarm" ya kichawi, imewanasa.

Sasa hapo kwa watu wanaoamini uchawi, hicho kitendo kilikuwa ni uthibitisho kwamba uchawi upo.

Lakini polisi wa Mombasa walifanya uchunguzi wakagundua kuwa, ule wote ulikuwa ni mpango wa mganga mmoja wa kienyeji kujutangaza. Wale watu waliokuwa wanacheza uchi walikuwa wamelipwa ili kumtangaza huyo mganga, watu waone mganga fulani ana dawa kali ya kulinda gari.

Sasa hapo kwa mtu ambaye anaamini uchawi huo ni uthibitisho tayari atasema "nimeona kwa macho yangu watu wanacheza uchi", kama alivyosema OMOYOGWANE kumbe ni utapeli wa watu tu.

Story ya hao matapeli wa Mombasa ipo hapa.

Daah hatari sana ,watu wanadanganywa sana na waganga feki ,bado kuna hawa manabii feki nao wanawapiga pesa sana wakina mama!! Inabidi serikali iingilie kati kuwasanua misukule iliyonaswa.

Kuna Tapeli Mwingine ana kanisa Buza Kwa Lulenge aisee jamaa anawadanganya watu sana ,yaani mtu yeyote atakayepiga simu lazima apone hata akiwa na ugonjwa ambao hauna tiba ,cha kushangaza hiyo namba muda wote inatumika hata kama hakuna mtu aliyepiga simu ,jamaa anachofanya anaingia studio anatengeza conversation za mtu anayepiga simu kumbe tayari kashapewa script then wanahadaa wasikilizaji,wanarusha vipindi recorded.
 
Habari wadau

Binafsi nashangaa sana watu hasa wasomi wenye smartphone wanaoamini story za ushirikina zama hizi

Ukweli ni kwamba ukijipa muda wako kujifunza zaidi kuhusu Anthropology, elimu ya Human psychology na Science of Emotion ilivyo. watajua ukweli mwingi sana wa ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na unavyodanganyika

Watu wakijipa muda zaidi na kusoma kuhusu history za uchawi hasa msako wa wachawi (Witch Hunts in the Western World) kwenye karne zilizopita ulikuaje na kwa nini kilisababisha msako huo usitishwe. pia wakasoma kuhusu msako wa wachawi uliotokea marekani pia maarufu kama The Salem Witch Hunt na ilikuaje marekani wakaachana na misako hiyo pia, watajua ukweli kuhusu uchawi.

Kisha wakarudi kwenye youtube na kuangalia video za magic tricks zinavyofanya kazi. watajua waganga na wanaojifanya wachawi wanatumia mbinu gani kuhadaa watu.

Mfano kuna video nyingi za youtube za Sheikh Othman michael akishirikiana na Shehe Jafar kitwana ( mganga mstaafu) wakieleza kila kitu kuhusu uchawi na huku wakionesha na mifano ya jinsi waganga wa kienyeji na wachawi wanavyotapeli watu kwa kutumia Placebo effects na magic tricks. yaani ukizijua hizo hakuna mganga ataeweza kukudanganya hasa ukielewa mbinu zao na mazingaombwe yao.

Nashangaa sana kijana wa zama hizi kuamini ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati elimu zinapatikana kwa urahisi sana.

Jamani kwenye internet tusiangalie tu kina mwijaku na diamond. tumieni internet kupata elimu na kuelewa jinsi ya kusolve changamoto zetu.

Jidanganye tu.. ni akili yako,uko free kuitumia
 
Mkuu soma biblia toka mwanzo hadi ufunuo kwa makin
then ukimaliza urudie kama mara mbili then uje usome huu uzi uloandika

Uchawi umetajwa sana huko na mambo ambayo walifanya.
Mapepo ya utambuzi n.K
Kwani biblia ni ukweli!?
 
INategemea unavyoichukulia wewe
Kitu kama ni cha ukweli hata kama nikikichukulia kuwa uongo, haikibadilishi wala kukifanya kuwa cha uongo.

Kitu kama ni cha uongo hata kama nikikichukulia kuwa ni ukweli,
Haibadilishi wala kukifanya kitu hiko kuwa cha kweli kwasababu ya mtazamo wangu binafsi

Unaelewa hilo!?

Mwenye mdahalo hapo ni wewe

Mwenye hoja za biblia kama kigezo na ushahidi katika kweli ni wewe,

Wewe unaichukuliaje biblia ni ukweli ama uongo hadi Umeleta utetezi wa habari za uchawi kuandikwa humo ?
 
Na H
Habari wadau

Binafsi nashangaa sana watu hasa wasomi wenye smartphone wanaoamini story za ushirikina zama hizi

Ukweli ni kwamba ukijipa muda wako kujifunza zaidi kuhusu Anthropology, elimu ya Human psychology na Science of Emotion ilivyo. watajua ukweli mwingi sana wa ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na unavyodanganyika

Watu wakijipa muda zaidi na kusoma kuhusu history za uchawi hasa msako wa wachawi (Witch Hunts in the Western World) kwenye karne zilizopita ulikuaje na kwa nini kilisababisha msako huo usitishwe. pia wakasoma kuhusu msako wa wachawi uliotokea marekani pia maarufu kama The Salem Witch Hunt na ilikuaje marekani wakaachana na misako hiyo pia, watajua ukweli kuhusu uchawi.

Kisha wakarudi kwenye youtube na kuangalia video za magic tricks zinavyofanya kazi. watajua waganga na wanaojifanya wachawi wanatumia mbinu gani kuhadaa watu.

Mfano kuna video nyingi za youtube za Sheikh Othman michael akishirikiana na Shehe Jafar kitwana ( mganga mstaafu) wakieleza kila kitu kuhusu uchawi na huku wakionesha na mifano ya jinsi waganga wa kienyeji na wachawi wanavyotapeli watu kwa kutumia Placebo effects na magic tricks. yaani ukizijua hizo hakuna mganga ataeweza kukudanganya hasa ukielewa mbinu zao na mazingaombwe yao.

Nashangaa sana kijana wa zama hizi kuamini ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati elimu zinapatikana kwa urahisi sana.

Jamani kwenye internet tusiangalie tu kina mwijaku na diamond. tumieni internet kupata elimu na kuelewa jinsi ya kusolve changamoto zetu.

Na
Hakuna Mungu wala shetani
 
I’m open minded and that’s why I’m asking for proof.

Just show me that sorcery and black magic are real.

Why is it so hard to prove it?
Haya mambo approach yake sio kama ile ya mathematics, prove the Pythagoras Theorem on a piece of paper. Ni mambo ya kiroho na yapo subtle sana ndio maana wengi wanashindwa kuyaelewa au hata kuyafuatilia. Ni safari inataka utayari wa kujifunza kama upo tayari nitakutumia clips za watu wenye first hand experience kwenye hayo mambo halafu you can move on from there but you have to be true to yourself and let truth find its way in you. Ukiwa hivyo utajifunza a whole new world which is unknown to common person.
 
Kama kuna parallel unseen world wewe umejuaje ipo?
Kuna mambo mengi ambayo ni unseen lakini wanadamu wanajua kuwa yapo na wanayatumia. Haya mambo yana exist intellectually tu. Hujawahi kuona mawimbi ya simu lakini unayatumia kila siku. In fact mambo mengi ni yale yasiyoonekana.
 
kuhusu kupata pesa ama utajiri waganga wanacheza pia na human psychology ya kukupa masharti ambayo yatakufanya uwe mbahili na unatunza sana pesa na kuwekeza.
Hapa umepuyanga, waganga hawanaga elimu ya uwekezaji, wao ni makafara tu, na sina uhakika kama kunamtu amefankiwa kupata pesa au utajiri kwa ushauri wa mganga.
 
Gunduzi za kisayansi ndio sababu. magonjwa ambayo waliokuwa wanaamini yanasababishwa na uchawi, waligundua sababu zake kumbe ni za kisayansi.

Kadiri viwango vya elimu na kusoma na kuandika vilipoongezeka, watu walizidi kukosoa hali ya kuwinda wachawi na kuanza kutilia shaka uhalali wake. Elimu ndio ilileta mabadiliko katika mitazamo ya kiakili na kitamaduni. Rationalism zilianza kuchukua nafasi ya ushirikina na hofu, na kusababisha kupungua kwa imani katika uchawi na nguvu zisizo za kawaida.

Zaidi ya hayo, mifumo ya kisheria na mahakama katika Ulaya ilifanyiwa mageuzi ambayo yalifanya iwe vigumu zaidi kuwashtaki na kuwanyonga watu kwa madai ya uchawi. maana sheria mpya zilitaka hukumu ziendeshwe kwa kufata ushahidi unaonekana kwa macho, na sio kwa imani tena

serikali za ulaya ziliamua kuachana na sheria za Kanisa ( church laws) katika kuendesha nchi zao, sababu kanisa ndio lilikuwa na mchango mkubwa katika kuamini kuendeleza na kuendeleza uwindaji wa wachawi. maana biblia ilisema wachawi wauwawe, kumbuka zamani nchi za ulaya zilikuwa zinaendeshwa kwa kufata biblia na sheria za kanisa zinasemaje kama vile saudi arabia leo wanavyofata quran inasemaje katika kuendesha nchi yao.

Zaidi ya hayo, mabadiliko ya kiuchumi na kijamii, kama vile mabadiliko kutoka kwa ukabaila hadi ubepari, yalisababisha kuporomoka kwa miundo ya jadi ya jumuiya ambayo iliunga mkono mawazo ya kuwinda wachawi. Kadiri viwango vya elimu na kusoma na kuandika vilipoongezeka, watu walizidi kukosoa hali ya kuwinda wachawi na kuanza kutilia shaka uhalali wake.

Kwa ujumla, mchanganyiko wa mabadiliko ya kisayansi, kiakili, kisheria, kidini na kijamii ulichangia kuachana na uwindaji wa wachawi huko Ulaya na America
Habari wadau

Binafsi nashangaa sana watu hasa wasomi wenye smartphone wanaoamini story za ushirikina zama hizi

Ukweli ni kwamba ukijipa muda wako kujifunza zaidi kuhusu Anthropology, elimu ya Human psychology na Science of Emotion ilivyo. watajua ukweli mwingi sana wa ubongo wa binadamu unavyofanya kazi na unavyodanganyika

Watu wakijipa muda zaidi na kusoma kuhusu history za uchawi hasa msako wa wachawi (Witch Hunts in the Western World) kwenye karne zilizopita ulikuaje na kwa nini kilisababisha msako huo usitishwe. pia wakasoma kuhusu msako wa wachawi uliotokea marekani pia maarufu kama The Salem Witch Hunt na ilikuaje marekani wakaachana na misako hiyo pia, watajua ukweli kuhusu uchawi.

Kisha wakarudi kwenye youtube na kuangalia video za magic tricks zinavyofanya kazi. watajua waganga na wanaojifanya wachawi wanatumia mbinu gani kuhadaa watu.

Mfano kuna video nyingi za youtube za Sheikh Othman michael akishirikiana na Shehe Jafar kitwana ( mganga mstaafu) wakieleza kila kitu kuhusu uchawi na huku wakionesha na mifano ya jinsi waganga wa kienyeji na wachawi wanavyotapeli watu kwa kutumia Placebo effects na magic tricks. yaani ukizijua hizo hakuna mganga ataeweza kukudanganya hasa ukielewa mbinu zao na mazingaombwe yao.

Nashangaa sana kijana wa zama hizi kuamini ushirikina na kwenda kwa waganga wa kienyeji wakati elimu zinapatikana kwa urahisi sana.

Jamani kwenye internet tusiangalie tu kina mwijaku na diamond. tumieni internet kupata elimu na kuelewa jinsi ya kusolve changamoto zetu.

Mm nimesoma anthropology mkuu UDSM- pale. Uchawi upo! Na tumepata dodoso. Uchawi upo wa aina mbili ambao unahusisha object zilizokosa nasaba zako. Na Kuna ule unaohitaji object zenye vinasaba vyako kama nywele, nyuzi kutoka kwenye nguo uliyovaa, kucha nk.

Kuna lekcha wa UDSM-ana PhD ya anthropology ashapaa na ungo na mpaka Leo ukienda pale coss utapnywesha. Anachechemea, mana huyo ndie alitibu tatizo la wazee wenye macho mekundu shinyanga kuuliwa. Anthropology unatumia ethnographic study... Lazima na wewe ushiriki/upishi na jamii unayoifanyia tafiti ili upate uhalisia wa ndani (Emic). Mana uhalisia upo wa aina mbili
 
Screenshot_20240405-093725_Firefox.jpg

Kijana acha mbwembwe.. mtu anayejua kitu huwa anakieleza kwa urahisi kila mtu anamuelewa.

Maelezo yako tu yanaonesha ni wale wanaokariri ili wafaulu mitihani. Ila hawaelewi wanachokariri.

Nakuwekea link usome

Back
Top Bottom