Xiao qui shui
JF-Expert Member
- Feb 26, 2022
- 6,461
- 11,345
Siku moja mfate mchoma mahindi mmoja, au yule jamaa anayekuuziaga kahawa mpe hiyo idea atakushukuru sana, kuliko kuja kuandika mtandaoni huku kuhusu kazi hizo maana huku ni nadra sana kuwaata watu wa hivo coz huku jamiiforums na sio TikTokHivi kijana akiamka akaenda machinjioni Vingunguti akawa anafanya shughuli zake hapo hata kuuza ngozi na kwato Kuna mtaji wa milion ngapi, huyo Kijana anayekaa hapo ni rahisi hata akipata mtaji akaagiza ng'ombe karatu na akaanzia kuliko mtembeza kahawa hata akiwa na milion ataongeza tangawizi na iliki tu ili apike chai tamu
Good 👍 broBrother, chochote kile unachokiona mbele ya macho yako kinaweza kukutoa ama kukudidimiza. Hamna guarantee popote pale. Mali ni AKILI yako tu.
Kuna unachokidharau ila amini usiamini kuna mwenye akili alikitumia hikohiko akajikomboa na kufika ngazi fulani.
Mimi nikiwa nimesoma mpaka chuo kikuu, nilishangaa sana kuja kumkuta mshikaji tulosoma naye form four akafeli, eti anamiliki bajaji na pikipiki kadhaa barabarani. Hapo ilikuwa 2018.
Leo hii 2025 ninapoandika haya, ana bajaji kumi na kitu barabarani na pikipiki sijui ngapi, hata vijana walosoma wanamfuata kumwomba kazi ingali wakati ule alipofeli na kuanza kuendesha bodaboda tulikuwa tunamtumia kama mfano wa mtu aliyefeli maisha.
Hapo nikajifunza katika haya maisha, akili ndiyo MALI yenyewe na si vinginevyo.
Mmiliki wa KFC aliwaza kuuza vipande vya kuku (chicken wings, chicken breast & drum sticks) sasa billionaire. Biashara yake ipo kila pande ya dunia.Yaani vijana wetu sijui kwa nini huwa hawawazi vitu vikubwa[emoji30], imagine nchi za wenzetu kwa wazungu watoto wako grade 3 lakini wameanza kuwaza kua matajiri wakubwa, kufanya innovations kubwa kubwa, but huku kwenye wanawaza kuuza vipande vya tikiti kwenye deli? are we serious?
Aki ccm ni mashetani.
nimemaanisha hawa wetu hawawazi kwa ukubwa. David Sanders muanzilishi wa kfc kwanza alikua anatengeneza fried chicken kwenye mgahawa mdogo, then akawa anaweka spices ambazo anapenda ili nyama ya kuku itoke tofauti, watu wakapenda sana kuku zake mgahawa wake ukawa maarufu sana na akatajirika sana, then later akaanza kufungua braches sehemu tofauti tofauti then akaruhusu franchise ambazo zimesambaa duniani kote.Mmiliki wa KFC aliwaza kuuza vipande vya kuku (chicken wings, chicken breast & drum sticks) sasa billionaire. Biashara yake ipo kila pande ya dunia.
Siyo kila mtu lazima afanye inventions. Hata huko kwa wazungu siyo kila mtu anavumbua vitu vikubwa tu.
Mc Donald's wanapika vyakula tu ila matajiri wakubwa sana.
Kwahiyo mtaji wa tray moja ya mayai ambayo ni elfu 10, inaweza kuanzisha shamba?
NAKAZIA MKUU....Mshukuru sana Mungu kwa kuweza kuanzisha biashara unazoona ni za maana. Usitukane wakungu...
Maisha ni safari ndefu
Tuambizane ukweli ambao watu wengi huwa hatuambiani, Huwa tunafarijiana tu
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliwambia vijana huwezi kutoboa maisha Kwa kuuza uduvi, watu wakamwijia juu
Huo uvivu wa kukataa kumwaga jasho na kuumiza akili ndo hivo tunauwa vijana wanakosa ubunifu na kuishia kuwa masikini wa kutupwa
Kijana ukiwa na nguvu Fanya kazi au biashara Kwa bidii na tengeneza kesho yako
Kijana uliyekamilika usifanye biashara au shughuli zifuatazo
1. Kuuza genge
Kijana wa miaka 20/ 22/23, unajisifu kumiliki genge, yaani nguvu zako zote na akili unashinda unakata kabichi na kuuza kitunguu 100, lini utashika million 100, lini utaenda China au Dubai, lini utakaa baa ule mtungi wa laki 5
Kwanini usikimbie Kariakoo ukachukua mzigo wa nguo au cover A simu ukimbize chap upige faida ya maana
2 Kushona viatu
Kijana mwenye nguvu upo kibarazani unashona na kungarisha viatu.
Binafsi laZima ni kudharau nikikuta unafanya hii shughuli Dar es salaam
3. Kuchoma vitumbua
Kijana mwenye nguvu unaibuka na idea ya kuchoma vitumbua, utatoboa lini, fikiria biashara ya kukutoa mapema
4 Kuuza miguu ya kuku
Hii biashara inatakiwa wafanye wabibi, kijana mdogo unauzaje biashara ya mabibi kama hii
Amka acha uvivu Katie jasho upate pesa
5. Kuchemsha mayai
Kijana mjinga unatembea na trey ya mayai mtaani ati upo mjini unapambana, we ni jinga na pumbavu kwanini usije huku tukalime maharage na mahindi
6. Kuuza kahawa, tangawizi na kashata
Hapa kijana unajimaliza kifikira, jinga sana wewe Tanzania kubwa hivi, amani yote hii, unapata wazo la kutembeza kahawa kwenye birika.
Kwanini usifate kuku Morogoro,
7 kuchoma mahindi
8. Kuuza vipande vya matikiti kwenye deli
Yaani ununue Tikitiki ukate vipande kadhaa na eti ukawe tajiri
9 Kuuza supu ya utumbo na makongoro
10 kuuza dawa za mbu na sumu ya panya
Hizi ni baadhi ya biashara za kijinga ambazo kijana hupaswi kuzifanya
Sawa mkuuSiku moja mfate mchoma mahindi mmoja, au yule jamaa anayekuuziaga kahawa mpe hiyo idea atakushukuru sana, kuliko kuja kuandika mtandaoni huku kuhusu kazi hizo maana huku ni nadra sana kuwaata watu wa hivo coz huku jamiiforums na sio TikTok
Hata na hivyo ni vijana wachache sana wa umri huo wa miaka 20/22/23 ambao utawakuta wakihishughulisha, Wengi wanajua kula bata tu, kutulia maghetoni na kufukuzia warembo [emoji3]
Tena kama huyo ukute kaaga kwao Tandahimba au Simuyu ati akatafute maisha mjiniMimi nimeshakutana na kijeba pande la mtu linauza kata kucha nne linazunguka bar hadi bar nyingine. Ukisema ununue katakucha zote nne ni elfu kumi na mbili. Kwakweli hayo ni matumizi mabaya ya nguvu. Vijana tubadilike tuache ujinga