Ukiwa Dar es Salaam unaweza kudhani maisha umeyapatia, kumbe umechelewa sana bila kujua

Ukiwa Dar es Salaam unaweza kudhani maisha umeyapatia, kumbe umechelewa sana bila kujua

Yaani Haya Maisha Bwna.

Yanaweza kuwa yamekupiga Chenga ila bado ukawa unaamini umeyapata.

Hasa hasa kama una ishi Dar kuna kaimani kanakujia kichwani kwamba huko Mbeya hakuna kitu, kuna kasumba inakupumbaza kichwani kwamba huko Mtwara kumejaa maskini tu na hakuna hela. Yaani Kichwa kinajaa na kuvimba kabisa kwamba wanaoishi Singida au Nzega Tabora ni watu wenye hali duni.

Tena kuna kitu kinakujaa kabisa unaamini watu wa Tanga wanakula bata gani bwana? Kuna nini cha ajabu Tanga? Kwanza kule Rami yenyewe ya magumashi.

Kumbe Hapo Dar ulicho nacho ni Geto la Chumba Master, Sebule na Jiko, TV ya Nchi 50, Saboofa la Aborder na Mademu kama wawili hivi wa kubadilisha badilisha na wanakugombania.

Huku Mkoani Nachingwea, Dumila, Handeni na Rufiji Vijana wana miliki Mamilioni ya Fedha na Miradi kadhaa isiyohamishika yenye thamani mpaka 200M.

We mali zako hazifiki hata 10M na hilo Duka lako la Mpesa, Tigopesa, halopesa etc.

Huku watu wanakula Bata si la Nchi hii. Wana Majumba mazuri, watoto wa kwenda.

Magari ya kufa mtu ya kifahari hata kama hayafiki 50M lakini hizi za 15M, 18M, 20-25M hadi 45M zipo za kumwaga.

Wewe unajidai mademu wawili wamejaa Enjoface na Macream huku watu wanapiga hadi 8 Kuku wa Kienyeji.

Kwenye Biashara ndio usiseme. Mshindo mmoja tu unatoboa maisha.
Vice versa is true
 
Nafungua Uzi kwa kusema Dar es salaam ni mkoa kama mikoa mingine, nashangaa mnavyoikuza kanakwamba ni paradiso kiasi cha kusema kuna Dar na mikoani.
Huo msemo wa Dar na mikoani naomba muufute kwa maana Dar ni mkoa.
 
Ushauri uliojaa manung'uniko😂😂😂 Daslam yenyew haihitaji VISA kwenda na bado mnalalamika.Ingekuwa ukifika Mbezi Luis unaombwa passport mbona mngepasuka sana.

Asiwadanganye mtu hata matajiri wa mikoani huwa hawakauki Daslam.Hizo ngebe za kumiki sijui vitu gani vya huko kolomije haifikii hadhi ya Kiwanja cha 20×20 kwenye jiji la Chalamila.

Daslam ndio mji wenye hadhi Tz yote, huko kwingine kunahesabika kama nchi jirani na Tz( Daslam).
Sasa ww huna mtaji na mambo yenyewe unayaona yalivyo kwanini usizame mikoani ukalime Mihogo upate mtaji uludi dar ufanye kazi halali sio kukaba kaba Asilimia 70 ya wakazi wa DAR wanaishi kijanja janja tu hawana Cha kufanya na lait kama magu angekuwepo ujanja ujanja ulikuwa unawatokea puani WEWE NUNUA SIMU YA LAKI 8 Mimi laki. Nane nikinunua mbuzi 16 kwa mwaka wanazaa mara mbili nakuwa 32 halafu watoto nawo wanazaa safi huku mambo mengine yanaenda lakin sio mbaya
 
Hizi akili zenu za kwenye makaratasi zingekuwa sahihi wote mnaoikashifu Daslam mngekuwa mabilionea.

Hayo magazijuto unayopiga hapo ukiwa na njaa wenzako wengi tu waliyapiga na mpaka kesho wapo apeche alolo.Bwanamdogo Daslam ni mji wa kipekee kama ukishindwa kuishi Dar wewe utakuwa kiazi mbatata wa mwisho na hutaweza kuishi hata huko mikoani.

Huyo unayemsema alikuwa anakomesha mission town yeye mbona alikimbia chaki akaenda kwenye vieteee😂😂😂 kijana acha stori za pauka pakawa my friend usione mtu anaitwa tajiri ukazani anauza upuuzi upuuzi sijiu mikate na karanga.

Hapa duniani unatakiwa uwork smart not harder.Hard workers wote ni slaves na hawatatoka huko mpaka mwisho wa dunia.

Hela inafata mkondo hela haitaki kelele.Kaa vizuri na anza kusalimia watu utakula mema ya nchi.
 
Nafungua Uzi kwa kusema Dar es salaam ni mkoa kama mikoa mingine, nashangaa mnavyoikuza kanakwamba ni paradiso kiasi cha kusema kuna Dar na mikoani.
Huo msemo wa Dar na mikoani naomba muufute kwa maana Dar ni mkoa.
Jiji Tanzania ni moja tu Dar kwingine kote ni mikoani
 
Maisha yapo hivi,

Kwa mfano mtu asiye na Ajira anaamua kutokuja Dar, yaani jiji linakuwa na walioajiriwa tu

Nani atachimba shimo la taka,

Nani ataangusha miti,

Nani atafyeka kiwanja chako,

Nani huyo wa kuzibua vyoo vikijaa,

Nani huyo msomi aliyeajiriwa akuoshee passo yako,

Nani atatumwa kazi ili alipwe 5000 hadi 3000.

Nani atatembeza vitu unavyonunua ukiwa kwenye foleni.

Mungu anajua ndiyo maana hao uliowataja wapo mkoani na wengine wapo Dar na umasikini wao
 
Sasa hayo maisha mbona hawayapati..wanaishi kama wanyama. Mtu anakimbizana na magari kwenye jua kali kwenye barabara anauza maji au karanga ni mateso
Mtu anayekuja Dar es Salaam usiku na kuondoka mchana ni ngumu sana kuona kuwa Dar kuna fursa na Changamoto.Dar wako wanaoishi peponi na wanaopata shida.Ukienda mbeya hivyo hivyo,Morogoro hivyo hivyo,Arusha hivyo hivyo tena pale vijana wako loose loose.Kikubwa tafuta pesa usaidie wengine kwenye jamii yako usijikite kujilinganisha na rafiki yako anayeishi Dar.
 
Nilimjibu mwenzako hapo juu mimi mzaliwa wa Dar. Nimejenga Dar na nilirithi nyumba Dar tena prime area. Hivyo Dar ni my domicile yaani nazikwa Kisutu. Hapa tunajadili uchumi na kufanikiwa kimaisha, wengi wa mnaokuja mjini mnaishia umachinga na sasa hivi bodaboda au mnaishia kukata viuno kwenye bar ili kujikimu hayo si maisha.
Umeongea pumba
 
Sasa ww huna mtaji na mambo yenyewe unayaona yalivyo kwanini usizame mikoani ukalime Mihogo upate mtaji uludi dar ufanye kazi halali sio kukaba kaba Asilimia 70 ya wakazi wa DAR wanaishi kijanja janja tu hawana Cha kufanya na lait kama magu angekuwepo ujanja ujanja ulikuwa unawatokea puani WEWE NUNUA SIMU YA LAKI 8 Mimi laki. Nane nikinunua mbuzi 16 kwa mwaka wanazaa mara mbili nakuwa 32 halafu watoto nawo wanazaa safi huku mambo mengine yanaenda lakin sio mbaya
sio rahisi hivyo kama unavyodhani
 
Back
Top Bottom