Ukiwa mtumishi wa umma hakikisha kila wiki unatengeneza fedha sawa na mshahara wako wa mwezi mmoja

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Huu ni ushauri tu kwa watumishi.
Kutokana na kupigwa na vitu vizito kichwani kama vile Sheria mpya za kikokotoo, na danadana za ongezeko la mshahara pamoja na serikali kushindwa kukopesha watumishi wake bila riba au kwa riba isiyozidi 5% napenda kuwashauri watumishi wa umma wahakikishe chini juu kila wiki wafunge na hesabu ya mshahara wa mwezi mmoja.

Kama unalipwa laki 8 basi kwa mwezi makusanyo yako nje ya mshahara yagote 3.2 ml.

Kama mshahara wako laki 6 basi ikimbize milioni 2.4.

Kama mshahara wako ni milioni 1 basi ikimbize milioni 4 ndani ya mwezi.

Hii itakusaidia kujipanga na maisha baada ya kustaafu.

Hii itakusaidia pia kuishi kwa furaha wewe na familia yako kama wanavyoishi wanasiasa.

Utaipata wapi hiyo Mimi hainihusu.

Hakikisha tu unaingiza 400% ya mshahara wako kila mwezi.

Kuna Mzee mmoja kastaafu mwaka mwezi Machi.

Anazimia hovyo hovyo, sukari imepanda , pressure imepanda. Kikokotoo kimemkokotoa. Kama angekuwa makini kwenye biashara za ujasiriamali asingefikia huko.

Fanyeni ujasiriamali watumishi 😭😭😭😭.
 
Auze vitafunwa kwa wanafunzi wake. Kwa walio mjini kwa walio kijijini hapo kilimo hakiepukiki
Kila mualimu akianza kuuza ubuyu na maandazi wako waalimu 20 kwenye shule naani atanunua? Tena ukweli ni kwamba watoto wengi hawaji na pesa za kula katika shule za ummah wengi hutoka kaya masikini kupewa 500 ya barafu ni kipengera nyumbani
 
Kwamfano mualimu grade A mwenye mshahara wa 370,000 mwenye familia ya watoto wawili na mke anae hitajika kazini kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 8 jioni afanye ujasiliamali gani
Na sio saa nane, ni saa tisa na nusu ndo tunatoka kazini, mpaka kufika nyumban around saa kumi hivi.!
Fanyeni kunichangia mawazo na fedha Mwalimu wa watoto wenu niishi jamani.!
 
Huu ni ushauri tu kwa watumishi.
Kutokana na kupigwa na vitu vizito kichwani kama vile Sheria mpya za kikokotoo, na danadana za ongezeko la mshahara pamoja na serikali kushindwa kukopesha watumishi wake bila riba au kwa riba isiyozidi 5% napenda kuwashauri watumishi wa umma wahakikishe chini juu kila wiki wafunge na hesabu ya mshahara wa mwezi mmoja.

Kama unalipwa laki 8 basi kwa mwezi makusanyo yako nje ya mshahara yagote 3.2 ml.

Kama mshahara wako laki 6 basi ikimbize milioni 2.4.

Kama mshahara wako ni milioni 1 basi ikimbize milioni 4 ndani ya mwezi.

Hii itakusaidia kujipanga na maisha baada ya kustaafu.

Hii itakusaidia pia kuishi kwa furaha wewe na familia yako kama wanavyoishi wanasiasa.

Utaipata wapi hiyo Mimi hainihusu.

Hakikisha tu unaingiza 400% ya mshahara wako kila mwezi.

Kuna Mzee mmoja kastaafu mwaka mwezi Machi.

Anazimia hovyo hovyo, sukari imepanda , pressure imepanda. Kikokotoo kimemkokotoa. Kama angekuwa makini kwenye biashara za ujasiriamali asingefikia huko.

Fanyeni ujasiriamali watumishi 😭😭😭😭.
Unafundisha watu kuwa wezi?
 
Back
Top Bottom