Ukiwa kijana Fanya biashara au shughuli ya kukutoa, sio kupoteza muda kwenye biashara za ovyo

Mkuu kama huna uwezo wa kupata kula unaweza kupata Luxuru life?

Hizo zenu kama hizi tulizipiga sana enzi tukiwa chuoni.

Tulipoingia field tulikuta mambo yako Tofauti.

Somo ni kwamba mtu ambaye hata kula tu ni shida atawezajw kuwaza Beyond?

Kila tajiri unayemwona au mfanyabiashara alianza chini.

Nyie inaonekana ni Kula kulala bure hata hamuelewi au mmeshiba hela za ccm mnawaona wengine ni wajinga.
 
Hizi ukiwa na malengo zinakuvusha. Kuna kijana mmoja ana boxer, ametengeneza cluster ya wateja wake, kazi yake huanza saa 10 alfajiri na kumalizika saa tatu asubuhi kila siku, anaingiza wastani wa elfu sitini kila siku. Kazi ya masaa 6.
 
Hatukatai kuanzia chini
Lakini angalia na chini penyewe
Binafsi nitamheshimu winga wa Kariakoo ambaye hana hata 100 ila anatafuta wateja anauza, anapata maarifa ya wap bidhaa zipo za bei nafuu, anapata connection na matajiri wenye stoo kubwa, anapata kucheza na bei huyo ni rahisi kutoboa kuliko majina viatu au anayeuza supu ya utumbo Buguruni
 
wape mitaji wafanye biashara kama ambazo unafanya wewe, waachane na kuuza vitumbua bro!
 
Mkuu hoja zako nazikubali na sikudhani kama ningeeleweka tofauti.

Kuna wale watu ambao wamekaa pale pale miaka nenda rudi,sio kwa sababu nyingine bali ni kutokuwaza beyond

Hatusemei wale ambao tunajitafuta kupat mkate wa siku,huwezi kuhesabu moja nane kumi,lazima uende kwa hatua kama ulivyosema.

Kuna watu wao wanawaza biashara kama ajira,yaani hawawazi kwamba kesho mambo yanaweza kuwa kama sio leo...

Sijui umenipata mkuu ?
 
Dubai, mtungi wa laki 5, hata mwalimu hawezi fanya hivo
 
Haijalishi unafanya Nini!, hapa duniani unahitaji mtu tu akupoint hayo mengine ni makelele tu, sijui Smart, connection na ujinga ujinga mwengine
 
Kwahiyo mtaji wa tray moja ya mayai mabo ni elfu 10, inaweza kuanzisha shamba?
Mkuu Vijana wengi unaona wanazura Mitaani sijui kuuza uduvi, Kusajili Line kutembeza mayai wametoka Vijijini uko ambako kuna abundant ya Mashamba tena unakuta ni ya familia na hakuna watu wanayalima

Mfano kule kwetu sisi kuna Mito na Mazao mengi ya Biashara yanastawi ila Vijana wao mtu kulima zao la Biashara kwa kumwagilia maji avune aanze kujitanua pole pole anaona Ni mziki badala yake anaingia tamaa ya na yeye aje mjini ndio unamkuta anazagaa kusajili line au Kuuza tray moja ya mayai kwa siku.
 
Huna haki ya kusema kwamba wanofanya biashara hizo ni wajinga kwa sababu huwapi hela wewe, na kama unekuwa unawapa hela halafu hawafanyi kama unavyotaka wewe ndo tungesema una haki ya kuwalaumu na kuwaona wajinga..
Nasema watanue fikiria, si sawa Kwa kijana mwenye nguvu sio mgonjwa kukaa Kushona viatu au kuuza matiti kwenye deli.
Hana mtaji sawa lakini kufikiria vitu chanya vinaweza kumsaidia baadaye
 
Nasema watanue fikiria, si sawa Kwa kijana mwenye nguvu sio mgonjwa kukaa Kushona viatu au kuuza matiti kwenye deli.
Hana mtaji sawa lakini kufikiria vitu chanya vinaweza kumsaidia baadaye
Ni kweli kwamba wanatakiwa watanue fikra ila hawana watu wa kuwapush hata wakitanua fikra itakuwa kazi bure tu, maana pesa ndo inadetermine maisha yaendaje,

kuna watu wanawaza kujenga nyumba za maana lakini hawana pes wanaishia kujenga nyumba za miti na tope,
kuna watu wanaamini wakianza na kazi hizo mdogo mdogo watakusanya pesa ya biashara kubwa lakini ndo hivo hawapati

NB: SHUKURU MUNGU KWA HIKO KIDOGO ALICHOKUPA MA SIO KUANZA KUJILINGANISA NA WENGINE NA KUONA NJIA ZAO ZA KUTAFUTA PESA HAZIFAI KISA ZINAINGIZA PESA KIDOGO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…