jaap
JF-Expert Member
- Dec 25, 2018
- 4,888
- 6,459
Mkuu huyo mwanamke anayefanya hivyo inategemea mila na tamaduni zao, kila jamii ina mila na tamaduni zake kwaiyo unapotaka kuoa mwanamke jaribu kujua mila na tamaduni zao zipo je, kuna baadhi ya makabila mtoto kike akishaolewa tu yeye anakuwa sehemu ya familia ya mume wake kwao alipo zaliwa na kuishi panakuwa siyo kwao tena kwao panakuwa upande wa mume, kwa hiyo mwanamke kama huyu hawezi kufanya mambo ya ajabu ajabu kwa mume kwasababu mume hana kazi au kafuzwa kazi na kama huyu mke ana kipato lazima atakuwa anampa mumewe na kufanya maendeleo pamoja ya familia.Mfumo wa sasa wa Dunia jinsia zote zinasoma na usishangae kukuta wanawake ndyo wasomi wengi kuliko hata wanaume.
Cha ajabu wanaajariwa na kulipwa mishahara wengine isitoshe wanalipwa mishahara mikubwa kuliko hata Waume zao.Cha ajabu hao wanawake hao wanaolipwa mishahara mikubwa wanategemea Waume zao katika Kila kitu pasipo kujali wana kipato Cha kawaida.
Mwanaume analipwa laki 5 Mwanamke analipwa milioni 2 lakini Mwanaume akiyumba kiuchumi huyu mwanamke Anamuona mwanaume wake mzigo na kumtukana.Pesa zake anazitoa Kwa uchungu.Sasa hizo pesa ulisoma zikusaidie nini kama unashindwa kumsaidia mume wako Kwa muda anapofelli kiuchumi.
## mwalimu wa wanawake haoni mbele