Ni kweli mkuu.
Hakuna uongo rahisi kumdanganya mtu kama uongo ambao yeye anataka kuusikia.
Kwa hivyo hao waganga wanatumia saikolojia ndogo tu kujua udhaifu wa mtu na kumdanganya humo humo.
Kuna watu wawili walikutwa wanacheza uchi pembeni ya gari Mombasa Kenya.
Watu wakajaa kuwatazama.
Habari ilikuwa ni kwamba wale watu wawili waliokuwa wanacheza uchi, walikuwa ni wezi walioiba gari yenye "alarm" ya kichawi, imewanasa.
Sasa hapo kwa watu wanaoamini uchawi, hicho kitendo kilikuwa ni uthibitisho kwamba uchawi upo.
Lakini polisi wa Mombasa walifanya uchunguzi wakagundua kuwa, ule wote ulikuwa ni mpango wa mganga mmoja wa kienyeji kujutangaza. Wale watu waliokuwa wanacheza uchi walikuwa wamelipwa ili kumtangaza huyo mganga, watu waone mganga fulani ana dawa kali ya kulinda gari.
Sasa hapo kwa mtu ambaye anaamini uchawi huo ni uthibitisho tayari atasema "nimeona kwa macho yangu watu wanacheza uchi", kama alivyosema
OMOYOGWANE kumbe ni utapeli wa watu tu.
Story ya hao matapeli wa Mombasa ipo hapa.
By close of business Wednesday, every Kenyan had heard, seen pictures or watched that video of 2 naked men in Mombasa. As the story went, the two men had stolen a car – a Nissan Fuga
diasporamessenger.com