Ukiwa Dar es Salaam unaweza kudhani maisha umeyapatia, kumbe umechelewa sana bila kujua

Inanihusu pale ambapo muda anaoupoteza huleta ushawishi kwa wengine ili waupoteze kama yeye..Mm ni sehemu ya jamii,siwezi kujitenga nayo wakati tunaishi kwa kutegemeana
Hapana,

Wewe unataka ku control watu katika maisha yao waishi kama wewe unavyotaka na si kama wao wanavyotaka.

Watu wakiamua kupoteza nuda wao ni haki yao.

Kwani wamekulazimisha wewe kupoteza nuda waki?

Hiyo ni fursa kwako, wakipoteza muda wewe fanya kazi unazotaka bila ya mashindano kutoka kwao.
 
Stori yako umeigeuza juu chini...ukikaa mkoani ukamiliki Raum na nyumba unaonekana una maisha ila Nenda Mjini uone mbweni,masaki, mbezi beach na pengineo utajua mikoani hakuna matajiri wapo watu wenye hela ya kula.
 
Hahaa jamaa ana assumptions za uongo
Ndio hapo ni ngumu mtu wa Dar kumtambia maisha mtu mkoani hasa akiwa hajafanya chochote home. Maana Kuna muda watu huwa wanajuta kwanini wapo mjini Bora wangeishi shamba.

Sema watu wa mikoani huwa ndo huwa wanahizo assumption kuwa watu wa Dar wamefanikiwa hivo kuanza kuwatolea maneno ya shombo

Kwasababu kama mafanikio inabidi wajiuluze wote waliopo mikoani wamefanikiwa?
 
Kama nakuelewa vile!
 
Zitafute zilipo hiyo sio kazi yangu,kama ni NBS au wewe mwenyewe sawa
Ila mm nazungumzia uhalisia mtaani
Mtaani wapi huko? Hizi hoja zinaongelewa sana na wasio wakazi wa dar sijui ni kwanini.

Dar pamechangamka kifursa kuanzia level ya chini ya maisha mpaka level ya juu. Kuna sehemu kuitafuta elfu 5 kwa siku ni mtihani sana.
 
Hawajiamini
 
Hizo ni imani potofu mkuu.Mtu ukiwa Dar es salaam au ukiishi Ulaya ndugu zetu hutuchukulia kama tumeshatoka kimaisha. Mara nyingi wengi hudanganyika na life style yetu tunapokuja mapumziko huko nyumbani, ukweli ni kwamba huwa tumejipanga kwa kipindi hicho na maisha mnayoyaona kwa wakati huo yalikuwa budgetted before. Kumbukeni mengi tunayoyaona au kuyasikia katika dunia hii siyo halisi ishini maisha yenu.
 
You are Right
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…