Ukiwa kijana Fanya biashara au shughuli ya kukutoa, sio kupoteza muda kwenye biashara za ovyo

Ukiwa kijana Fanya biashara au shughuli ya kukutoa, sio kupoteza muda kwenye biashara za ovyo

Sehemu kubwa ya maisha ni kupambana na changamoto, mada imeibua changamoto bila njia za kujikwamua kutokana na changamoto iliyoibuliwa. Wachangiaji pia wanapita humo humo.
Suluhu ni kuwaasa wafikirie biashara itakayokuwa na kwenda mbali.
 
ukweli mtupu vijana akili mgando nina vijana nawajuwa tangu nasoma mpaka namaliza around 2014 naingia kitaa bado wana mishe hiyo hiyo tena boda boda sio zao ni za boss na mimi kwa sasa hawaniwezi japo japo kwenye maisha kuna mda tunakutana na bahati
 
Ninamfahamu muuza chapati ambae ana uhakika wa kulaza 50+K kila siku anayofungua. Sijui huyu nae atakufa masikini ingali pesa hiyo ya eneo moja imeshampa biashara zaidi ya moja?

Hivi Bakhresa si anauza ice cream? Nae atakufa masikini sio?

NB: ulichokosea ni kutokujua kuwa baadhi ya biashara ulizozitaja hapo zikisimamiwa na kukuzwa zinaweza kuwa kubwa na kuondoa umasikini.
 
Ninamfahamu muuza chapati ambae ana uhakika wa kulaza 50+K kila siku anayofungua. Sijui huyu nae atakufa masikini pesa hiyo ya eneo moja imeshampa biashara zaidi ya moja?

Hivi Bakhresa si anauza ice cream? Nae atakufa masikini sio?

NB: ulichokosea ni kutokujua kuwa baadhi ya biashara ulizozitaja hapo zikisimamiwa na kukuzwa zinaweza kuwa kubwa na kuondoa umasikini.
Hujaelewa
Kuna kuuza chapati au kitumbua katika ubunifu utakaofanya mtu biashara iliwe.

Waza mjinga anayenunua Tikiti na kukata vipande na kuweka kwenye deli atakuwa huyo?
Au kijana ana nguvu anatembeza shanga Mburahati
 
Kosa lako ni kuisema biashara kiujumla. Ungesema mtu ambae hajiboreshi tangu mwanzo tungekuelewa.

Mfano, ukisema kilimo hakilipi ingali kuna watu wana maisha makubwa na hicho kilimo utakuwa umekosea mkuu. Hoja yako ilikuwa nzuri ila uwasilishaji wako haukuwa katika uhalisia.
 
Hizi ukiwa na malengo zinakuvusha. Kuna kijana mmoja ana boxer, ametengeneza cluster ya wateja wake, kazi yake huanza saa 10 alfajiri na kumalizika saa tatu asubuhi kila siku, anaingiza wastani wa elfu sitini kila siku. Kazi ya masaa 6.
Umesema vyema mkuu. Wapo boda wanalaza pesa nyingi kuliko baadhi ya wanaounga mkono hii hoja hapa mkuu. Shida si aina ya biashara. Shida ni mpangilio wa biashara husika.

Nilipo namjua mwamba anaeuza chapati si chini ya 500 kila siku. Na hapo anaifanya kazi hiyo kwa nusu ya siku tu.
 
Kosa lako ni kuisema biashara kiujumla. Ungesema mtu ambae hajiboreshi tangu mwanzo tungekuelewa.

Mfano, ukisema kilimo hakilipi ingali kuna watu wana maisha makubwa na hicho kilimo utakuwa umekosea mkuu. Hoja yako ilikuwa nzuri ila uwasilishaji wako haukuwa katika uhalisia.
Hakika upo sahihi
Nimesisitiza zaidi vijana wazingatie zaidi matumizi ya nguvu walizo nazo Sasa na akili.
Sio hekima kijana una nguvu umetoka mfano huku Kagera upo Dar es salaam unauza nyembe bar
 
Hakika upo sahihi
Nimesisitiza zaidi vijana wazingatie zaidi matumizi ya nguvu walizo nazo Sasa na akili.
Sio hekima kijana una nguvu umetoka mfano huku Kagera upo Dar es salaam unauza nyembe bar
Hapa umesema na ninapaunga mkono. Nguvu bila akili wakati mwingine haikusogezi. Hivi vitu vikiunganishwa mtu anaweza kupiga hatua kirahisi na kwa haraka sana.
 
Tuambizane ukweli ambao watu wengi huwa hatuambiani, Huwa tunafarijiana tu
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliwambia vijana huwezi kutoboa maisha Kwa kuuza uduvi, watu wakamwijia juu

Huo uvivu wa kukataa kumwaga jasho na kuumiza akili ndo hivo tunauwa vijana wanakosa ubunifu na kuishia kuwa masikini wa kutupwa

Kijana ukiwa na nguvu Fanya kazi au biashara Kwa bidii na tengeneza kesho yako

Kijana uliyekamilika usifanye biashara au shughuli zifuatazo

1. Kuuza genge
Kijana wa miaka 20/ 22/23, unajisifu kumiliki genge, yaani nguvu zako zote na akili unashinda unakata kabichi na kuuza kitunguu 100, lini utashika million 100, lini utaenda China au Dubai, lini utakaa baa ule mtungi wa laki 5
Kwanini usikimbie Kariakoo ukachukua mzigo wa nguo au cover A simu ukimbize chap upige faida ya maana

2 Kushona viatu
Kijana mwenye nguvu upo kibarazani unashona na kungarisha viatu.
Binafsi laZima ni kudharau nikikuta unafanya hii shughuli Dar es salaam

3. Kuchoma vitumbua
Kijana mwenye nguvu unaibuka na idea ya kuchoma vitumbua, utatoboa lini, fikiria biashara ya kukutoa mapema

4 Kuuza miguu ya kuku
Hii biashara inatakiwa wafanye wabibi, kijana mdogo unauzaje biashara ya mabibi kama hii
Amka acha uvivu Katie jasho upate pesa

5. Kuchemsha mayai
Kijana mjinga unatembea na trey ya mayai mtaani ati upo mjini unapambana, we ni jinga na pumbavu kwanini usije huku tukalime maharage na mahindi

6. Kuuza kahawa, tangawizi na kashata
Hapa kijana unajimaliza kifikira, jinga sana wewe Tanzania kubwa hivi, amani yote hii, unapata wazo la kutembeza kahawa kwenye birika.
Kwanini usifate kuku Morogoro,

7 kuchoma mahindi

8. Kuuza vipande vya matikiti kwenye deli
Yaani ununue Tikitiki ukate vipande kadhaa na eti ukawe tajiri

9 Kuuza supu ya utumbo na makongoro

10 kuuza dawa za mbu na sumu ya panya

Hizi ni baadhi ya biashara za kijinga ambazo kijana hupaswi kuzifanya
Ni mada nzuri, tatizo Moja tu; mbona hujazisema hizo biashara zenye kulipa?!!!!
 
Uzi wako hujakaa kushahuri.. uzi umekaa kidharau na kujiona wewe ndio umeshamaliza..

Kwani kuna kosa kijana kuanza kuuza chapati?
Chapati hazina shida ila shirikisho nguvu na akili ukue sio unakuwa mchoma chapati miaka 15
 
Umesema vyema mkuu. Wapo boda wanalaza pesa nyingi kuliko baadhi ya wanaounga mkono hii hoja hapa mkuu. Shida si aina ya biashara. Shida ni mpangilio wa biashara husika.

Nilipo namjua mwamba anaeuza chapati si chini ya 500 kila siku. Na hapo anaifanya kazi hiyo kwa nusu ya siku tu.
Upo sawa kabisa, Kwani pringles si ni viazi vile? Tofauti ya Baba halidi muuza chips na Fredric J. Baur aliyekuja na idea ya Pringles ni namna walivyovitazama viazi pengine na mtaji lakini wote ni wafanyabiashara wa viazi.

Nadhani tupeane motisha ya kutazama hizi hizi biashara zetu local kwa mtazamo tofauti na tunavyozitazama, pengine ikazalisha jambo tofauti.
 
Umesema vyema kabisa mkuu. Kwa sababu ukubwa wa biashara zote upo katika zinazoonekana biashara ndogo. Bakhresa si anauza ice cream? Tupeane motisha kwenye mtizamo chanya kama ulivyosema ndugu.

Namna tunavyotizama jambo ndio utofauti unapotokea.
 
Back
Top Bottom