Ukiwa Dar es Salaam unaweza kudhani maisha umeyapatia, kumbe umechelewa sana bila kujua

Kwamba unamsema chingaboy aka harmonize ?
 
Basi tatizo hapo ni la hao wanaotoka mikoani kuja dar, ila born here here hawana shida ndio kwanza wanakimbilia mikoani kutafuta fursa.
 
Unakuta kajitu kamejibanza kwenye kibanda chenye joto kali na mbu kwa Rulenge au buza ndani ndani huko ila anamdharau mtu mwenye maisha yake huko Busokelo. Tabia mbaya
 
Kwanini hili linakushughulisha mpaka umelianzishia thread?

Kama mtu kaamua kuishi Dar anaona hapo ndipo kuna maisha mazuri huo si uhuru wake tu na anaishi anavyotaka, tatizo liko wapi?
Anawakumbusha watu mikoani kuna fursa pia.
 
Anawakumbusha watu mikoani kuna fursa pia.
Watanzania wengi ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kwa watu wasiowajua, kuhusu mambo wasiyoyaelewa.
 
Acha makasiriko....hamia Dar na wewe
 
Dar watu wengi wanapoteza tu muda ila hawajijui wakishtuka umri umeenda mm. Nilishtuka mapema sasa hv huwa naenda dar kula bata
 
Huko mkoani watu wanatusua maisha sana sana aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…