Ukiwa kijana Fanya biashara au shughuli ya kukutoa, sio kupoteza muda kwenye biashara za ovyo

Ukiwa kijana Fanya biashara au shughuli ya kukutoa, sio kupoteza muda kwenye biashara za ovyo

Hivi kijana akiamka akaenda machinjioni Vingunguti akawa anafanya shughuli zake hapo hata kuuza ngozi na kwato Kuna mtaji wa milion ngapi, huyo Kijana anayekaa hapo ni rahisi hata akipata mtaji akaagiza ng'ombe karatu na akaanzia kuliko mtembeza kahawa hata akiwa na milion ataongeza tangawizi na iliki tu ili apike chai tamu
Siku moja mfate mchoma mahindi mmoja, au yule jamaa anayekuuziaga kahawa mpe hiyo idea atakushukuru sana, kuliko kuja kuandika mtandaoni huku kuhusu kazi hizo maana huku ni nadra sana kuwaata watu wa hivo coz huku jamiiforums na sio TikTok
 
Brother, chochote kile unachokiona mbele ya macho yako kinaweza kukutoa ama kukudidimiza. Hamna guarantee popote pale. Mali ni AKILI yako tu.

Kuna unachokidharau ila amini usiamini kuna mwenye akili alikitumia hikohiko akajikomboa na kufika ngazi fulani.

Mimi nikiwa nimesoma mpaka chuo kikuu, nilishangaa sana kuja kumkuta mshikaji tulosoma naye form four akafeli, eti anamiliki bajaji na pikipiki kadhaa barabarani. Hapo ilikuwa 2018.

Leo hii 2025 ninapoandika haya, ana bajaji kumi na kitu barabarani na pikipiki sijui ngapi, hata vijana walosoma wanamfuata kumwomba kazi ingali wakati ule alipofeli na kuanza kuendesha bodaboda tulikuwa tunamtumia kama mfano wa mtu aliyefeli maisha.


Hapo nikajifunza katika haya maisha, akili ndiyo MALI yenyewe na si vinginevyo.
Good 👍 bro
 
Screenshot_20250518_130942_WPS Office.jpg


Whatsapp: 0687746471/0612607426
 
Jamani hzo ni kweli lakini sio rahisi kufika huko kwa comfort zone kwa kijana anaetoka fMilia za kimaskini mnajua mkiwa na umasikini wa familia akili ina stuck kujua mambo nikupe mfano mnajitafutaaa zikija siku kuu au sherehe za kifamilia ela yote mna prune kwa sherehe sijui ngoma sijui nguo utanyanyukaje na hata akili haichaj ushaingia ww mageroni mwa vijana wa chini na kati mambo wanayomiliki wala hayawasaidii
 
Yaani vijana wetu sijui kwa nini huwa hawawazi vitu vikubwa[emoji30], imagine nchi za wenzetu kwa wazungu watoto wako grade 3 lakini wameanza kuwaza kua matajiri wakubwa, kufanya innovations kubwa kubwa, but huku kwenye wanawaza kuuza vipande vya tikiti kwenye deli? are we serious?

Aki ccm ni mashetani.
Mmiliki wa KFC aliwaza kuuza vipande vya kuku (chicken wings, chicken breast & drum sticks) sasa billionaire. Biashara yake ipo kila pande ya dunia.
Siyo kila mtu lazima afanye inventions. Hata huko kwa wazungu siyo kila mtu anavumbua vitu vikubwa tu.
Mc Donald's wanapika vyakula tu ila matajiri wakubwa sana.
 
Mmiliki wa KFC aliwaza kuuza vipande vya kuku (chicken wings, chicken breast & drum sticks) sasa billionaire. Biashara yake ipo kila pande ya dunia.
Siyo kila mtu lazima afanye inventions. Hata huko kwa wazungu siyo kila mtu anavumbua vitu vikubwa tu.
Mc Donald's wanapika vyakula tu ila matajiri wakubwa sana.
nimemaanisha hawa wetu hawawazi kwa ukubwa. David Sanders muanzilishi wa kfc kwanza alikua anatengeneza fried chicken kwenye mgahawa mdogo, then akawa anaweka spices ambazo anapenda ili nyama ya kuku itoke tofauti, watu wakapenda sana kuku zake mgahawa wake ukawa maarufu sana na akatajirika sana, then later akaanza kufungua braches sehemu tofauti tofauti then akaruhusu franchise ambazo zimesambaa duniani kote.

Hivo elewa,utofauti huu sasa. Alikua mfanyabiashara mdogo wa nyama za kuku. Then akafikiria anaboreshaje biashara yake ? akatafuta spices nzuri anazizipenda akaziongeza kwene nyama, then akabuni style nzuri ya kuzikaanga ziwe crunch kutafuna. Ubunifu huo ukapendwa na umeifanya KFC kuwepo duniani kote leo hii.

Sasa wakwetu hawana ule moyo wa kukuza biashara zao kwa ubunifu zaidi, sababu akiuza mishkaki akapata elf 5 au alf 10 ya kula anaridhika, anabaki kuuza mshkaki ule ule miaka hata 5+ anauza tu mishkaki kwa mtindo ule ule iilimradi anakula anavaa malonya, amepanga au kajenga tuvyumba tuwili baaasi hafikirii kukua zaidi.

I hope umeelewa utofauti.
 
Endelea kufua nguo za shemeji yako,

Kikubwa humpi mtu kula, wala pa kulala acha kiherehere na maisha ya watu,
 
Namba 9 nakupinga biashaea ya kongoro inapesa nina ushahidi yakinifu nina mwanafamilia anafanya io kwasiku analza 20k faida , pia kuna kazi ukifanya kutoboa sahau
Ulinzi
Usafi
Viwandani
Na zotee zisizo na marupurupu
 
Tuambizane ukweli ambao watu wengi huwa hatuambiani, Huwa tunafarijiana tu
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliwambia vijana huwezi kutoboa maisha Kwa kuuza uduvi, watu wakamwijia juu

Huo uvivu wa kukataa kumwaga jasho na kuumiza akili ndo hivo tunauwa vijana wanakosa ubunifu na kuishia kuwa masikini wa kutupwa

Kijana ukiwa na nguvu Fanya kazi au biashara Kwa bidii na tengeneza kesho yako

Kijana uliyekamilika usifanye biashara au shughuli zifuatazo

1. Kuuza genge
Kijana wa miaka 20/ 22/23, unajisifu kumiliki genge, yaani nguvu zako zote na akili unashinda unakata kabichi na kuuza kitunguu 100, lini utashika million 100, lini utaenda China au Dubai, lini utakaa baa ule mtungi wa laki 5
Kwanini usikimbie Kariakoo ukachukua mzigo wa nguo au cover A simu ukimbize chap upige faida ya maana

2 Kushona viatu
Kijana mwenye nguvu upo kibarazani unashona na kungarisha viatu.
Binafsi laZima ni kudharau nikikuta unafanya hii shughuli Dar es salaam

3. Kuchoma vitumbua
Kijana mwenye nguvu unaibuka na idea ya kuchoma vitumbua, utatoboa lini, fikiria biashara ya kukutoa mapema

4 Kuuza miguu ya kuku
Hii biashara inatakiwa wafanye wabibi, kijana mdogo unauzaje biashara ya mabibi kama hii
Amka acha uvivu Katie jasho upate pesa

5. Kuchemsha mayai
Kijana mjinga unatembea na trey ya mayai mtaani ati upo mjini unapambana, we ni jinga na pumbavu kwanini usije huku tukalime maharage na mahindi

6. Kuuza kahawa, tangawizi na kashata
Hapa kijana unajimaliza kifikira, jinga sana wewe Tanzania kubwa hivi, amani yote hii, unapata wazo la kutembeza kahawa kwenye birika.
Kwanini usifate kuku Morogoro,

7 kuchoma mahindi

8. Kuuza vipande vya matikiti kwenye deli
Yaani ununue Tikitiki ukate vipande kadhaa na eti ukawe tajiri

9 Kuuza supu ya utumbo na makongoro

10 kuuza dawa za mbu na sumu ya panya

Hizi ni baadhi ya biashara za kijinga ambazo kijana hupaswi kuzifanya

Kazi inahitaji Akili, ubunifu, ubora, Wateja.
Hizo KAZI zote zina watu wanapesa kukushinda kwa KAZI hizohizo.

Inategemea unafanyaje
 
Mimi nimeshakutana na kijeba pande la mtu linauza kata kucha nne linazunguka bar hadi bar nyingine. Ukisema ununue katakucha zote nne ni elfu kumi na mbili. Kwakweli hayo ni matumizi mabaya ya nguvu. Vijana tubadilike tuache ujinga
Tena kama huyo ukute kaaga kwao Tandahimba au Simuyu ati akatafute maisha mjini
Kumbe jitu lipo linatembeza nyembe za kucha, limeacha ardhi na mapori kwao
 
Back
Top Bottom