Kuna mambo mengi ambayo ni unseen lakini wanadamu wanajua kuwa yapo na wanayatumia. Haya mambo yana exist intellectually tu. Hujawahi kuona mawimbi ya simu lakini unayatumia kila siku. In fact mambo mengi ni yale yasiyoonekana.
Sijakataa. Nimeuliza amejuaje ili tuhakiki huo ujuzi.
Kwa sababu hata mimi naweza kusema mimi ndiye Mungu na hilo ni jambo lisilojulikana tu, utakubali?
Hayo mawimbi ya simu yanapimwa, yanapimika, yanafuata kanuni za hesabu na fizikia zenye logical consistency, yanapitisha mawasiliano ya simu, tunaweza kuhakiki kwamba yapo.
Kuna sehemu ya ulimwengu ambayo mwanga wake haujatufikia, the unobservable universe, tunaweza kupiga mahesabu tukaelewa kwa nini ulimwengu huu hauonekani, kwa kutumia the speed of light, distance, mathematics etc.
Sasa naelewa kuwa kuna vitu vipo na havionekani, hili sijalibishia. Hilo si tatizo kwangu. I only need to know the electromagnetic spectrum and the limit of visible kight to know that. That is not tje issue.
Lakini pia, kuna vitu havionekani kwa sababu havipo.
Sasa, mtu anaposema hiki kipo lakini hakionekani, tutajuaje kuwa hiki kipo lakini hakionekani kweli na si kwamba hakionekani kwa sababu hakipo?
Ndipo hapo nilipotaka maelezo ili kufanya uhakiki.
Na hamjanipa maelezo hayo bado.
Nikisema vibwengo wapo lakini hawaonekani tu, ni tofauti na kusema radio waves zipo lakini hazionekani tu.
Vibwengo hawapimiki, hawaonekani, hawathibitishiki kuwapo.
Radio waves tunazipima, tunajua mahesabu yake, tunajua wavelengths zake, wengine watasema zinaonekana kwa kutumia kifaa cha radio.
Sasa huo ulimwengu usioonekana mnaousema ni upi? Mnajuaje kwamba upo kweli na si hadithi za vibwengo zisizothibitishika tu?