Ukiwa kijana Fanya biashara au shughuli ya kukutoa, sio kupoteza muda kwenye biashara za ovyo

Hivi kijana akiamka akaenda machinjioni Vingunguti akawa anafanya shughuli zake hapo hata kuuza ngozi na kwato Kuna mtaji wa milion ngapi, huyo Kijana anayekaa hapo ni rahisi hata akipata mtaji akaagiza ng'ombe karatu na akaanzia kuliko mtembeza kahawa hata akiwa na milion ataongeza tangawizi na iliki tu ili apike chai tamu
 
Fedha Zina macho na miguu!!

UUkionaukoo umedumu na utajiri ujue Kuna Siri kuu zaidi ya kufanya kazi kwa bidii pekee!!

Kuna mstari umechorwa wa kiwango Cha wewe kumiliki pesa!ukizidi lazima ujiunge nao wenye Siri zao!

Ukiona wewe ni tajiri na Bado hujapata changamoto ya kufuatiliwa ujue una Hela ya mboga tu!!

RIP Rama wa Kariakoo!!
 
Fafanua zaidi wenye siri zao kina nani mkuu
 
Sio dharau, jamaa kaandika ukweli mchungu.

Ki mtazamo wako unaweza ona jamaa ana dharau ila alicho andika ni sahihi, huwezi kupata pesa za kukufanya uwe sonko kwa hizo biashara. Hizo kazi utapata pesa za kula na kubadilisha viwalo, ila kama unataka mapesa mengi inabidi ubadili mawazo.

Sio kudharau ila ni ngumu sana, vijana tumieni akili zenu vizuri. Ingieni chaka huko pambanieni kesho yenu, acheni kulaza akili zenu.
Acha dharau bata ww
 
Bajaji ikiwa yako binafsi na ukajitambua na ukajua nini unafanya ni miaka miwili tu wewe ni sonko. Inshu ya ulemavu popote pale unapata ata kama husukumi hiyo kitu, ajali haina kinga. Acha mawazo mgando.
 
Unaweza kukuta wewe Ni masikini kuliko jamaa anaitwa Mick aliekuja mjini Dar na kuajiriwa kuuza kahawa Kariakoo akapata mtaji akaanza kuuza ya kwake akaajiri vijana na yeye.
Akapata pesa ya kujenga nyumba Kitunda, akafungua duka kubwa.
Usidharau kazi inayompa mtu ridhiki.
 
Ni ukweli mchungu, mwenye akili timamu kakuelewa.

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Yaani vijana wetu sijui kwa nini huwa hawawazi vitu vikubwa[emoji30], imagine nchi za wenzetu kwa wazungu watoto wako grade 3 lakini wameanza kuwaza kua matajiri wakubwa, kufanya innovations kubwa kubwa, but huku kwenye wanawaza kuuza vipande vya tikiti kwenye deli? are we serious?

Aki ccm ni mashetani.
 
2 Kushona viatu
Kijana mwenye nguvu upo kibarazani unashona na kungarisha viatu.
Binafsi laZima ni kudharau nikikuta unafanya hii shughuli Dar es salaam
Mzee Bakhresa wa Azam alianza biashara ya kushona viatu Kariakoo, kisha kuuza ice cream.
Sasa hivi tajiri anaeweza kulisha ukoo wenu wote maisha yenu yote.
 
Brother, chochote kile unachokiona mbele ya macho yako kinaweza kukutoa ama kukudidimiza. Hamna guarantee popote pale. Mali ni AKILI yako tu.

Kuna unachokidharau ila amini usiamini kuna mwenye akili alikitumia hikohiko akajikomboa na kufika ngazi fulani.

Mimi nikiwa nimesoma mpaka chuo kikuu, nilishangaa sana kuja kumkuta mshikaji tulosoma naye form four akafeli, eti anamiliki bajaji na pikipiki kadhaa barabarani. Hapo ilikuwa 2018.

Leo hii 2025 ninapoandika haya, ana bajaji kumi na kitu barabarani na pikipiki sijui ngapi, hata vijana walosoma wanamfuata kumwomba kazi ingali wakati ule alipofeli na kuanza kuendesha bodaboda tulikuwa tunamtumia kama mfano wa mtu aliyefeli maisha.


Hapo nikajifunza katika haya maisha, akili ndiyo MALI yenyewe na si vinginevyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…